Huu ulikuwa mlango mkuu wa kuingilia katika ngome ya Mtemi Isike mwana Kiyungi iliyoitwa Isyunula mnamo 1890. Katika kuwajengea uelewa mpana warembo wa Redds Miss Tabora 2013 wikiendi iliyopita walipelekwa Kwihara lilipo tembe la mvumbuzi maarufu duniani Dr David Livingstone na pia walipata fursa ya kutembelea mabaki ya iliyokuwa ngome (Ikulu) ya Mtemi maarufu wa Unyanyembe Mtemi Isike mwana Kiyungi ambaye alipigana na Wajerumani na kuwashinda kwa miaka 5 mpaka wajerumani walipotuma mamluki wa Kiarabu kuisoma ngome hiyo ndipo walipofanikiwa kuishambulia kwa mizinga ambapo Mtemi huyo shujaa wa Unyanyembe kabla ya kukamatwa na Wajerumani akakusanya familia yake wakiwemo wake zake na jeshi lake wakajifungia ndani akajiripua na baruti na kufa, kwani aliona bora kufa kuliko kukamatwa na wakoloni. Mungu amlaze mahala pema peponi shujaa huyu! |