11/11/13

Nyawana kuzikwa kesho Tabora!

NYAWANA |Mama wa matashititi enzi za uhai wake
MULARD | MUME WA ZAMANI WA NYAWANA [CHANZO CHA PICHA]

Mwanamuziki maarufu wa Taarabu marehemu Nyawana Fundikira anatarajiwa kuzikwa kesho mchana au jioni kutegemeana na uwasili wa mwili wa marehemu mkoani Tabora. Ambapo baada ya kufanyiwa yale yote muhimu mkoani Dar mwili wake utasafirishwa kwa njia ya gari mpaka mjini Tabora kwa mazishi.



Mazishi yake yatafanyika kijijini kwao Itetemya yalipo makaburi na Ikulu ya familia ya kichifu ya Fundikira na Mtemi Isike Mwana Kiyungi. Nyawana Fundikira ambaye ameacha watoto wawili Said Murad (22) na Queen Murad (15) ambao alijaliwa kuwapata katika ndoa yake yake ya kwanza na Bw. Omar Khamis Murad (pichani). Murad mwanamichezo maarufu sana mjini Tabora ni meneja wa uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.

Breaking news! Mwanamuziki wa Taarabu Nyawana Fundikira afariki dunia mchana huu!

Mama Nyawana enzi za uhai wake
Mwanamuziki wa muziki wa taarab Nyawana Isale au Maarufu Nyawana Fundikira aka Mamaa Matashtiti amefariki leo hii mchana jijini Dar es Salaam alipokuwa akikimbizwa hospitalini baada kuzidiwa Inafahamika kuwa ameugua Malaria kwa siku kadhaa, kwa habari zaidi kuhusu kifo chake na mazishi tutaendela kujuzana humu na kwingineko. RIP mwanawane Nyawana!

Picha kwa hisani ya taarabuzetublog!

Duniani kuna mambo!

Hawa nao wakatoa yao kali chini ya bahari.

Baadhi ya watu wamekuwa wakipenda siku yao muhimu katika maisha yao iwe ya kukumbukwa daima. Kwa mfano wengi wamefunga ndoa zao katika mazingira ya ajabu na wengine wamekwenda mbali zaidi na kuamua kufunga pingu za maisha wakiwa uchi wa mnyama. Bi harusi Shelley Davie na Bwana harusi Josh Hughes wa Melbourne, Australia wao walitoa kali zaidi pale walipooana wakiwa uchi kabisa.

Josh Hughes na Shelley Davie wakifunga pingu za maisha uchi.