06/15/15

Prof Mark Mwandosya asaka wadhamini Kilimanjaro


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais(Kazi Maalum) Prof,Mark Mwandosya mara baada ya kufika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaro wakati akiwa njiani kutafuta wadhamini.
Prof,Mwandosya akiteta jambo na RC Gama mara baada ya kukutana.
Prof,Mark Mwandosya akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi ,Angela Kairuki walipokutana katika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimpatia kipaza sauti Prof Mwandosya asalimie wajumbe waliokuwa katika ukumbi huo.
Profesa Mwandosya akizungumza katika ukumbi huo.
Prof Mwandosya akitoka katika ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Kilimanjaromara bada ya kusalimia.
Prof, Mwandosya akiagana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama mara baada ya kusalimia .
Prof,Mark Mwandosya akiondoka ukumbini hapo kuendelea na safari ya kusaka wadhamini mkoani Arusha.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

Pamoja na kukosa tunzo ya Kili ki mizengwe Christian Bela apagawisha Tabora!

Christian Bella akijimwaga jukwaani.
Masaa machache baada ya kukosa kitatanishi tunzo ya wimbo bora wa mwaka katika Kili Music Awards Christian Bela (King of melodies) alipagawisha wapenzi wa muziki mjini Tabora alipoporomosha bonge la show akiwa na kundi zima la Malaika Band. Christian Bela alitarajiwa na  wadau wa muziki nchini kuwa angebeba tunzo hiyo bila ushindani mkubwa kutokana na wimbo wake wa Nani kama mama ambao aliomshirikisha Ommy Dimpoz kutamba sana katika vituo vyote vya redio na Runinga hapa nchini, lakini kama kawaida ya tunzo hizo zinazosimamiwa na BASATA na kudhaminiwa na kampuni ya utengenezaji bia ya Tanzania TBL zimekuwa zikilalamikiwa kila mwaka huku waanadaaji wakioneka kuweka pamba mbichi masikioni. Tunzo hiyo ya wimbo bora wa mwaka ilienda kwa wimbo wa Mwana wa msanii Ali Kiba. Onesho hilo lilifanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi Tabora.
Bella akifanya yake jukwaani.

Mashabiki wa Malaika Band wakpozi
Hapo sasa!


Baadhi ya mashabiki wakijmwaga!


Music Producer Dula K kulia na msanii Masha Kay kushoto wakiwa na mdau.

Wacha wee Benny Ngwasuma akijiachia



Papaa Allex Ntonge mwaya mwaya!

Picha na habari na Mkala Fundikira TBN CENTRAL ZONE