February 2014

Mama Agnes Matle Ngula afariki leo asubuhi!

Bibi Agnes Matle Ngula enzi za uhai wake
Aliyekuwa naibu waziri wa fedha  Bw Venance Ngula leo hii asubuhi amempoteza mkewe Bibi Agnes Matle Ngula ambaye alikuwa akiugua kwa muda sasa. Mtoto wa kwanza wa marehemu Wali Francis Ngula anayeishi New Jearsey America anatarajia kuwasili jijini Dar kwa mazishi ya mama yake mpendwa siku ya Alhamisi. Tutaendelea kujuzana mipango ya mazishi hpa na kwingine. Mungu ailaze pema peponi roho ya mama yetu mpendwa Mama Agnes Ngula.
AMEN!
Bw na Bibi Venance Ngula wakiteta jambo enzi za uhai wa Bibi Agnes Matle Ngula
Mama Ngula akibandikwa mabusu na mwanae Wali Francis Ngula na mkewe Enika Kombe Ngula muda mfupi baada ya harusi yao mwaka juzi .
Mtoto wa mwisho wa mama Agnes, Nancy Ngula akiwa na marehemu 
Bibi Agnes Matle Ngula enzi za ujana wake.
Francis Wali Ngula
Habari na picha kwa hisani ya Francis na Nancy Ngula

Shabiki wa Liverpooll auawa kwa kumkejeli shabiki wa Arsenal!

Raha iliyoje 5-1????
Shabiki wa miaka mingi wa Liverpool Anthony Mutheiya alikufa muda mfupi baada ya firimbi ya mwisho katika mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal jumamosi iliyopita baada ya kuchomwa kwa kisu na shabiki wa Arsenal aliyetambulika kama David Mwangi ambaye anadaiwa alikimbia eneo la tukio Marethe Bar mjini Meru, Kenya ambapo wawili hao walitazama mchezo huo pamoja, ilisemekana Mutheiya alimkejeli Mwangi kupita kiasi na kwa muda mrefu juu ya matokeo ya mchezo huo ambapo Mwangi akashindwa kuvumilia na ndipo alipochomoa kisu na kumchoma nacho Mutheiya ambaye alikimbizwa hospitali lakini akafariki baadaye. 

Obama na Beyonce wazushiwa jambo!

Mtandao wa dailystar.co.uk wa nchini Uingereza ambao ni maarufu kwa habari za kidaku, leo hii umechapisha habari ilizodaiwa na mwandishi wa habari Mfaransa Paschal Rostain kuwa gazeti linaloheshimika nchini Marekani la Washinton Post linatarajiwa kuandika habari kuwa the most powerful man in the world, Rais wa Amerika Bw Barack Obama ana mahusiano ya kimapenzi na mwimbaji Byonce Knowles ambaye ni mke wa mwanamuziki Jay-Z. Rostain alikaririwa akisema "Unajua katika siku hizi kuna habari kubwa inatarajiwa kuchapishwa na gazeti la Washington Post kuwa Obama na Beyonce wana uhusiano usiofaa, na akaongeza "Dunia nzima italiongelea hili sana" 

Lakini msemaji wa gazeti hilo Wasington Post Bw Kriss Coratti alipoulizwa juu ya habari hiyo akasema hana habari yeyote juu ya hilo ila akaongeza Rais Obama na mkewe wamekuwa na matatizo hivi karibuni, "Lakini sijui zaidi ya hapo"

Baada ya yote hayo Paschal Rostain sasa ameeleza kuwa hajawahi kusema kitu chochote ya Rais Obama na mkewe.

Beyonce  kupitia msemaji wake alikanusha madai hayo na kusema "Ni kichekesho". Hata hivyo inafahamika kuwa familia ya Obama ni rafiki na familia ya Beyonce Knowles ambapo Beyonce aliimba siku ya kuapishwa Barack Obama na vile vile aliimba katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Michelle Obama kutimiza miaka 50.
Ahsante sana kwa wimbo mzuri. Obama akimshukuru Beyonce siku ya kuapishwa kwake.
Siku ya kuapishwa Obama
Happily married; Beyonce na mumewe Jay-Z

Kwani timu yako ikifungwa goli tano lazima uanguke?

Baada ya timu ya Arsenal (The Gunners) jana kupokea kipigo kikali kilichoendana na maumivu makali cha goli 5-1 toka kwa timu ya Liverpool (Bwawa la maini) aka (Liverfools) kocha Arsene Wenger aliteleza na kuanguka nje ya stesheni ya treni ya LIVERPOOL LIME STREET akiwa anaelekea kupanda treni kuelekea London baada ya mchezo huo wa Barclays Premier league ambapo askari wawili walikimbilia kumuinua kutoka hapao alipoangukia. Wenger alionekana mwenye maumivu makali kufuatia mwereka huo ambapo mashabiki wengi wa Manchester United wamedhihaki wenzao wa Arsenal kuwa mwereka huo ni kiwewe cha kufungwa na Liverpool na hatimaye kupoteza uongozi wa ligi hiyo maarufu duniani.


Ouch!

Maumivu makali!
Pole baba,haya simama!

Picha kwa hisani ya Twitter/TSBible, habari kwa hisani ya mailonlne

Hanifa Fundikira ahitimu uzamili!

Mwanadada Hanifa Mdemu Fundikira leo hii katika chuo kikuu cha Northampton amehitimu shahada ya uzamili katika utalii  (Masters in Tourism management) Blog hii na blog mama Keronyingi blog zinachukua fursa hii kumpongeza bibi Fundikira kwa mafanikio haya makubwa ki elimu. Tunamtakia afya njema na mafanikio katika yote ayafanyayo.

Bibi Hanifa Mdemu Fundikira akipozi nje ya Chuo kikuu cha Northampton nchini England baada ya kuhitimu.