November 2015

Mkurugenzi wa Amana bank afunga wiki ya huduma kwa wateja tawi la Mwanza!

Mkurugenzi wa benki ya Amana  Dk Muhsin Masoud  akimkabidhi  zawadi mteja Yasmin Ismail Mussa kwa utunzaji bora wa fedha katika tawi la Mwanza.


Benki ya Amana leo hii imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo katika tawi la Mwanza mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud alitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wenye sifa tofauti tofauti kama ioneshavyo pichani. 

Mkurugenzi huyo alikutana na wateja mbali mbali tawini  hapo ili kubadilishana nao mawazo na pia kupokea maoni toka kwao katika kuboresha huduma kwa wateja wa benki hiyo pekee ya Ki Islamu nchini. 

Kilele hicho cha wiki ya huduma kwa wateja kimefanyika katika matawi yote ya benki hiyo ambayo kwa Dar es Salaam ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na Main, vile vile Arusha na Mwanza.
Mkurugenzi wa Amana Bank Dk Muhsin Masoud akimzawadia Bw Juma Kivuruga kwa kuwa mfanyakazi bora kwa tawi la Mwanza, Kivuruga alipigiwa kura na wafanyakazi wenziye wa tawi hilo.
Daud Lweno akizawadiwa na Mkurugenzi wa Amana Bank kama mteja mzuri kulipia miamala ya TRA katika tawi la Mwanza.
Mteja Yasmin Ismail akikata keki ya kuadhimisha miaka minne tangu kufunguliwa kwa benki hiyo, huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao wakifuatilia tukio hilo kwa umakini.
Bw Juma Msabaha meneja huduma kwa wateja wa Amana bank akijibu baadhi ya maswali kuhusu benki hiyo toka kwa waandishi wa habari.
Meneja wa tawi la Mwanza Saleh Awadh akiongea na mteja wa benki hiyo.
Hawa Maftah wa Amana Bank akimhudumia mteja mapema leo katika tawi.
Mkurugenzi Dk Muhsin Masoud akiongea na mmoja wa mamia ya wateja aliokutana nao leo katika tawi la jijini Mwanza ambako alikuja rasmi kwa shughuli ya ufungaji wa wiki ya huduma kwa wateja.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa benki hiyo na mkurugenzi wao.
Zainab Barker ambaye ni meneja huduma kwa wateja wa tawi la Mwanza.
Ibtisam Akrabi akimhudumia mteja katika tawi la Mwanza.
Mahmoud Maimu akimhudumia mteja.

Benki ya Amana yazindua wiki ya huduma kwa wateja baada ya kutimiza miaka minne!


Mteja wa muda mrefu wa bemki ya Amana Bw Masoud Khalfan ambaye akizindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Main la benki ya Amana jijini Dar ka kukata utepe. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud, Kulia ni mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mohamed Mussa, kushoto ni mteja wa siku nyingi wa benki hiyo Bw Dossa.
Mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mussa kushoto akiwa na mkuu wa kitengo cha fedha Bw Fahad Hamid siku ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Amana Bank imeadhimisha miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24 Novemba 2011. Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi siku ya jumatatu wote walikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi yetu yote ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.
Meneja wa tawi la Main  Bi Aisha Awadh akimwelekeza kitu mteja wa benki mama Sangawe.
Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7 Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na za kisasa. Amana Bank mpaka sasa ina matawi saba ambapo manne yapo jijini Dar nayo ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na main ambapo ndipo makao makuu ya benki hiyo ya aina yake nchini.

Mfanyakazi wa benki ya Amana (Kushoto) akiwahudumia wateja kwa viburudisho katika siku ya wiki ya huduma kwa wateja wiki hii.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidiTunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu  huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.
Mtoa huduma kwa wateja Bi Zainab wa tawi la Mwanza akimhudumia kwa viburudisho mteja wa benki hiyo.

Mteja huyu akijipatia huduma katika tawi la Mwanza
Huduma kwa wateja.
Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya 27/11/2015, kwa hafla ya  kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank ambapo mkurugenzi wa benki hiyo  Dk Muhsin Masoud atakuwa katika tawi la jijini Mwanza mjini kukutana na wateja na kupokea maoni na ushauri wa kila aina utakaotolewa na wateja wao.
Baadhi ya wateja wakijipatia huduma katika benki ya Amana tawi la jijni Arusha.

Huduma kwa wateja zikiendelea jijini Arusha.