mkalamatukio: Elimu
Showing posts with label Elimu. Show all posts

VYUO VYATAKIWA KUTOA ELIMU KULINGANA NA MAHITAJI YA AJIRA HAPA NCHINI



Na Woinde Shizza,Arusha
VIJANA wengi  wanaohitimu vyuo hawapati kazi mara tu ya kuhitimu

masomo yao kutokana na kutokuwepo kwa vyanzo vya ajira vinavyokwenda
sambamba na ongezeko la wahitimu na kuchangia kuwepo kwa wimbi la
wahitimu wasiokuwa na ajira nchini.



Hayo yalisemwa    na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na
utalii ,Selestini Gesimba alipokuwa akizungumza katika mahafali ya
tano ya Chuo cha Taifa cha Utalii(NCT) ,kampasi ya Arusha ambapo jumla
la wanafunzi 55  walihitimu fani za mapishi, uokaji,mapokezi,na huduma
ya vyakula na vinywaji katika ngazi ya cheti.



Alivitaka vyuo mbalimbali kutoa elimu kulingana na mahitaji ya ajira
ili kuwezesha wanafunzi wanaohitimu kupata ajira  kwa haraka na
hatimaye kuondokana na changamoto ya wimbi kubwa la wanafunzi
wanaohitimu na kukaa mtaani bila ajira.



Gesimba alitoa rai kwa vijana wa kitanzania kujiunga na Chuo cha Taifa
cha Utalii ili wapate ujuzi ambao utatoa fursa ya kufanya kazi kwenye
sekta ya utalii na pia fursa ya kuweza kujiajiri wenyewe.



‘sekta ya utalii nchini ni ya muhimu sana na inapaswa kudhaminiwa
kwani imekuwa ikichangia asilimia 17.5 kwenye pato la Taifa na
kuifanya kuwa ya kwanza kwa kuingizia Taifa Dola bilioni mbili
ikifuatiwa na sekta ya madini ambayo imeliingizia Taifa Dola bilioni
1.7 mwaka 2004 .’alisema Gesimba.



Alisema kuwa, sekta hiyo ni miongoni mwa sekta inayokuwa kwa kasi
kubwa duniani ambapo imekuwa ikikua kwa  asilimia 4.5 hadi 5 kwa mwaka
ambapo imekuwa chachu ya kukuza na kuendeleza sekta nyingine za
kiuchumi kama kilimo, miundombinu , mawasiliano na usafiri pamoja na
kuwa kichochea kikubwa cha kupunguza umaskini katika jamii.



Naye Mtendaji Mkuu wa wakala wa chuo cha Taifa cha Utalii ,Rosada
Msoma alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutoa mafunzo na
kuwaunganisha wanafunzi wake na fursa mbalimbali za ajira ambapo kwa
mwaka huu kati ya wanafunzi hao 55 tayari wanafunzi 21 wameshapata
ajira huku wengine wakiendelea kuitwa kwenye usahili maeneo
mbalimbali.



Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake,Neema Mollel alisema
kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu
wa jenereta pindi umeme unapokatika chuoni hapo, ukosefu wa hostel
changamoto inayosababisha wanafunzi wanaosoma mbali kutoweza
kuhudhuria kozi mbalimbali chuoni hapo.



Aidha waliomba chuo hicho kuwezeshwa zaidi na kuweza kutoa kozi
mbalimbali kwa ngazi ya diploma ili kuwawezesha wanafunzi wake kupata
elimu ya juu zaidi ambapo itawawezesha kukabiliana na changamoto ya
ajira ndani na nje ya nchi.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ,Adoh  Mapunda alisema kuwa,serikali
mkoani Arusha wapo tayari kushirikiana na chuo hicho katika kuboresha
huduma mbalimbali za masomo ili kuwezesha chuo hicho kukua zaidi na
kuendelea kutoa elimu iliyo bora zaidi.



Mapunda alikitaka chuo hicho kuboresha zaidi maswala ya hoteli ili
kuwavutia wateja wengi zaidi kuweza kujiunga chuoni hapo kutokana na
elimu nzuri ,na kuwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa
kukitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi kwa ujumla.

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA BAJAVERO DAR WAPATA MAFUNZO JUU YA HEDHI SALAMA.

Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama. 
Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
 Daktari Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho

Wanafunzi wakiwa wanafundishwa moja ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya na Daktari Edna Kiogwe.

Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Tano sita na saba wakiwa wanafurahia Jambo wakati wa mafunzo
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato  wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani.

Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com  umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero,

Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia.

Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi  huahirisha shughuli za kimasomo  kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao

Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi. 


Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa  Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na huwa wanadhani mwanamke peke yake ndio anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna

Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya  Bajavero  walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora  na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory  ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.

KAWAIDA Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama. Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake? Daktari Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho Wanafunzi wakiwa wanafundishwa moja ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya na Daktari Edna Kiogwe. Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Tano ,sita na saba wakiwa wanafurahia Jambo wakati wa mafunzo Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani. **** Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero, Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia. Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi huahirisha shughuli za kimasomo kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye peke yake anaeingia hedhi. Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na hua wanadhani mwanamke peke yake ndo anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia "Alisema Dkt. Edna Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya Bajavero walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.


Habari na picha kwa niaba ya blogs za mikoa

Hanifa Fundikira ahitimu uzamili!

Mwanadada Hanifa Mdemu Fundikira leo hii katika chuo kikuu cha Northampton amehitimu shahada ya uzamili katika utalii  (Masters in Tourism management) Blog hii na blog mama Keronyingi blog zinachukua fursa hii kumpongeza bibi Fundikira kwa mafanikio haya makubwa ki elimu. Tunamtakia afya njema na mafanikio katika yote ayafanyayo.

Bibi Hanifa Mdemu Fundikira akipozi nje ya Chuo kikuu cha Northampton nchini England baada ya kuhitimu.