11/18/13

Mama Hawa Haji Kamanga kuzikwa kesho!

Marehemu Bibi Hawa Kamanga 1941-2013
Mama Hawa Kamanga ambaye alifariki leo hii asubuhi mnamo saa 2:40 katika hospitali maalum ya wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam ameacha watoto 6, wa kiume watano na wa kike mmoja. Kati ya hao watatu wanaishi marekani nao ni Haji, Kaela na Hizza. Wengine wawili wa kiume wanaishi Tanzania ambao ni  Zakaria (kaka mkubwa) na Pioka. Na mmoja wa kike  Anna Kange anaishi Holland, Marehemu ameacha wajukuu 11 na kitukuu mmoja. Baada ya wanafamilia kukaa kikao, imeamuliwa kuwa marehemu atazikwa kesho saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu na shughuli zote za msiba zipo Sinza Vatican. 

Blog hii imnesikitishwa sana na kifo hiki, mwandishi wa habari hii alipata kumtembelea marehemu alipokuwa amelazwa kwa Dk Mvungi wiki tatu zilizopita. Blog inawapa pole watoto,wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu!

MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI! AMIN


Chanzo cha habari na picha Hizza Kamanga,Grace Mmari, Houston Texas/ Tausi Khalid Dar, Tanzania.

Bibi afariki saa 48 baada ya kujua wajukuu zake wamefika hospitali kumuona!

Katika hali ya kusikitisha Mama Hawa Haji Kamanga (71) alifariki leo hii saa 2.40 Hospitalini Ocean Road  baada ya kupigania uhai wake kwa siku kadhaa alizokuwa na hali mbaya sana lakini ilielekea alipigana kubaki hai mpaka pale wajukuu zake wawili walipofika toka America siku ya Jumamosi na kwenda moja kwa moja Ocean Rd Hospital kumuona Bibi yao. Wajukuu zake hao Kaela Jr (3)na Hadassah Bianca (1) walipofikishwa wodini Marehemu akaambiwa wajuu zako wamekuja kukuona inasemekana marehemu aliyekuwa na hali mbaya kwa wakati huo alitabasamu na kujaribu kusema kitu lakini hakuweza kutoa sauti, lakini bila shaka alifurahi kujua hatimaye wajukuu zake wamemkuta akiwa hai, na hatimaye akaamua muda ulikuwa sahihi kuacha kupigania uhai wake. Mama Hawa Kamanga ana watoto kadhaa wanaoishi nchini Marekani. Marehemu alilazwa Ocean Road wiki mbili hivi baada ya kuhamishiwa hapo kutokea katika hospitali ya Dk Mvungi ambako alilazwa kwa uchunguzi wa awali. Kwa sasa mipango ya mazishi inafanyika na tutaendelea kufahamishana humu na kwingineko.
    Inna Lillah wa inna illahi Rajiun!