2013

Chozi!

Mjane wa Nelson Mandela Mama Graca Machel akifuta machozi.



Binti ya Nelsona Mandela, Mandla akiongea machache kabla ya Mazishi ya Madiba
Umati wa viongozi wa nchi mbali mbali duniani na watu mashuhuri wakihudhria mazishi ya Mandela kijijini kwake Qunu leo hii.
Wiinie Mandela, Rais Jackob Zumah Mjane wa Nelson Mandela, Mama Graca Machel.
 Picha na habari kwa hisani ya mirroronline


Kama Mandela hatoenda peponi nani ataenda?

Winnie Mandela na Askofu Desmond Tutu
Mke wa zamani wa Mandela Winnie Mandela kushoto na mjana wa Mandela Mama Graca Machel wakifuta machozi.
Msafara wa mwili wa Mandela ukiwasili Qunu jana.

Kapumzike kwa amani Baba Madiba ndivyo lisemavyo bango hili la baadhi ya waombolezaji
Msafara ukiwasili Qunu jana
Habari na picha kwa hisani ya mirroronline

Hali ya hewa ilivyotesa Huko kaskazini mashariki mwa Marekani wikiendi iliyopita!

Gari dogo likiwa imeacha barabara baada ya theluji nyingi kudondoka na kupelekea dereva wa gari hilo kupoteza mwelekeo na kutumbukia pembezoni mwa barabara(Free way)
Wikiendi iliyopita ilikuwa ni ya heka heka kubwa katika miji iliyo Kaskakazini mashariki mwa nchi ya Marekani ambapo barabara nyingi zilipitka ama kwa taabu au kutopitika kabisa katika majimbo ya Pennsylyvania na New Jersey ambapo pia imeelezwa kulikuwa na uchelewesho katika usafiri wa anga ambapo baadhi ya wasafiri walishindwa kuelekea waendako kwa takribani masaa matano hivi. Hata hivyo hali ilielekea kurudi katika ukawaida wake kuanzia j3 kwa maeneo ya Philadelphia na kwingineko.
Hali ya hewa ikiwa tata katika barabara hii ambapo kama ionekanavyo gari kadhaa zimepatwa na ajali hivyo kushindwa kuendelea na safari na pia kuziba kabisa upitikaji wa barabara hiyo wikiendi iliyopita.
Watoto nao walipata muda wa kuchezea snow
Misururur mikubwa ya magari ilionekana maeneo mengi huko America wikiendi iliyopita
Hata mitaani pia hapakusamehwa na hali mbaya ya hewa
Ramani hii ilionesha maeneo yaliyoathirika zaidi.
Picha na habari kwa hisani ya kijana mpole Francis Wali Ngula aka Baba Wamali kutoka Mount Laurel, New Jersey

Shujaa wangu Nelson Mandela!

Nelson Rolihlala Mandela, the man must have come from another planet, after his release from Roben Island prison, he suprised the whole world for urging fellow black South Africans to forgive and forget for all the oppression they suffered from the hands of white South Africans who thought they were first class citizens and superior to all other races in the country. At the end justice prevailed!

I will always remember Nelson Rolihlala Mandela as my hero,selfless leader and a true legend! Rest in peace Madiba your legacy will live on!

Roy Keane amshambulia vikali Ferguson!

Nyakati za furaha:Sir Alex na nahodha wa zamani wa Man united Roy Keane wakibeba juu moja ya makombe ya EPL waliyoyashinda pamoja
Katika hali isiyoshangaza wengi Roy Keane amemshambulia kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson kuwa anapenda nguvu na utawala hata sasa ingawa si meneja tena wa Man united. Keane anayefahamika vema kwa utata wake ndani na nje ya uwanja amefikia kusema kuwa Brian Clough ndiye kocha bora aliyewahi kufundishwa naye na si Sir Alex kocha mwenye rekodi bora kuliko yeyote katika historia ya ligi ya Uingereza na ambaye yeye Keane aliwezeshwa kushinda mataji 7 ya premier league, makombe manne ya FA, kombe moja la ulaya na kombe 1 la klabu bingwa ya dunia na ngao za hisani zisizohesabika. Lakini Keane ambaye Alex Ferguson amemuelezea kuwa ni mwenye ulimi mchafu kuliko kingine chochote na kuwa anaweza kumfanya mtu mwenye kujiamini sana kunyong'onyea na kuwa kama mtoto mdogo asiyeweza kujitetea kwa kutumia ulimi wake mchafu(maneno) bado anaumizwa na kitendo cha Ferguson kumtimua Old Trafford baada ya yeye Keane kuwasema vibaya wachezaji wadogo wakiwemo Rio Ferdinand, Darren Fletcher kuwa hawapaswi kuichezea Man United alisema maneno hayo baada ya Man united kufungwa bao 4-1 Mwaka 2005 dhidi ya Middlesborough. Ndipo Ferguson akaamua kumfukuza Roy Keane pamoja na kuwa Fergie alihakikisha Roy Keane analipwa mshahara wake wote uliobaki na pia Roy Keane akapewa mechi ya Testimonial amabzo hupewa mchezaji aliyecheza timu moja kwa muda usiopungua miaka 10. Roy Keane aliichezea Man united kwa miaka 12 na nusu.
Alex Ferguson, ameelezwa na Roy Keane kuwa ni mwenye kupenda nguvu na kutawala.
Habari na picha kwa hisani mirroronline

Arsene Wenger/Alex Ferguson na David Moyes waenda Xmas shopping pamoja!

Huyu bwana kushoto mwa picha anajiuliza ninaowaona ndio wenyewe ama?

Je inaweza ikawa kweli, kuwa Arsene Wenger, David Moyes na Sir Alex Ferguson wakaenda shopping pamoja? 
Jana waenda shopping ya Christmas nchini Uingereza waliweza kujikuta wakipigana vikumbo na sura maarufu kama Kocha wa zamani wa Man united Sir Alex Ferguson, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na Kocha mpya wa Man united David Moyes lakini kumbe hao wote hawakuwa wao halisi bali ni watu wanaofanana nao tu, ingawa watu kadhaa walistushwa na uwepo wa watatu hao wakifikiri ni wenyewe, pia mamia ya waenda shopping walipiga picha watu hao. Wazo hilo lilitolewa na National Football Museum ambao walitaka kunogesha sherehe za Christmas nchini Uingereza(Uk) 


Come on ref what is that?
Picha na habari kwa hisani ya mirroronline

Mpiga mbizi shujaa amkaribia Papa!


Wapiga mbizi Vincent Canabal na Daniel Botelho walihatarisha maisha yao ili kumkaribia papa hatari katika pwani ya visiwa vya Bahama huko Marekani katika fukwe za Tiger ambapo Vincent alikuwa akimlisha chakula cha mbwa, papa  huyo mwenye urefu wa futi 16 alivutiwa na chakula hicho ndipo akawa mtulivu.

Vincent akimlisha papa chakula cha mbwa.

Tom Daley asema yeye ni shoga!

Tom Daley(20)akionesha medali yake

Tom Daley Akiwa mchezoni
Mruka majini bingwa wa medali 2 za Olimpiki Muingereza Tom Daley(20) juzi alichukua uamuzi wa kujitangaza hadharani kupitia mtandao wa YUOTUBE kuwa yeye ni shoga. Kijana huyo mkazi wa Portsmouth, England anasemekana 
kuangukia katika penzi la mcheza sinema Dustin Lance Black ambaye ni muasisi wa chama cha kutetea haki cha American Foundation for Equal Rights ambacho kimekuwa mstari wa mbele kutetea ushoga na haki zake.
Dustin Lance Black(40) ndiye sugar daddy wa wa Kijana mtanashati Tom Daley.
Elton John na kidosho wake David Furnish
Hata hivyo si ajabu kwa nchi ya England kuwa na watu mashuhuri mashoga nao ni pamoja na Elton John, George Michael ambaye ameoana na David Furnish na hata viongozi wa seriikali hasa Dave Cameron alipata kusikika akitaka kuzishinikiza nchi zinazosaidiwa na England ziwape haki mashoga nchini ikiwemo Tanzania, baadae Cameron alikanusha habari hizo. 
Habari na picha kwa hisani ya mirroronline

Mfanyakazi wa SWISSPORT Dar es Salaam afariki ghafla!

Salustian Boniface Clement alizaliwa 07/4/1962 na kufariki 29/11/2013.
Familia ya Salustian inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Bw Salustian Clement kilichotokea ghafla siku ya Ijumaa jijini Dar es Salaam. Taarifa za msiba huu ziwafikie Familia ya Oswald Ndibalema waliopo England na popote pengine walipo, familia ya Lwakatere popote walipo pamoja na ndugu na jamaa wote wa marehemu. Marehemu Salustian ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya SWISSPORT ameacha mke na watoto watatu. Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda mjini Bukoba yatakayofanyika kesho mchana mjini hapo.
Habari na picha kwa hisani ya Edgar Oswald
Mwili wa Marehemu ulipokuwa ukisafishwa kwenda Airport.

Hapa ni kanisa Katoliki la Chang'ombe jijini Dar ambapo mwili wa marehemu uliagwa.Mungu ailaze roho yake pema peponi Ameen!

Shabiki wa Ajax ajeruhiwa vibaya baada ya kuanguka toka jukwaani

Watoa huduma ya kwanza wakimhudumia shabiki aliyeanguka akishangilia goli la pili.

Mshabiki wa timu ya Ajax Amsterdam ambaye hakutajwa jina, jana alianguka alipokuwa akishangilia bao la  pili la timu yake dhidi ya Fc Barcelona lililofungwa na Danny Hoesen. Inakadiriwa mtu huyo alianguka toka urefu wa futi 16 alikutwa kalala katika dimbwi la damu
Baadae watu wa huduma ya kwanza toka kwa magari mawili ya Ambulance na helikopta moja walimtibu mtu huyo na kumpeleka hospitali. Ajax ilifanikiwa kuifunga Barcelona katika mchezo huo wa Ubingwa wa Ulaya. Lakini haikufahamika hali ya mshabiki aliyeanguka ilikuwa ikiendeleaje.
Amsterdam Arena ionekanavyo kwa nje.


Tabora Funga mwaka Bash kuburudishwa wa na Belle9!

Msanii mkali wa Bongo Flava Belle9 atakuwa ni mmoja wa wasanii watatu watakaoburudisha Tamasha la Club Royal Funga Mwaka Bash litakalofanyika mjini Tabora katika ukumbi maarufu wa New Royal Garden. Akiongelea tamasha hilo mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo Mashaka Chura aka Mzee wa maini na Figo mkurugenzi wa Chura Fashion alisema maandalizi yamekamilika, wapenzi wa muziki wa Bongo Flava wanaotarajia kwenda kujiachia Ijumaa hii wajitokeze kwa wingi dukani kwake ambapo kuna pamba mpya na kali za kila aina ili watakapoingia katika tamasha hili la kuuaga mwaka 2013 wawe wametisha. Tamasha hilo pia litashuhudia wasanii Squizer na Ziggy Dee aliyetamba na wimbo wa Eno Mic pia wakitumbuiza ukumbini Royal Garden. Tamasha hili limewajia kwa udhamini wa Serengeti Breweries Ltd, Clouds Media Group, Chura Fashion, Gonala Pharmacy, Millenium Barber shop, Tabora Rest House, Nbs Classic, Mtingoni Company Ltd, Mussoma Batteries, CgFm 89.5, VoT fm 89.0 na Clouds Media Group.

Mama Hawa Haji Kamanga kuzikwa kesho!

Marehemu Bibi Hawa Kamanga 1941-2013
Mama Hawa Kamanga ambaye alifariki leo hii asubuhi mnamo saa 2:40 katika hospitali maalum ya wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam ameacha watoto 6, wa kiume watano na wa kike mmoja. Kati ya hao watatu wanaishi marekani nao ni Haji, Kaela na Hizza. Wengine wawili wa kiume wanaishi Tanzania ambao ni  Zakaria (kaka mkubwa) na Pioka. Na mmoja wa kike  Anna Kange anaishi Holland, Marehemu ameacha wajukuu 11 na kitukuu mmoja. Baada ya wanafamilia kukaa kikao, imeamuliwa kuwa marehemu atazikwa kesho saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu na shughuli zote za msiba zipo Sinza Vatican. 

Blog hii imnesikitishwa sana na kifo hiki, mwandishi wa habari hii alipata kumtembelea marehemu alipokuwa amelazwa kwa Dk Mvungi wiki tatu zilizopita. Blog inawapa pole watoto,wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu!

MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI! AMIN


Chanzo cha habari na picha Hizza Kamanga,Grace Mmari, Houston Texas/ Tausi Khalid Dar, Tanzania.

Bibi afariki saa 48 baada ya kujua wajukuu zake wamefika hospitali kumuona!

Katika hali ya kusikitisha Mama Hawa Haji Kamanga (71) alifariki leo hii saa 2.40 Hospitalini Ocean Road  baada ya kupigania uhai wake kwa siku kadhaa alizokuwa na hali mbaya sana lakini ilielekea alipigana kubaki hai mpaka pale wajukuu zake wawili walipofika toka America siku ya Jumamosi na kwenda moja kwa moja Ocean Rd Hospital kumuona Bibi yao. Wajukuu zake hao Kaela Jr (3)na Hadassah Bianca (1) walipofikishwa wodini Marehemu akaambiwa wajuu zako wamekuja kukuona inasemekana marehemu aliyekuwa na hali mbaya kwa wakati huo alitabasamu na kujaribu kusema kitu lakini hakuweza kutoa sauti, lakini bila shaka alifurahi kujua hatimaye wajukuu zake wamemkuta akiwa hai, na hatimaye akaamua muda ulikuwa sahihi kuacha kupigania uhai wake. Mama Hawa Kamanga ana watoto kadhaa wanaoishi nchini Marekani. Marehemu alilazwa Ocean Road wiki mbili hivi baada ya kuhamishiwa hapo kutokea katika hospitali ya Dk Mvungi ambako alilazwa kwa uchunguzi wa awali. Kwa sasa mipango ya mazishi inafanyika na tutaendelea kufahamishana humu na kwingineko.
    Inna Lillah wa inna illahi Rajiun!

Shabiki wa Arsenal apoteza nyumba baada ya Man United kuishinda Gunners!

Hali mbaya
Robin Van Persie akiwazamisha The Gunners
Shabiki mkereketwa wa timu ya Arsenal (the Gunners) Mganda Henry Dhabasani mkazi wa jijini Kampala alijikuta akipoteza nyumba yake  dhidi Rashid Yiga ambaye aliweka dau la gari ya Toyota Premio na mkewe baada ya kudai Man united ingeifunga Arsenal bila shaka na wazee wa kijadi walikuwepo na kushuhudia dau hilo likipitishwa kwa maandishi kabla ya mchezo huo amabao mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Robin Van Persie alifunga bao pekee la mchezo katika kipindi cha kwanza na kuwasimamisha The Gunners katika mbio zao za kutaka kujikita zaidi katika usukani wa ligi hiyo maarufu na yenye msisimko kuliko zote duniani. Gazeti la Observer la Uganda lilieleza kuwa shabiki huyo Dhabasani mwenye wake watatu na watoto watano alizirahi baaada ya mchezo kwisha. Hata hivyo aliondoshwa katika nyumba yake siku iliyofuata.

[Video] KISOMO CHA MWISHO CHA MAMAA NYAWANA FUNDIKIRA MDA MFUPI KABLA YA MAZISHI

UHARAKA WA MUDA WA KUHAKIKISHA MWILI WA MAREHEMU UNAZIKWA ULIZINGATIWA TU MARA BAADA YA MWILI WA MAREHEMU KUWASILI TABORA MNAMO SAA 12 JIONI. KISOMO CHA MWISHO NA MAOMBI YA MWISHO ILIFANYWA KISHA KUELEKEA KATIKA MAZIKO YA MWILI WA NYAWANA FUNDIKIRA KATIKA MAKABURI YA ITETEMYA AMBAKO IKO IKULU YA MACHIFU WA UKOO WA FUNDIKIRA. 
ILIPOFIKA MUDA WA SAA 1:10 USIKU SHUGHULI YA MAZIKO ILIENDELEA NA KUHAKIKISHA MWILI WA MAREHEMU UMEPUMZISHWA.

*UMATI MKUBWA WA WATU ULITANDA PEMBEZONI MWA BARABARA WAKISHUHUDIA MSAFARA WA KUELEKEA KATIKA MAZISHI, ILIKUWA NI MAAJABU HAIJAWAHI TOKEA HAPO MKOANI*
UMATI WA WATU NJIANI KUELEKEA MAZISHI YA NYAWANA 
[TUNAOMBA RADHI KWA VIDEO HII KWANI HAIJACHUKULIWA KATIKA MAZINGIRA BORA, VIKWAZO VILIKUWA VINGI IKIWEMO MWENDOKASI WA GARI NA GIZA]

PICHA ZA MAZISHI YA NYAWANA FUNDIKIRA

MAMAA NYAWANA AMEPUMZISHWA KATIKA MAKAZI YAKE YA MILELE KATIKA MAKABURI YA ITETEMYA HAPA MKOANI TABORA, NJE KIDOGO NA MJI
MAZISHI YAMECHELEWESHWA KUTOKANA NA KUCHELEWA KUWASILI KWA MWILI HUO WA MAREHEMU

Umati unaosubiri mwili wa Nyawana umevunja rekodi!


Kadri muda uendavyo ndivyo watu wamezidi kufika ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo ya Gongoni, Tabora mjini. Hata hivyo mwili wake umechelewa kidogo kuwasili mjini hapa lakini watu wameendelea kujazana wakikaa juani bila taabu yeyote. Hii ni ishara kuwa watu wa Tabora walimkubali sana Nyawana ambaye wao walipenda kumwita Mamaa Nyawana au Jembe! kwani watu wapatao elfu moja wamejitokeza kushuhudia au kutoa heshima za mwisho kwa Nyawana.

Sheikh akitoa mawaidha mawili matatu kwa wahudhuriaji








Waombolezaji wakisubiri mwili wa Marehemyu Nyawana uwasili kutoka Dar es Salaam.






Chakula kikiandaliwa



Waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni kubwa kwa kuondokewa na kipenzi cha Tabora Mamaa Nyawana
Huzuni huzuni huzuni!