04/20/15

WATANZANIA WAFANYA VIZURI MBIO ZA NGORONGORO MARATHONI 2015


Waziri mkuu Mstaafu , Fredrick Sumaye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo waandaji buda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio za Km 21 Katika gate la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro,
Waziri mkuu Msaatfu Fredirick Sumaye akikimbia sambamba na rais wa shirikisho la riadha Tanzania,RT,Athony Mtaka(Kushoto kwake) mkuu wa mkoa wa Arusha ,Daud Ntibenda,pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatau Omary Kwaang kuashiria kuanza kwa mbio za Ngorongoro Marathoni.
Maratibu wa Mbio , Meta Paul akiwa na mmoja wa wasiamamizi ,Leila wakati wakiwaandaa wanariadha kuanza mbio za Km 21 katika lango la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.
Mbio zikianza rasmi.
Baaadhi ya washiriki katika mbio hizo ,walikuwemo pia wadhamini kama Maremga Investment,hapa Marenga mwenye truck suit nyeusi akijaribu kukimbiza upepo.
Awawli mbio zikiwa bado ndio zimeanza kundi la wakimbiaji lilionekana wote wanakimbia kwa karibu.
Muda ulivyosonga na hatua ndivyo zilivyo ongezeka.
Hatimaye wakaanza kuachana mmoja baada ya mmoja,
Wengine wakaamua kwenda pamoja ili kupeana moja.
wengine wakafunguka zaidi.
Hatimaye wakapatikana wakimbiaji watatu wakaongoza hadi mwisho wa mbio na hawa ni ,Joseph Theofily(katikati),George Gerald (kulia) na Emanuel Giniki.
Mkimbiaji raia wa Kenya ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu kuonesha umahiri wake katika mbio hizo.
Msichana pekee aliyekuwa akiongoza ni Failuna Abdi .
Nyuma ya Failuna alikuwepo Nathalia Elisante.
Mshindi wa kwanza katika Mbio za Ngorongoro Maratahoni 2015 ,Joseph Theofily akimaliza mbio hizo katika uwanja wa Mazingira Bora akitumia muda wa 1:03:09.
Mshindi wa Pili katika mbio hizo ,George Gerald akihitimisha mbio hizo akitumia muda wa 1:03:36
Mshindi wa tatu ,Emanuel Giniki akikalimilisha mbio kwa muda wa 1:03:42.
Giniki akijaribu kupoza koo mara baada ya kumaliza mbio.
Mkimbiaji wa klabu ya riadha ya Holili,Osward Moris akihitimisha mbio.
Mshindi wa kwanza kwa kina dada Failuna Abdi akihitimisha mbio katika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 1 :10:25
Mgeni rasmi katika mbio hizo ,Waziri mkuu Mstaafu ,Fredirck Sumaye akiingia uwanjani huku akihitimisha mbio za km 21 .

WANARIADHA wa Tanzania Joseph Theofily wa klabu ya riadha ya Holili ya mkoani Kilimanjaro na Failuna Abdi wa klabu ya riadha ya Winning Spirit ya jijini Arusha wamefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya taifa baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika mbio za kimataifa za
Ngorongoro Marathoni kwa upande wa wanaume na wanawake.

Mwanariadha Theofily alifanikiwa kumaliza mbio za km 21 akitumia muda wa saa 1:03:09 na kujinyakulia kitita cha sh Mil, 1. mbele ya wakongwe wengine kutoka nchi za Kenya ,Uganda na Malawi huku Gabriely Gerald wa klabu ya Winning Spirit ya jijini Arusha akishika nafasi ya pili akimaliza mbio akitumia saa 1:03:36 na kujinyakulia kitita cha sh laki 5.

Emanuel Giniki alifanikiwa kushika nafasi ya tatu na kujinyakulia zawadi ya sh 250,000,nafasi ya nne ikichukuliwa na Ezekiel Therop huku mwanariadha Mohamed Msenduki wa klabu ya Wining Spirit ya jijini Arusha akimaliza nafasi ya tano.

Mwanariadha wa kike Failuna aliyerejea hivi karibuni kutoka nchini Brazil kushiriki mashindano ya mbio za Km 15 ambazo alifanikiwa kumaliza mbio hizo katika nafasi ya saba,aliwaongoza wakongwe kama Banuelia Bryton ,Marry Naali Jackline sakilu na Catherine Range akimaliza mbio katika nafasi ya kwanza kwa kutumia muda wa saa
1:10:25.

Failuna aliyejinyakulia zawadi ya kitita cha kiasi cha sh Mil,1. alifuatiwa kwa karibu na mpinzani wake Nathalia Elisante aliyetumia muda wa 1:14:40 na kuzawadiwa kitita cha sh 500,000 huku nafasi ya tatu  ikichukuliwa na Magdalena Crispine aliyetumia muda wa 1:15:56, nafasi ya nne na tano ikienda kwa Anjelina Tsere na Merry Naali.

Mbio za kimataifa Ngorongoro Marathoni zinafanyika zikiwa na lengo la kuwawezesha watoto wa jamii ya kimasai kupata elimu ikiwemo kumalizia shule ya Endulen iliyoko Ngorongoro na kutangaza urithi wa utalii kupitia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro huku ikishirikisha pia mbio za Kilomita tano kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali pamoja na  Km 2.5 kwa wanafunzi.


Kwa picha zaidi ingia hapa,

www.dixonbusagaga.blogspot.com

MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO.

 Watoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.
 Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.
 Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.
 Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto