mkalamatukio

Historia yajirudia Miss Kanda ya Kati 2013

Maua Kimambo Karlstrom Miss Tabora namba mbili 2011.
Miss Tabora namba mbili Sabrina Juma.
 Historia imejirudia tena baada ya warembo wawili wa Redds Miss Tabora 2013 Sabrina Juma na Anastazia Donald kufanikiwa kuingia katika shindano la Taifa (Redds Miss Tanzani 2013) warembo hao wamefuata nyayo za warembo Maua Kimambo aka Maua Karlstrom na Delilah Patrick washiriki wa Miss Tabora 2011 ambao nao waliingia Miss Tanzania baada ya shindano kali la Miss kanda ya kati mwaka 2011. Katika shindano hilo la Redds Miss central zone 2013 lililofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa Kilimani club Ijumaa ya tarehe 14/06/2013 mrembo Happiness Ruta ambaye pia ni Miss Dodoma 2013 alifanikiwa kunyakua taji la Redds Miss Central zone akfuatiwa na mrembo Sabrina Juma aliyeshika nafasi ya pili, huku Miss Singida 2013 akishika nafasi ya tatu. Hata hivyo majaji wakiongozwa na Bw Hashim Lundenga mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania waliona wachukue warembo wanne kwenda Miss Tanzania badala ya watatu baada ya Miss Tabora Anastazia Donald ambaye alishika nafasi ya nne kuweka ushindani mkali na kuwalazimisha majaji kufikiri mara mbili na kuamua kuchukua warembo wanne kitu ambacho Chief Judge Hashim Lundenga alikiri haijawahi kutokea huko nyuma.

Top five.

Miss Tabora 2013 Anastazia Donald.

Delilah Patrick, Miss Tabora namba tatu mwaka 2011

Washiriki wa Miss Tabora walipotembelea mabaki ya ngome ya Mtemi Isikie mwana Kiyungi!


Huu ulikuwa mlango mkuu wa kuingilia katika ngome ya Mtemi Isike mwana Kiyungi iliyoitwa Isyunula mnamo 1890.
Katika kuwajengea uelewa mpana warembo wa Redds Miss Tabora 2013 wikiendi iliyopita walipelekwa Kwihara lilipo tembe la mvumbuzi maarufu duniani Dr David Livingstone na pia walipata fursa ya kutembelea mabaki ya iliyokuwa ngome (Ikulu) ya Mtemi maarufu wa Unyanyembe Mtemi Isike mwana Kiyungi ambaye alipigana na Wajerumani na kuwashinda kwa miaka 5 mpaka wajerumani walipotuma mamluki wa Kiarabu kuisoma ngome hiyo ndipo walipofanikiwa kuishambulia kwa mizinga ambapo Mtemi huyo shujaa wa Unyanyembe kabla ya kukamatwa na Wajerumani akakusanya familia yake wakiwemo wake zake na jeshi lake wakajifungia ndani akajiripua na baruti na kufa, kwani aliona bora kufa kuliko kukamatwa na wakoloni. Mungu amlaze mahala pema peponi shujaa huyu!
Mzee Kibisuka Kasuka Said Fundikira ndiye aliyetoa maelezo kwa warembo wa Redds Miss Tabora 2013 juu ya ngome hiyo
Mzee Kibhisuka akiwahadithia wrembo jambo fulani. 
Warembo wakimsikiliza kwa makini.

Hapa wakitazama ulipo mlima baada ya kuambiwa kitu juu ya mlima huo.

Hapa wakitoka eneo ilipo ngome ya Isyunula.

Mrembo Kurwa akiuliza swali la mwisho kwa mwenyeji wao!

Warembo wa Redds Miss Tabora 2013 waenda kuzuru tembe la Dr Livingstone

Mzee Hamisi 
Kamati ya Redds Miss Tabora 2013 jana iliwapeleka warembo wao katika kijiji cha Kwihara kilometa 12 hivi toka Tabora mjini ambako walizuru tembe la Dr David Livingstone ambaye alikuwa mvumbuzi wa mambo mbali mbali ikiwemo vyanzo vya mito barani Afrika. Washiriki hao walikieleza kituo cha tv cha Clouds kuwa wamefurahishwa na ziara hiyo kwani imewaongezea uelewa juu ya mambo ya kale husasan David Livingstone . Wikiendi ijayo warembo hao wamepangiwa kutembelea nyumba za watoto yatima na wodi ya watoto katika Hospitali ya Kitete ya mjini Tabora.


Bango hili linaonesha tarehe, siku na mwaka aliopita  Livingstone 

Mrembo Cornencia akijitwisha kibuyu

Mrembo Faidha Hamis akijaribu mkufu uliotengenezwa kwa simbi.

Hapa wakimsikiliza Mzee Hamisi

Mrembo Sabrina Juma

TABASAMU

Cornencia akihojiwa na TBC

Pili Issa (Matron) kushoto akimshikia Mic, Cornencia. aliyekuwa akihojiwa na Nidudu Iddy wa Clouds Tv

Anastazia akihojiwa na clouds Tv


Mazoezi ya Redds Miss Tabora 2013 yaendelea!

Redds Miss Tabora 2013" Ni zaidi ya urembo"

Mazoezi ya shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Tabora 2013 yameendelea tena jana ambapo jumla ya warembo kumi na mbili watashindania taji la Redds Miss Tabora 2013, shindano lililopangwa kufanyika tarehe 31. 05 2013 katika ukumbi wa Frankman Palace. Mgeni wa heshima anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Fa.tma Mwassa. Viingilio vitakuwa sh elfu 10 kwa viti vya kawaida na sh elfu 20 kwa VIP. Msanii Ommy Dimpoz ndiye atakayenogesha shindano hilo huku Mc atakuwa Bambo Dickson wa ze comedy ya EATV.
Faidha na Sabrina

Anna akipozi

Cat walk]Warembo Grace Felix Chiku Ramadhani na Anna. 





Rehema Maginga

Adam Fundikira alinibebesha mkoba wa kaseti-Hamisi Dakota

Hamisi Dakota
Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu Hamisi Dakota alisema Adam Fundikira ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Club Royal ya Tabora alikuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake akiwa anakua hapa Tabora katika miaka ya thamanini ambapo ambapo ameeleza alivyokuwa akiruka ukuta wa nyumbani kwao usiku wakati wazazi wake wakiwa wamelala ili kumuwahi Adam ambebee mkoba wa kaseti na kupata ubwete wa kuingia Disco bure. Adam alikuwa Dj katika ukumbi wa Honey Pot(Mwana Isungu) ambayo kwa sasa inaitwa Club Royal.

Awali Dakota aliwaita jukwaani Mkala Fundikira na Adam Fundikira na kusema "Nimewaita hawa hapa jukwaani kwa kuwa hawa wanatoka katika familia ya ki chifu ya Fundikira ambayo ndio ilikuwa mtawala wa mkoa huu kabla ya uhuru ingawa palikuwa na utawala wa kikoloni kama wasimamizi, hivyo nimewaita kwa heshima kwani usipowaheshimu watemi(Machifu) unaweza ukashitukia vyombo vinaungua bila ya sababu za msingi. Aliwahi kuja Totoo Ze Bingwa akaunguza vyombo hapa Tabora, ni vema tunapoenda katika miji ya watu tupige hodi" Dakota aliyesema hayo usiku wa alhamisi ya tarehe 2 April2013 ambapo bendi ya Mapacha watatu ilitumbuiza katika ukumbi wa Frankman Palace.

Dakota akisistiza jambo.

Adfun Smiler na Mratibu wa Miss Tabora 2013

Mkala Fundikira na Hamisi Dakota

Warembo wa Redds Miss Tabora 2013 wakijfua vikali

Najifua mpaka kieleweke
Warembo watakaoshiriki shindano la kumtafuta Redds Miss Tabora 2013 litakalofanyika katika ukumbi wa Frankman Palace  mnamo tarehe 31.Mei.2013 wamekuwa wakiendelea na mazoezi makali chini ya mwalimu wao Miss Pili Issa ambaye ni Miss Tabora 2010 katika ukumbi wa Club Royal mjini Tabora. Katika onesho hilo ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Fatma Mwassa kama mgeni rasmi, kiingilio kitakuwa sh elfu 10 kwa viti vya kawaida na sh elfu 20 kwa viti maalum VIP.



Nina asili ya Tabora! - Ommy Dimpoz!

Msanii anayekuja juu kwa kasi kama moshi wa kifuu Ommy Dimpoz ambaye hivi juzi alihojiwa na kituo maarufu cha redio mkoani Tabora CG fm 89.5, alisema pamoja na kuimba katika wimbo wa wasanii wa Kigoma lakini yeye pia ana asili ya Tabora kwa kuwa Mama yake mzazi aliziliwa na kukulia hapa kabla ya kuhamia Dar, na pia aliweka wazi kuwa baba yake ndio mtu wa Kigoma. Ommy Aliyekuwa akihojiwa na Ibrahim Haruna na DJ Kessy wa CGfm 89.5 ambao ni wadhamini wa Redds Misss Tabora 2013.