mkalamatukio

Nipeni mwaka mmoja tu muone mabadiliko Kinondoni!- Karama (Kalapina) Masoud

Mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bw Karama Masoud aka Kalapina akiwahutubia wakazi wa Kinondoni Moscow kituo cha polisi jijini Dar es Salam leo jioni.
Msanii maarufu wa muziki wa kufoka foka nchini Bw Karama Masoud (Kalapina) leo hii aliendelea na kampeni zake za kutafuta kura katika jimbo la Kinondoni ambapo leo alifanya mkutano Kinondoni Moscow kituo cha polisi mkutano ambao ulihudhuriwa na wagombea udiwani wa kata za Ndugumbi, Magomeni, Mzimuni na Kigogo.



Awali wasanii wa muziki wa kizazi kipya Domokaya, TID, KR Mullah wa TMK Family walitoa burudani safi kwa wakazi wa eneo hilo waliohudhuria mkutano huo wa kampeni. Hata hivyo katika hali ya kustaajabisha ilitokea sintofahamu katika mkutano huo baada ya generator mbili kushindwa kufanya kazi na kuufanya mkutano huo kusimama kwa muda, ambapo ilifuatwa generator nyingine ya tatu ambayo nayo ilichukua muda mpaka ilipoweza kufanya kazi. 

Akiongea kwa hisia kali na wapiga kura hao, Kalapina alisema "Nikiwa mzaliwa na niliyekulia Kinondoni naelewa matatizo yenu kuanzia mazingira machafu, mafuriko ya mara kwa mara na gonjwa hatari la kipindupindu  na mengineyo mkinipa kura za kuniwezesha kwenda bungeni nitahakikisha katika kipindi cha mwaka mmoja tu mtaona mabadiliko ya mazingira hapa Kinondoni na ninawaruhusu nisipotekeleza mje mnifanyie fujo nyumbani kwangu na hata polisi wakija nitawaambia wananchi wangu wana haki ya kufanya wafanyalo kwa kuwa sijatimiza ahadi zangu.

Akimuelezea mbunge aliyepo sasa Mh Idi Azan alisema "Kwa miaka 10 sasa hali ya mazingira ya Kinondoni imedorora, Idi Azan hana lolote alifanyalo yani yupo yupo tu" aliongeza kusema "Kama kuna mtu yupo hapa alipata kumsikia Idi Azan akiongea chochote aje hapa aniambie nitampa sh elfu 10, jambo ambalo lilizua kelele za watu wakisema hawajawahi kumsikia akiongea chichote bungeni"
  

Baadhi ya wakazi wa Kinondoni Moscow wakimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bw Kalapina leo jioni.
Mbgombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bi Asma (mwenye kilemba cha zambarau) akifuatilia hotuba mbali mbali mbali katika mkutano wa kampeni ya ubunge leo.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha ACT Bw Nixon Tugara akihutubia wakazi wa Kinondoni Moscow
Mgombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bi Asma akiwasalim wakazi wa Kinondoni Moscow waliojitokeza kumsikiliza mgombea ubunge wa jimbo hilo Bw Karama Masoud. 

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Q Chillah (fulana nyeupe) na TID (mwenye miwani na balaghashia) wakifuatilia mkutano baada ya kufanya maonesho kabla ya mkutano huo kuanza.
Baaadhi wa wafuasi wa Bw Kalapina ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni wakifuatilia mkutano.
Wagombea udiwani kwa tiketi ya ACT Wazalendo wa kata za Ndugumbi, Mzimuni, Kigogo na Magomeni wakitambulishwa kwa wapiga kura wa Kinondoni Moscow.
Mshabiki wa mgombea wa ACT Wazalendo ubunge wa jimbo la Kinondoni akishangilia huku akiwa kabeba bango lenye picha ya mgombea huyo.

Mgombea wa udiwani kata ya Hananasif wa ACT Wazalendo Bw Baruani aka Komandoo akiwasalim wapiga kura wake.







Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha ACT wazalendo Bw Nixon Tugara kulia na Bi Asma wakiwa jukwaani


Mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bw Karama Masoud Kalapina katikati akifuatilia mkutano huo wa kampeni.
Bi Asma akimtambulisha Kalapina kwa wapiga kura wa Kinondoni Moscow kituo cha polisi.

Kalapina akimwaga sera makini
Picha na habari na Mkala Fundikira

Mamia wafariki katika mkanyagano Saudi Arabia

Eid al-Adha

Image copyrightSaudi Civil Defence Directorate
Image captionWatu zaidi ya 717 waliokuwa wakishiriki sherehe za hija wamefariki kwenye mkanyagano uliotokea karibu na mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca, maafisa nchini Saudi Arabia wamesema.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema watu wengine 863 wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea eneo la Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca.
Maafa hayo yalitokea mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya kaida muhimu za mwisho katika ibada za hija.
Ndio mkasa mbaya zaidi kutokea wakati wa hija katika kipindi cha miaka 25.
Mahujaji husafiri hadi Mina wakati wa kuhiji kurusha mawe saba kwenye nguzo saba zijulikanazo kama Jamarat, ambazo huwakilisha shetani.
Nguzo hizo zimo katika eneo ambalo inaaminika Nabii Ibrahim alijaribiwa na shetani.
Ramani ya eneo la Mecca
Watu walikuwa wakielekea eneo la kurushia mawe, na wengine wakitokea huko pale ghafla watu walipoanza kuanguka.
Kulikuwa na raia wa Nigeria, Niger, Chad na Senegal miongoni mwa mataifa mengine.
Idara ya ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea "ongezeko la ghafla" la watu waliokuwa wakielekea kwenye kwenye nguzo za kurushiwa mawe.
Waziri wa afya wa Saudi Arabia Khaled al-Falih amesema mkanyagano huo ulitokea kwa sababu mahujaji walikosa kufuata maagizo.
"Wengi wa wahamiaji huenda bila kufuata ratiba iliyowekwa," amesema.
Mwandishi wa BBC Hausa Tchima Illa Issoufou aliyekuwa ameenda kuhiji ni mmoja wa walioathirika. Anasema shangazi yake alifariki na baadhi ya watu alioandamana nao hawajulikani waliko.
"Watu walikuwa tu wakiimba jina la Allah, huku wengine wakilia, wakiwemo watoto. Watu walianguka sakafuni na hakukuwa na wa kuwasaidia. Ni kana kwamba kila mtu alikuwa anajijali mwenyewe," amesema.
Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya sherehe za Eid al-Adha.
Idara ya ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema maafisa 4,000 wametumwa eneo hilo kusaidia pamoja na wahudumu 200 wa huduma za dharura.
Kurusha maweImage copyrightAP
Image captionMahujaji hukusanyika kurushia mnara mawe kama ishara ya kumrushia shetani mawe
Maandalizi ya ibada hizo za hija yalikuwa yamekumbwa na mkasa baada ya kreni kuanguka katika msikiti mkuu wa Mecca mwezi huu na kuua watu 109.
Hii si mara ya kwanza kwa mikasa kutokea wakati wa hija.
Mikasa mingine iliyotokea wakati wa kuhiji:
2006: Mahujaji 364 walifariki wakati wa kurushia mawe mnara unaoashiria shetani
1997: Mahujaji 343 walifariki na 1,500 kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto
1994: 270 waliuawa katika mkanyagano
1990: Mahujaji 1,426 waliuawa katika mkanyagano njia za kupitia chini za kuelekea maeneo matakatifu
1987: Watu 400 walifariki maafisa wa serikali walipokabiliana na waandamanaji waliounga mkono Iran.
Habari na picha kwa hisani ya BBCswahili

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA IDD EL HAJI KWA MAKUNDI MBALIMBALI


 Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Mwakilishi wa Mahabusu ya Watoto Upanga, Regina Kuname msaada wa vyakula na kitoweo cha mbuzi na mafuta ya kula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya ya Idd El Haji Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo (kulia), akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Chama cha kulea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza, Hassan Hamisi kwa ajili ya sherehe hiyo.
 Mbuzi wakiingizwa kwenye gari baada ya wahusika kukabidhiwa.
 Vyakula vilivyotolewa na Rais Jakaya Kikwete vikiwa eneo la tukio vikisubiri kuchukuliwa.
Mwakilishi wa Kituo cha Wazee na Wasiojiweza cha Nunge kilichopo Kigamboni, David Mpangala akiwa na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya kituo hicho.

Na Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya vyakula na kitoweo kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji ambayo inaadhimishwa duniani kote leo.

Zawadi hiyo imekabidhiwa kwa makundi hayo kwa niaba yake na Kamshna Msaidizi Kitengo cha Walemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo Dar es Salaam leo asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Fungamo alisema Rais ametoa zawadi hiyo kwa ajili ya Sikukuu ya Idd El Haji kama anavyofanya siku zote wakati wa sikukuu mbalimbali.

Fungamo alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni Mahabusu ya Watoto ya Upanga iliyopo Manispaa ya Ilala, Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Nunge, Kigamboni, Chuo cha Watu wenye Ulemavu cha Yombo Temeke na Kituo cha Kulelea Watoto Mayatima (Chakuwama) cha Sinza.

Alitaja vituo vingine kuwa ni Kituo cha Makao ya Watoto Yatima cha Mburahati, Ilala, Kituo cha Makao ya Watoto-Kurasini, Kituo cha Full Gospel, Temeke na Kituo cha Watoto Alsaad Children House Kurasini.

Alivitaja vituo vingine kuwa ni cha Vosa Mission cha Kongowe, Temeke na Kituo cha Kijiji cha Furaha kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Fungamo alitaja vituo vilivyopata zawadi hiyo ya Idd El Haji kwa upande wa Zanzibar kuwa ni Kituo cha Mabaoni kilichopo Pemba na Makazi ya Wazee Sebleni yaliyopo Unguja.

Alitaja vituo vingine vilivyopo mikoani vilivyopata zawadi hiyo kuwa ni kituo cha The Village of Home cha Dodoma, kituo cha Moyo Mmoja cha Bagamoyo mkoani Pwani, kituo cha watoto cha Tosamaganga kilichopo mkoani Iringa na Mahabusu ya Watoto Arusha na Tanga.

SWALA YA IDD EL HAJI ILIVYOFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Sheikh Abdu Kadri akiongoza swala ya Idd El Haji katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Waislam wa Tanzania leo waliungana na wenzao duniani kote kusherehekea Sikukuu ya Idd El Haji.
 Sheikh Nurdin Kishki alipohotuba baada ya swala hiyo.
 Sheikh  Othman Dishi akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika swala.
 Wanawake na watoto wakiwa kwenye swala hiyo.
 Mazuria ya kuswalia yakitandikwa kabla ya kuanza ibada.
 Hapa wakitawaza kabla ya kuinza kwa swala hiyo.
Abdurahi Suleiman (kulia), akiuza mafuta na manukato mbalimbali katika viwanja hivyo.
 Ibada ya swala ya Idd El Haji ikiendelea.
 Biashara ya Balaghashia ikiendelea katika viwanja vyao.
 Swala ikiendelea katika viwanja hivyo.
 Pikipiki na baiskeli zikiwa zimewekwa kwa pamoja kwa ajili ya usalama.
 Mwanahabari akichukua picha katika ibada hiyo.
 Waumini wa kiislam wakiwa katika viwanja hivyo wakati wa ibada hiyo.
 Hapa salamu zikiendelea.
 Sheikh Othmani Dishi (kushoto), akisalimiana na Sheikh Abdu Kadri kabla ya kuanza kwa swala hiyo.
 Swala ikifanyika katika viwanja hivyo.
 Swala ikifanyika kwa unyenyekevu mkubwa.
Swala ikiendelea.

Fwd: DkShein Aendelea na Kampeni Zake na Kusema Ataendeleza Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Kuleta Maendeleo Zaidi kwa Wazanzibar katika Wananchi Wake na Elimu Bure Zanzibar.


Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia Chama cha Mapinduzi pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Mpira Konde Kisiwani Pemba kuendelea na Kampeni Kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliofika katika uwanja wa kunde kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.wakati akiwasili katika viwanja hivyo vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wanachama wa CCM Wakimshangilia Mgombea wao wa Urais Dk Shein, wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Konde kwa ajili ya mkutano wake wa Tatu wa Kampeni zake kisiwani Pemba.
Taswira ya wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais kupitia CCM katika viwanja vya mpira Konde Pemba kama inavyooneka Mwanachama huyu wa CCM akishangilia akiwa na picha ya Mgombea Urais wa CCM Dk Shein.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad akiwahutubia na kutuoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo Zanzibar katika kipindi chake Dk Shein cha miaka mitano na kuwataka kumpa kura kwa mara ya pili kuendeleza mafanikio ya Maendeleo Zanzibar katika sekta mbalimbali za Jamii 

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.
Katibu wa Idara ya Uenezi Afisi Kuu Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu akiwahutubia Wananchi wa Konde katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein uliofanyika katika uwanja wa mpira Konde Kisiwani Pemba.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Khadija Aboud akiwahutubia Wananchi na Wana CCM kisiwani Pemba wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwahutubia Wananchi katika viwanja vya mpira Konde Kisiwani Pemba akiwa katika kampeni yake na kuwataka Zanzibar kukipigia kura Chama cha Mapinduzi kwa maendeleo na kudumisha Amani na Utulivu kwa Wananchi wake kwa maendeleo. 
Viongozi wa Jukwaa kuu wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, wakati akiwahutubia Wananchi wa Konde Pemba Wilaya ya Micheweni akiwa katika mikutano yake ya kampeni kisiwani Pemba.
Wazee wa CCM Wilaya ya Micheweni wakiwa katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar wakimsikiliza Dk Shein wakati akiwahutubia na kutowa Sera za CCM kwa wananchiwakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wanachama wa CCM wakimshangilia mshangilia Mgombea wa Urais Dk Shein, wakati akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Micheweni akiwa katika mikutano yake ya Kampeni Kisiwani Pemba.
Mwana CCM Pemba akishangilia wakati wa mkutano huo wa kampeni ya Urais wa Zanzibar katika viwanja vya Konde Pemba.
           Wananchi wakiwa katika viwanja vya mkutano Konde wakifuatilia mkutano huo.

Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya mpira Konde wakimsikiliza Mgombea Wao akiwahutubia katika mkutano wa Kampeni ya CCM Pemba.

            WanaCCM wakishangilia wakati wa mkutano huo katika viwanja vya mpira Konde Pemba.

Viongozi wa Jukwaa Kuu wakisimama wakati Dk Shein, akienda kuwahutubia Wananchi wakati wa Mkutano wake wa Tatu wa Kampeni Kisiwani Pemba uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.

Mgombea Urais wa Zanzinzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijiandaa kuwahutubia Wanachama wa CCM katika viwanja vya mpira Konde Kisiwani Pemba akiwa katika mikutano yake ya kampeni Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akiwahutubia Wananchi katika viwanja vya mpira konde kisiwani Pemba akiwa katika kampeni za kuomba kura kwa Wananchi kuendelea kuongoza Zanzibar kwa kipindi cha Pili ilin kuendelea maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar na kudumisha Amani na Utulivu kwa wananchi wake,
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Pemba wakati wa mkutano wake wa Kampeni na kuwataka kuichagua CCM kuzi kuwaletea maendeleo katika miradi mbalimbali na kuendelea kuongoza Zanzibarb kwa misingi ya Sheria na haki kwa maendeleo ya Wazanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Konde Ndg Omar Seif Abeid, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Tumbe Ndg Ali Khamis Bakar, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Micheweni Pemba, Ndg Shamata Shaame Khamis,, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Wingi Pemba Ndg.Said Omar Said, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Wingwi Pemba, Ndg Khamis Shaame Hamad, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Konde, Pemba, Ndg Ramadhani Omar Ahmed, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tumbe Pemba, Ndg Rashid Kassim Abdalla. wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Micheweni Pemba, Ndg Khamis Juma Omar, wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein, katika viwanja vya mpira Konde Pemba.
Wananchi wakishangilia wakati wa kuwatambulisha wagombea Ubunge na Uwakilishi na Udiwani wa Wilaya ya Micheweni Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Shein akiwatambulisha Wagombea Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Micheweni Pemba wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar katika viwanja vya mpira Konde Pemba. 
Wananchi wakishangilia wakati wa kuwatambulisha wagombea Ubunge na Uwakilishi na Udiwani wa Wilaya ya Micheweni Pemba.
Shekh akisoma dua baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika kastika viwanja vya mpira Konde Pemba Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akiondoka viwanja vya Konde Pemba baada ya kumaliza mkutano wake wa tatu wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde Pemba, akiongozania na Viongozi wa CCM.

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. Zanzinews.com