mkalamatukio

Ujumbe mzito wa Imetosha watembelea kituo cha Buhangija mjini Shinyanga!


Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.
Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga

Wajumbe wa Imetosha
 Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.  “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.

Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha

 Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa” alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10. 

Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.
Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284 wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.


 Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho



Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands!
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga


Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho


Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali
Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira 

EPUSHA AJALI OKOA MAISHA!


Ujumbe wa Imetosha Foundation wawasili Mwanza!


Salome Gregory akifuatiwa na Balozi Mdimu na Issaya Mwakilasa wakiteremka toka katika ndege iliyowasafirisha toka Dar mpaka Mwanza.

Picha ya kumbukumbu toka kushoto ni Issaya Wakuvwanga, Zaytuni Biboze, Salome Gregory, Henry Mdimu na Mkala Fundikira, Mwanza airport.
Ujumbe wa taasisi ya Imetosha inayojishughulisha na utoaji elimu juu ya kumaliza unyanyapaa,  ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini uliwasili jijini Mwanza leo hii saa 2 asubuhi kwa ziara ya siku 3 ambapo kati siku hizo tatu ujumbe huo utakutana na viongozi wa ki serikali na usalama wa baadhi ya mikoa na wilaya za kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Shinyanga. Lengo la mikutano hiyo ni kamati kujitambulisha kwa viongozi hao na kuwaeleza nini Imetosha inatarajia kufanya katika kanda hii mwezi ujao ambako pamekuwa na matukio mengi ya ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania. 

 Vile vile kamati itakuwa na siku moja ambapo itatembelea vyombo ya habari vya jijini hapa kabla ya kurejea Dar es Salaam.

Habari na picha na Mkala Fundikira wa Mkalamatukio/keronyingi blog

Kamati ya imetosha yatuma ujumbe mzito kanda ya ziwa!


Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari
Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya janga hili. Ujumbe huo utaongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw Masoud Kipanya, Balozi Henry Mdimu Mgaya na katibu Salome Gregory,wajumbe watakaongozana na viongozi hao ni pamoja na Mkala Fundikira, Isaya Mwakilasa (wakuvwanga aka Baba Andunje) Zaytun Biboze, Kelvina John na msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika.

Mwenyekiti Masoud Kipanya akiongea katika kilele cha matembezi ya hamasa yaliyofanyika jijini Dar
Dhumuni la safari hiyo itakayoupeleka ujumbe huo mpaka mkoani Shinyanga ni kwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali na usalama wa mikoa na za kanda hiyo iliyoathiriwa sana na janga la ukatili na mauaji ya watu wenye ualbino. Taasisi ya Imetosha imepanga kwenda kanda ya ziwa baadaye mwezi ujao ambapo timu itaenda maeneo yaliyoathiriwa na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa si kweli kwamba ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ualbino utapata mafanikio, elimu hizo zitatolewa kwa njia ya filamu mbali mbali, michezo ya kuigiza na matamasha ya muziki.
Hoteli ya Green Palm utakapofikia ujumbe wa Imetosha Foundation jijini Mwanza aka the Rock City.
Ujumbe huu ukiwa mjini Mwanza utakuwa chini ya udhamini wa hoteli ya Green Palm iliypo maeneo ya Bwiru, vile vile kampuni ya Mwananchi communication ltd (MCL) inayozalisha gazeti bora la Mwananchi na mengineyo itachapisha habari zote kuhusiana na msafara huo wa Imetosha kanda ya ziwa. Meneja wa hotel 

Isaya Mwakilasa wa (Orijino komedi) Henry Mdimu na familia ya Isaya aka Wakuvwanga
ya Green Palm Bw Juma Herman ameuambia mtandao huu kuwa "imekuwa rahisi kwetu (Green Palm Hotel) kudhamini makazi na usafiri kwa taasisi hiyo kwa kuwa inachofanya ni kitu chema basi nasi tumeona ni vema tuwatie nguvu kwa kuwapatia malazi na usafiri wa ndani kwa kipindi chote watakachokuwa jijini Mwanza, kwa kweli sasa imetosha ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino" aliongeza.
Wakiongea na mtandao huu kwa nyakati tofauti Mwenyekiti Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu walisema  wanashukuru sana kwa kitendo cha Green Palm na Mwananchi communictaion na kuwa ni vya kuigwa na makampuni mengine ili kuiwezesha taasisi hiyo kufikia malengo yake. Taasisi ya Imetosha haina vyanzo vya fedha hivyo kutegemea wahisani kama Green Palm Hotel na Mwananchi communication.
Maktaba Baadhi ya wajumbe wa Imetosha wakijiandaa kwenda katika mchezo wa Simba na Yanga

WANAFUNZI WA CARMAN AINSWORTH HIGH SCHOOL WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.

 Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe balozi Liberata Mulamula.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe, balozi Leberata Mulamula.
Mhe, balozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.
   Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.
Picha na habari kwa hisani ya Mubela Bandio wa Changamoto blog

Siku Mh Al Shaymaar Kweigir alipoweka uheshimiwa pembeni na kusema IMETOSHA!


Mh Al Shaymaar akicheza wimbo wa Imetosha na balozi Mdimu pamoja na  baadhi ya watu waliohudhuria matembezi ya uhamasishaji wimbo huo uliimbwa na msanii wa reggae Jhikoman Manyika  .
Siku ya matembezi ya uhamasishaji dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino yaliyofanika kutoka viwanja vya Biafra mpaka viwanja vya leaders mbunge wa viti maalum Mh Al Shaymaar Kweigir aliamua kuuvua uheshimiwa kwa muda na kujichanganya na wadau wengine walijitokeza kiwanjani hapo kwa kucheza kwa hisia kubwa yenye kuinesha kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Imetosha foundation za kuelimisha na hatimaye kutokomeza kabisa unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino duniani! Matembezi na tamasha viliandaliwa na Imetosha foundation kwa dhamini toka IPTL, Legendary Music, EFM Radio, TDL, Coca Cola, Ultimate security na Flexible studios
Mwenyekiti wa Imetosha foundation akimpongeza Mh Al Shaymaar baada ya matembezi.










MC mkongwa Mzee Mdachi akiwa katika pose!

Nyie chukueni selfie mie nimevutiwa na ya jukwaani!
Rose Manumba na Jamila wakiwakilisha!
Monica Joseph kulia akiongea na baadhi ya wadau wa harakati za Imetosha

Emmanuel Masaka akijiuliza Nitumie camera gani hapa????

Kelvina na Jestina  wa Jestina George blog
Wajumbe  wa Imetosha foundation!
Picha zote na Mkala Fundikira wa keronyingi blog