mkalamatukio

Shabiki wa Chelsea mpigania haki za binadamu atuhumiwa kwa ubaguzi Paris!


Bw Richard Barklie akihutubia kongamano la haki za binadamu nchini India
Imebainika kuwa askari polisi wa zamani na mpigania haki za binadamu Bw Richard Barklie ni mmoja kati ya mashabiki watatu wa Chelsea waliomzuia mtu mweusi Suleyman Syla kupanda treni kwa kuwa ni mweusi. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya mchezo wa ubingwa wa ulaya (UEFA Champions league) kati ya Paris Saint Germain(PSG) na Chelsea uliochezwa jijini Paris Ufaransa jumanne iliyopita. Bwana Barklie alibainika baada ya Metropolitan Police ya Uingereza kuonesha picha za washukiwa wa tukio hilo zilizokamatwa na kamera za cctv za stesheni hiyo ya treni za ardhini maarufu kama METRO.

Bw Barklie ambaye pia ni mkurugenzi katika taasisi ya hiari mjini Belfast Northen Ireland ya WAVE TRAUMA CENTRE ameshasimamishwa kazi na taasisi hiyo kupisha upelelezi.

Barklie ambaye ni mmiliki wa tiketi ya msimu ya Chelsea fc akiwa na wenziwe watatu walimsukuma Bw Syla asiingie ndani ya treni (METRO) huku wakiimba (we are racists we are racists this is how we ike it) Sisis ni wabaguzi na hivi ndivyo tupendavyo. Police nchini England imeshawatambua watuhumiwa lakini hakuna aliyekamatwa mpaka sasa, Idara hiyo ya polisi imeeleza upelelezi utaingia hatua inayofuata.

Hata hivyo kupitia mwanasheria wake Bw Barklie amakanusha kuhusika na vitendo vya kibaguzi vilivyotokea siku hiyo lakini anakiri kuwepo eneo la tukio, na amedhamiria kujisafisha.

Metropolitan police pia imeeleza haiwezi kukamata mtu kwa makosa aliyoyafanya nje ya Uingereza, kwa mawazo yangu basi bila shaka Polisi ya Paris itabidi iiombe serikali ya England washukiwa wapelekwe Ufaransa kwa mahojiano na pengine kushtakiwa iwapo itaonekana wana kesi ya kujibu.

Kilabu cha Chelsea kupitia meneja wa timu Jose Mourinho kimeelzwa kusikitishwa na tukio hilo na kuwa kitawafungia wote watakapatikana na kesi ya kujibu. Taarifa ya msemaji wa kilabu hicho cha jijini London ameelza kuwa mmiliki wa timu hiyo Bw Roman Abramovich ametiwa kinyaa na kitendo hicho. Pia kilabu hicho kimeshamkaribisha Bw Syla London katika mchezo wa marudiano kati ya timu hizo mbili.
Picha ya Bw Barklie iliyochukuliwa toka cctv.
Hotuba India
Barklie akiwa katika harakati za haki za binadamu barani Afrika.
Bw Suleyman Syla ndiye mhanga wa tukio la kibaguzi lililotokea stesheni ya treni za chini ya ardhi (METRO) jijini Paris Ufaransa.
Picha na habari kwa hisani ya mailonline/AFP/Metropolitan police

Msanii Moses Bushagama aka Mez B afariki dunia leo!

Mez B enzi za uhai wake!
Msanii Moses Bushagama aka Mez B aliyewahi kung’ara na ngoma ya kikuku cha mama Roda ambayo mimi Mkala Fundikira nilimfanyia video yake katika miaka ya 2000 katika studio za Royal Productions, pamoja na nyimbo zingine nyingi amefariki dunia leo mjini Dodoma ambako mama yake huishi baada ya kuugua kifua kikuu(TB). Binafsi nimeshtushwa na kifo chake hasa baada ya kupata habari za kifo chake bila kufahamu kama alikuwa akiugua kwa muda.Mez alikuwa na kipaji cha aina yake na sauti laini, tutamkumbuika daima.
                           Mungu ilaze pema roho yake!
Picha kwa hisani ya Dj Choka

Simba yashindwa kuunguruma Tanga!


Timu ya Simba leo jioni ilishindwa kuunguruma dhidi ya Coastal union ya jijini Tanga kkatika mchezo uliopooza hivyo kuendelea kusuasua katika ligi ya msimu huo. Pamoja na kuleta mashabiki wengi toka jijini Dar timu hiyo ya Msimbazi haikucheza vizuri sana.



Homa ya mchezo kati ya Coastal union na Simba sports club yapamba moto!

Wakazi wa jiji la Tanga, viunga vya vyake na mikoa ya jirani leo hii watapata burudani inayotarajiwa kuwa ya kupendeza leo hii jioni mnamo saa 10.15 za jioni wakati Wekundu wa Msimbazi Simba SC itakapoingia katika stadia ya Mkwakwani kucheza mchezo wa Vodacom Premier league 2014/15 dhidi ya Coastal union ya jijini hapa kuwania pointi 3  muhimu hasa kwa Simba ambayo imekua ikifanya vibaya msimu huu na kupelekea hofu kwa washabiki wake kuwa uenda ikateremka daraja. Mpambano huo bila shaka utaoneshwa LIVE na kituo cha Televisheni cha AZAM ambacho mitambo yake imeonekana mje ya uwanja wa Mkwakwani, kama ionekanavyo hapo chini.
OB Van ya Azam Tv ikiwa tayai kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Mkwakwani stadium.
Sare za Simba SC zikiwa zimeanikwa kwa mauzo nje ya uwanja wa Mkwakwani
Mshabiki wa Simba kushoto akijadili bei ya fulana ya timu hiyo ya jijini Dar es Salaam karibu na uwanja wa Mkwakwani.
Picha na habari keronyingi blog

Mfereji mpya wa maji wahatarisha watumia barabara ya Boma Tabora!

Kushoto unaonekana mfereji wa maji.


Baada ya mfereji huo kuchimbwa na kujengewa kwa mawe, udongo uliotokana na uchimbaji wa mfereji huo umeachwa kando kando ya Boma Road nje ya Holiday Park Guest house na kusababisha adha katika upishanaji wa magari hasa makubwa yapitayo katika barabara hiyo ambayo kabla ya kuachwa vifusi hivyo vya udongo tayari ni nyembamba. Haikuweza kufahamika mara moja ni nani muhusika na huo mfereji lakini huenda ikawa mfereji huo ukawihusu Manispaa ya mkoa wa Tabora. Blogu hii ingependa kuwakumbusha wahusika kuondosha vifusi hivyo ili kuepusha ajali zinazoweza kuotoa eneo hilo.


Barabara ya Boma inavyoonekana pichani

Promota wa Lennox Lewis aamua kuwa mwanamke!

Frank Maloney akishangilia ushindi wa Lenox Lewis
Frank Maloney(61) promota maarufu wa ndondi wa zamani ambaye amewahi kuwa promota wa bingwa wa zamani wa uzito wa Juu Lennox Lewis ameamua kujibadili kuwa mwanamke na Kujiita Kellie. Kwa kauli yake Maloney alisema "Nimekuwa nikijisikia hivi tangu utotoni mwangu, hatimaye nimechoka kuishi kivulini. Pia alieileza ugumu ulikuwa ni kumfahamisha mkewe anachotaka kufanya, pia ameeleza atafanya operesheni ya badiliko la kijinsia, na kuwa hafanyi hayo ili awe na mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote bali ndivyo alivyokuwa akijisikia awe kwa miaka yote. 

Maloney anavyoonekana sasa akiwa kama Kellie. 
Ajuza Kellie akiweka pozi

Mtazamo wangu ni kuwa kwa nini kasubiri mpaka kazeeka?

Picha na habari kwa hisani ya mailonline na sunday mirror

Over pass yaporomoka na kuua watu wawili Brazil!

Barabara  mpya ya juu (over pass) iliyokuwa ikijengwa mjini Belo Horizonte nchini Brazil iliporomoka jana (Alhamisi) na kuanguakia malori matatu, gari dogo na basi la kusafirishia abiria na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 19. Hata hivyo maafisa wa uokoaji wameeleza kuna nafasi kubwa ya miili mingine kupatikana chini ya barabara hiyo. Barabara hiyo ilijengwa ili kupunguza msongamano katika kipindi hiki cha world cup nchini Brazil ambapo mjini Belo Horizonte ambapo pana uwanja wa Mineirao ambao utatumika kwa mchezo wa nusu fainali siku ya jumanne katika mfululizo wa fainali za kombe la dunia 2014. 
Kwa juu inaonekana over pass hiyo ikiwa imelala ardhini baada ya kuporomoka
Basi lililoangukiwa na barabara ambamo dereva wake ni mmoja wa watu wawili waliokufa papo hapo hapo jana.
Gari dogo lililoangukiwa na over pass mijini Belo Horizonte, nchini Brazil.
Malori mawili yanaonekana kubanwa na over pass hiyo huku waokoaji wakishauriana 
Uwanja wa Mineirao utakaochezewa mchezo nusu fainali mjini Belo Horizonte uliopo Km 3 toka eneo la ajali.
Picha kwa hisani ya AFP/ habari na mirror online