mkalamatukio

Mfereji mpya wa maji wahatarisha watumia barabara ya Boma Tabora!

Kushoto unaonekana mfereji wa maji.


Baada ya mfereji huo kuchimbwa na kujengewa kwa mawe, udongo uliotokana na uchimbaji wa mfereji huo umeachwa kando kando ya Boma Road nje ya Holiday Park Guest house na kusababisha adha katika upishanaji wa magari hasa makubwa yapitayo katika barabara hiyo ambayo kabla ya kuachwa vifusi hivyo vya udongo tayari ni nyembamba. Haikuweza kufahamika mara moja ni nani muhusika na huo mfereji lakini huenda ikawa mfereji huo ukawihusu Manispaa ya mkoa wa Tabora. Blogu hii ingependa kuwakumbusha wahusika kuondosha vifusi hivyo ili kuepusha ajali zinazoweza kuotoa eneo hilo.


Barabara ya Boma inavyoonekana pichani

Promota wa Lennox Lewis aamua kuwa mwanamke!

Frank Maloney akishangilia ushindi wa Lenox Lewis
Frank Maloney(61) promota maarufu wa ndondi wa zamani ambaye amewahi kuwa promota wa bingwa wa zamani wa uzito wa Juu Lennox Lewis ameamua kujibadili kuwa mwanamke na Kujiita Kellie. Kwa kauli yake Maloney alisema "Nimekuwa nikijisikia hivi tangu utotoni mwangu, hatimaye nimechoka kuishi kivulini. Pia alieileza ugumu ulikuwa ni kumfahamisha mkewe anachotaka kufanya, pia ameeleza atafanya operesheni ya badiliko la kijinsia, na kuwa hafanyi hayo ili awe na mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote bali ndivyo alivyokuwa akijisikia awe kwa miaka yote. 

Maloney anavyoonekana sasa akiwa kama Kellie. 
Ajuza Kellie akiweka pozi

Mtazamo wangu ni kuwa kwa nini kasubiri mpaka kazeeka?

Picha na habari kwa hisani ya mailonline na sunday mirror

Over pass yaporomoka na kuua watu wawili Brazil!

Barabara  mpya ya juu (over pass) iliyokuwa ikijengwa mjini Belo Horizonte nchini Brazil iliporomoka jana (Alhamisi) na kuanguakia malori matatu, gari dogo na basi la kusafirishia abiria na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 19. Hata hivyo maafisa wa uokoaji wameeleza kuna nafasi kubwa ya miili mingine kupatikana chini ya barabara hiyo. Barabara hiyo ilijengwa ili kupunguza msongamano katika kipindi hiki cha world cup nchini Brazil ambapo mjini Belo Horizonte ambapo pana uwanja wa Mineirao ambao utatumika kwa mchezo wa nusu fainali siku ya jumanne katika mfululizo wa fainali za kombe la dunia 2014. 
Kwa juu inaonekana over pass hiyo ikiwa imelala ardhini baada ya kuporomoka
Basi lililoangukiwa na barabara ambamo dereva wake ni mmoja wa watu wawili waliokufa papo hapo hapo jana.
Gari dogo lililoangukiwa na over pass mijini Belo Horizonte, nchini Brazil.
Malori mawili yanaonekana kubanwa na over pass hiyo huku waokoaji wakishauriana 
Uwanja wa Mineirao utakaochezewa mchezo nusu fainali mjini Belo Horizonte uliopo Km 3 toka eneo la ajali.
Picha kwa hisani ya AFP/ habari na mirror online

HAWA NDIYO WAREMBO WA REDDS MISS KANDA YA KATI 2014 [DODOMA]

Washindi watatu bora wa mashindano ya REDDS MISS KANDA YA KATI 2014, Mshindi akiwa ni Dorice Mole (katikati) akitokea mkoa wa singida, wa pili ni Zenna Motte (kushoto) akitokea Tabora katika Chuo Kikuu cha SAUT-TABORA na wa tatu ni Adelaide (kushoto). Warembo hao wakifurahia ushindi huo usiku wa tarehe 20 Juni, 2014

Vazi la ubunifu Miss Dar Indian Ocean

Vazi hili lilitia fora katika mavazi yote ya ubunifu


Miss Shamila
Warembo wa Miss Dar Indian Ocean wakionesha vazi la ubunifu siku ya kilele cha shindano hilo
Miss Sophia


Miss Mary Shila
Miss Mary Shila

Miss Monica Nshimba


Miss Sasha Deogratius(Talent winner)

Miss Janeth Geophrey
Miss Hasnat Hussein

Opening show ya Miss Dar Miss Indian Ocean ilivyoenda!


Washiriki wa Miss Dar Indian Ocean wakicheza  mziki wa kufungulia shindano
Mshiriki Miss Mary Shila alitia fora kwa uchezaji wake mziki kwa umahiri.
Suzannah Sawaya akinengua
Miss Camilla John
Mariam Salum akicheza opening show
Tunajimwaga



Mc Jose ambaye pia ndiye alifundisha warembo kucheza opening show.

Camilla John aibuka mshindi Redds Miss Dar Indian Ocean!

Miss Camilla John ndiye Redds Miss Dar Indian Ocean
Top 3, Miss Dar Indian Ocean Camilla John akiwa na Mary Shila kulia na Getrude Massawe
Top 5, toka kushoto Marim Salum, Mary Shila, Camilla John, Getrude Massawe na Hasnat Hussein
Muandaaji wa Redds Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahma Yusuph na mgeni rasmi Mh Abass Tarimba

Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Bw Albert Makoye akimkaribisha mgeni rasmi Bw Abass Tarimba afungue hafla rasmi.
Bw Abass Tarimba(MGENI RASMI) mkurugenzi wa Bahati nasibu ya taifa
Boy George akiwa na mdhamini CXC Africa Bw Charles Hamka wakijadili jambo fulani jana.
Majaji wa Miss Dar Indian Ocean wakifuatilia mwenendo wa shiondano hilo jana
Majaji wakitazama kwa makini moja washiriki akipita jukwaani toka kushoto Innocent Melleck, James Kissaka na Hassan Ally.