mkalamatukio

Mpiga mbizi shujaa amkaribia Papa!


Wapiga mbizi Vincent Canabal na Daniel Botelho walihatarisha maisha yao ili kumkaribia papa hatari katika pwani ya visiwa vya Bahama huko Marekani katika fukwe za Tiger ambapo Vincent alikuwa akimlisha chakula cha mbwa, papa  huyo mwenye urefu wa futi 16 alivutiwa na chakula hicho ndipo akawa mtulivu.

Vincent akimlisha papa chakula cha mbwa.

Tom Daley asema yeye ni shoga!

Tom Daley(20)akionesha medali yake

Tom Daley Akiwa mchezoni
Mruka majini bingwa wa medali 2 za Olimpiki Muingereza Tom Daley(20) juzi alichukua uamuzi wa kujitangaza hadharani kupitia mtandao wa YUOTUBE kuwa yeye ni shoga. Kijana huyo mkazi wa Portsmouth, England anasemekana 
kuangukia katika penzi la mcheza sinema Dustin Lance Black ambaye ni muasisi wa chama cha kutetea haki cha American Foundation for Equal Rights ambacho kimekuwa mstari wa mbele kutetea ushoga na haki zake.
Dustin Lance Black(40) ndiye sugar daddy wa wa Kijana mtanashati Tom Daley.
Elton John na kidosho wake David Furnish
Hata hivyo si ajabu kwa nchi ya England kuwa na watu mashuhuri mashoga nao ni pamoja na Elton John, George Michael ambaye ameoana na David Furnish na hata viongozi wa seriikali hasa Dave Cameron alipata kusikika akitaka kuzishinikiza nchi zinazosaidiwa na England ziwape haki mashoga nchini ikiwemo Tanzania, baadae Cameron alikanusha habari hizo. 
Habari na picha kwa hisani ya mirroronline

Mfanyakazi wa SWISSPORT Dar es Salaam afariki ghafla!

Salustian Boniface Clement alizaliwa 07/4/1962 na kufariki 29/11/2013.
Familia ya Salustian inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Bw Salustian Clement kilichotokea ghafla siku ya Ijumaa jijini Dar es Salaam. Taarifa za msiba huu ziwafikie Familia ya Oswald Ndibalema waliopo England na popote pengine walipo, familia ya Lwakatere popote walipo pamoja na ndugu na jamaa wote wa marehemu. Marehemu Salustian ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya SWISSPORT ameacha mke na watoto watatu. Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda mjini Bukoba yatakayofanyika kesho mchana mjini hapo.
Habari na picha kwa hisani ya Edgar Oswald
Mwili wa Marehemu ulipokuwa ukisafishwa kwenda Airport.

Hapa ni kanisa Katoliki la Chang'ombe jijini Dar ambapo mwili wa marehemu uliagwa.Mungu ailaze roho yake pema peponi Ameen!

Shabiki wa Ajax ajeruhiwa vibaya baada ya kuanguka toka jukwaani

Watoa huduma ya kwanza wakimhudumia shabiki aliyeanguka akishangilia goli la pili.

Mshabiki wa timu ya Ajax Amsterdam ambaye hakutajwa jina, jana alianguka alipokuwa akishangilia bao la  pili la timu yake dhidi ya Fc Barcelona lililofungwa na Danny Hoesen. Inakadiriwa mtu huyo alianguka toka urefu wa futi 16 alikutwa kalala katika dimbwi la damu
Baadae watu wa huduma ya kwanza toka kwa magari mawili ya Ambulance na helikopta moja walimtibu mtu huyo na kumpeleka hospitali. Ajax ilifanikiwa kuifunga Barcelona katika mchezo huo wa Ubingwa wa Ulaya. Lakini haikufahamika hali ya mshabiki aliyeanguka ilikuwa ikiendeleaje.
Amsterdam Arena ionekanavyo kwa nje.


Tabora Funga mwaka Bash kuburudishwa wa na Belle9!

Msanii mkali wa Bongo Flava Belle9 atakuwa ni mmoja wa wasanii watatu watakaoburudisha Tamasha la Club Royal Funga Mwaka Bash litakalofanyika mjini Tabora katika ukumbi maarufu wa New Royal Garden. Akiongelea tamasha hilo mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo Mashaka Chura aka Mzee wa maini na Figo mkurugenzi wa Chura Fashion alisema maandalizi yamekamilika, wapenzi wa muziki wa Bongo Flava wanaotarajia kwenda kujiachia Ijumaa hii wajitokeze kwa wingi dukani kwake ambapo kuna pamba mpya na kali za kila aina ili watakapoingia katika tamasha hili la kuuaga mwaka 2013 wawe wametisha. Tamasha hilo pia litashuhudia wasanii Squizer na Ziggy Dee aliyetamba na wimbo wa Eno Mic pia wakitumbuiza ukumbini Royal Garden. Tamasha hili limewajia kwa udhamini wa Serengeti Breweries Ltd, Clouds Media Group, Chura Fashion, Gonala Pharmacy, Millenium Barber shop, Tabora Rest House, Nbs Classic, Mtingoni Company Ltd, Mussoma Batteries, CgFm 89.5, VoT fm 89.0 na Clouds Media Group.

Mama Hawa Haji Kamanga kuzikwa kesho!

Marehemu Bibi Hawa Kamanga 1941-2013
Mama Hawa Kamanga ambaye alifariki leo hii asubuhi mnamo saa 2:40 katika hospitali maalum ya wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam ameacha watoto 6, wa kiume watano na wa kike mmoja. Kati ya hao watatu wanaishi marekani nao ni Haji, Kaela na Hizza. Wengine wawili wa kiume wanaishi Tanzania ambao ni  Zakaria (kaka mkubwa) na Pioka. Na mmoja wa kike  Anna Kange anaishi Holland, Marehemu ameacha wajukuu 11 na kitukuu mmoja. Baada ya wanafamilia kukaa kikao, imeamuliwa kuwa marehemu atazikwa kesho saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu na shughuli zote za msiba zipo Sinza Vatican. 

Blog hii imnesikitishwa sana na kifo hiki, mwandishi wa habari hii alipata kumtembelea marehemu alipokuwa amelazwa kwa Dk Mvungi wiki tatu zilizopita. Blog inawapa pole watoto,wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu!

MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI! AMIN


Chanzo cha habari na picha Hizza Kamanga,Grace Mmari, Houston Texas/ Tausi Khalid Dar, Tanzania.

Bibi afariki saa 48 baada ya kujua wajukuu zake wamefika hospitali kumuona!

Katika hali ya kusikitisha Mama Hawa Haji Kamanga (71) alifariki leo hii saa 2.40 Hospitalini Ocean Road  baada ya kupigania uhai wake kwa siku kadhaa alizokuwa na hali mbaya sana lakini ilielekea alipigana kubaki hai mpaka pale wajukuu zake wawili walipofika toka America siku ya Jumamosi na kwenda moja kwa moja Ocean Rd Hospital kumuona Bibi yao. Wajukuu zake hao Kaela Jr (3)na Hadassah Bianca (1) walipofikishwa wodini Marehemu akaambiwa wajuu zako wamekuja kukuona inasemekana marehemu aliyekuwa na hali mbaya kwa wakati huo alitabasamu na kujaribu kusema kitu lakini hakuweza kutoa sauti, lakini bila shaka alifurahi kujua hatimaye wajukuu zake wamemkuta akiwa hai, na hatimaye akaamua muda ulikuwa sahihi kuacha kupigania uhai wake. Mama Hawa Kamanga ana watoto kadhaa wanaoishi nchini Marekani. Marehemu alilazwa Ocean Road wiki mbili hivi baada ya kuhamishiwa hapo kutokea katika hospitali ya Dk Mvungi ambako alilazwa kwa uchunguzi wa awali. Kwa sasa mipango ya mazishi inafanyika na tutaendelea kufahamishana humu na kwingineko.
    Inna Lillah wa inna illahi Rajiun!