Maandalizi ya hafla ya Mh Samuel Sitta kutangaza nia ya kugombea urais yaiva!

Maandalizi ya hafla ya Mh Samuel Sitta kutangaza nia ya kugombea urais yaiva!

Baadhi ya waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari wa mkoani Tabora na wa nje ya mkoa wakiwasili Itetemia

Hatimaye Mh Samuel Sitta leo atatangaza nia kijijini kwao Itetemia ambako atatambikiwa kimila na kupewa cheo cha Mwizukulu mkulu ikimaanisha (mjukuu mkubwa) Samuel Sitta ni mjukuu wa mtemi wa zamani wa Unyanyembe Marehemu Mtemi Saidi Fundikira baada ya kutambikiwa hapa Ikulu ya Unyanayembe ndipo atatangaza nia ya kuomba kuteuliwa na CCM ili agombee urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Samuel Sitta ni mwanasiasa mkongwe hapa nchini Tanzania. Matangazo ya hafla hii yanarushwa moja kwa moja na VOT FM 89.0 ya mjini Tabora pamoja na Radio one stereo.

Wanyanyembe wakiwasili katika Ikulu yao Itetemia
Baadhi ya viongozi wa ngoma ya Uswezi

Apolo, Salu SECURITY na Adam Fundikira wakiwa Itetemia
Mbunge wa Tabora mjini Mh Aden Rageh akiwasili Itetemia
Mh Rageh akikaribishwa na kiongozi wa CCM mkoa wa Tabora


Waswezi
Ngoma za Lugaya






Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira
Wayege wakicheza ngoma


Habari na picha kwa hisani ya 
Mkala Fundikira wa TBN central zone