Bw Richard Barklie akihutubia kongamano la haki za binadamu nchini India |
Bw Barklie ambaye pia ni mkurugenzi katika taasisi ya hiari mjini Belfast Northen Ireland ya WAVE TRAUMA CENTRE ameshasimamishwa kazi na taasisi hiyo kupisha upelelezi.
Barklie ambaye ni mmiliki wa tiketi ya msimu ya Chelsea fc akiwa na wenziwe watatu walimsukuma Bw Syla asiingie ndani ya treni (METRO) huku wakiimba (we are racists we are racists this is how we ike it) Sisis ni wabaguzi na hivi ndivyo tupendavyo. Police nchini England imeshawatambua watuhumiwa lakini hakuna aliyekamatwa mpaka sasa, Idara hiyo ya polisi imeeleza upelelezi utaingia hatua inayofuata.
Hata hivyo kupitia mwanasheria wake Bw Barklie amakanusha kuhusika na vitendo vya kibaguzi vilivyotokea siku hiyo lakini anakiri kuwepo eneo la tukio, na amedhamiria kujisafisha.
Metropolitan police pia imeeleza haiwezi kukamata mtu kwa makosa aliyoyafanya nje ya Uingereza, kwa mawazo yangu basi bila shaka Polisi ya Paris itabidi iiombe serikali ya England washukiwa wapelekwe Ufaransa kwa mahojiano na pengine kushtakiwa iwapo itaonekana wana kesi ya kujibu.
Kilabu cha Chelsea kupitia meneja wa timu Jose Mourinho kimeelzwa kusikitishwa na tukio hilo na kuwa kitawafungia wote watakapatikana na kesi ya kujibu. Taarifa ya msemaji wa kilabu hicho cha jijini London ameelza kuwa mmiliki wa timu hiyo Bw Roman Abramovich ametiwa kinyaa na kitendo hicho. Pia kilabu hicho kimeshamkaribisha Bw Syla London katika mchezo wa marudiano kati ya timu hizo mbili.
Picha ya Bw Barklie iliyochukuliwa toka cctv. |
Hotuba India |
Barklie akiwa katika harakati za haki za binadamu barani Afrika. |
Bw Suleyman Syla ndiye mhanga wa tukio la kibaguzi lililotokea stesheni ya treni za chini ya ardhi (METRO) jijini Paris Ufaransa. |