mkalamatukio

Mama Samia Suluhu Awasili Kigoma, Wananchi Wasimamisha Shughuli Kumlaki

Baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan Kata ya Igagala, Uvinza Mkoani Kigoma wakimtaka awasalimie kabla ya kuendelea na safari. Mgombea mwenza huyo wa CCM ameingia mkoani Kigoma kwa ziara ya kampeni kuinadi ilani ya CCM.

Baadhi ya Wananchi wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara kumlaki mgombea mwenza wa urais CCM alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma kufanya mikutano yake ya kampeni.
Mgombea mwenza akizungumza na wananchi waliomsimamisha njiani kuwasilisha kero zao.
Mgombea mwenza CCM, Mama Suluhu akiwa ameshikilia kadi na bendera za vyama vya upinzani alizokabidhiwa na vijana waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM, alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma mwisho wa reli.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan Kijiji cha Mlyabibi, Mkoani Kigoma wakimtaka awasalimie kabla ya kuendelea na safari. Mgombea mwenza huyo wa CCM ameingia mkoani Kigoma kwa ziara ya kampeni kuinadi ilani ya CCM.
Wananchi na wanaCCM wakimshangilia mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili mkoani Kigoma kuanza ziara yake ya kampeni. Mama Suluhu kawasili mkoani Kigoma na kufanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kigoma Kusini, Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Baadhi ya vijana waliohama kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na CCM wakiwa wamemnyanyua juu mmoja wa viongozi aliyewashawishi kujiunga na chama hicho mara baada ya kupokelewa na mgombea mwenza wa CCM kwenye mkutano wa kampeni mjini Uvinza Kigoma. Zaidi ya vijana 60 wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Kata ya Uvinza, Himid Kisobwe wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mama Samia Suluhu.
Vijana waliojiunga na CCM kutokea chama cha NCCR-Mageuzi wakishangilia mara baada ya kumpokea Mama Samia Suluhu katika mkutano wa hadhara. Zaidi ya vijana 60 wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Kata ya Uvinza, Himid Kisobwe wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mama Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Community Center Jimbo la Kigoma Mjini.
Burudani baada ya mapokezi ya mgombea mwenza kuwasili mkoani Kigoma.
Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba (kulia) akisalimiana na mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia wanaCCM na wananchi katika Uwanja wa Community Center Jimbo la Kigoma Mjini.

Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia wanaCCM na wananchi katika Uwanja wa Community Center Jimbo la Kigoma Mjini. 

Picha na www.thehabari.com/Kigoma.

Harusi ya mwana TBN Dickson Busagaga ilivyofana!


dickson busagaga & salome mhozya wedding (9)
Dickson Busagaga na Salome Mhozya katika picha baada ya kufunga ndoa iliyowafanya kuungana na kuwa mwili mmoja tukio lililofanyika katika kanisa la Mt. Teresia wa Mtoto Yesu jimbo kuu la Tabora mnamo tarehe 23 Sep, 2015.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (8)
Waharusi (Dickson na Salome) wakionesha pete zao mara baada ya kuungana na kuwa kitu kimoja.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (2)
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao, hata walipoingia ukumbini katika sherehe ya usiku walidhihirisha kuto kubahatisha kuungana kwao.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (3)
Furaha ilitawala sana miongoni mwao na waalikwa wote.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (4)
dickson busagaga & salome mhozya wedding (5)
dickson busagaga & salome mhozya wedding (6)
MC Ndagula katika ubora wake wa kazi.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (7)
ZIFUATAZO NI PICHA ZA SENDOFF ILIYOFANYIKA TAREHE 19/09/2015 ORION

(TABORA HOTEL)

salome_mhozya_sendoff (1)
Picha ya pamoja ya maids, matron na aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa
salome_mhozya_sendoff (2)
salome_mhozya_sendoff (3)
Mrs Patrick na Salome (aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa) wakiingia ukumbini
salome_mhozya_sendoff (4)
salome_mhozya_sendoff (5)
salome_mhozya_sendoff (6)
salome_mhozya_sendoff (7)
salome_mhozya_sendoff (8)
Wazazi wa Salome wakisalimia waalikwa katika sherehe za kumuaga mtoto wao Salome.
salome_mhozya_sendoff (9)
salome_mhozya_sendoff (10)
Wanakamati katika ubora wao wa kukabidhi zawadi za kamati
salome_mhozya_sendoff (11)
Dickson Busagaga, Mume halala wa Salome.
salome_mhozya_sendoff (12)
Bw. Patrick (Best man)
salome_mhozya_sendoff (13)
salome_mhozya_sendoff (14)
salome_mhozya_sendoff (15)
salome_mhozya_sendoff (16)
salome_mhozya_sendoff (17)
salome_mhozya_sendoff (18)
salome_mhozya_sendoff (19)
Picha na aloyson.com -TBN Tabora

Kalapina aunguruma Mtambani kata ya Mzimuni!

Karama Masoud aka Kalapina akihutubia wakazi wa eneo la Mtamba kata ya Mzimuni leo jioni







Mwanaharakati Kalapina akimwaga sera kwa wakazi wa Magomeni Mikumi leo

Picha na Hassan Kachloul

Zetrida Ezekiel atoka na Ringa na Yesu!


Zetrida Ezekiel ni mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili aishiye mkoani Kigoma, amekuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili ambaye ni mwana kwaya wa  kikundi maarufu na kikongwe cha nyimbo za injili cha MKE MWEMA cha mjni Kigoma. Zetrida ameolewa na ni mama wa watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.

Lakini baada ya kupata rai nyingi na kwa muda mrefu toka kwa wachungaji wake na watu mbali mbali kuwa atengeneze albamu yake kama mwanamuziki wa kujitegemea,hatimae mwezi wa August mwaka huu Zetrida alikuja Dar es Salaam na kuanza kazi ya kutengeneza albam yake binafsi.
Zetrida Ezekiel akiwa katika pozi.



Album yake inayoitwa Ringa na Yesu ina nyimbo nane na nyimbo zote amezifanyia Tika records chini ya mtayarisha muziki maarufu nchini aitwaye Ephraim Kameta ambapo nyimbo sita katika albam yake hiyo zilitengenezwa na Kameta na mbili zikitengenezwa mtayarisha muziki machachari PG zote katika studio za Tika records pia. Katika albam hiyo kuna nyimbo kama Ringa na yesu liyobeba jina la albam Malaika, waombee maadui zako na nyingine nyingi zenye kiwango cha hali ya juu.

Akiongea na mtandao huu kwa njia ya simu Zetrida alipoulizwa ana mipango gani ya kufanya video ya albam hiyo Zetrida alisema "Natamani sana hata leo nianze kuandaa video lakini pesa inagomba kwa saa hasa baada ya kutoka kuandaa albam hii ya audio ambaye imechukua pesa nyingi kuandaa, inabidi nijpange tena kwanza"
Na alipoulizwa nini mipango yake ya baadae baada ya lutoa albamhiyo alisema "Mipango yangu ya baadae ni kumtangaza Yesu ndani na na nje ya Tanzania kwa kuwa ni kitu kilicho ndani ya damu yangu" Pia alielezea changamoto alizokutana nazo wakati akitayarisha albam hiyo ni pamoja kutofanya kazi kwa wakati uliopangiwa jambo ambalo hutokana na sababu mbali mbali ikiwemo katikizo la umeme, ambapo inatokea kazi iliyokuwa ifanyike jana inahamishiwa leo na wa leo ama utafanya kazi mida mibaya au kupangiwa siku nyingine. Lakini nashukuru sana kuwa nimeeza kumaliza albam hiyo bila tatizo.

Mwisho kabisa Zetrida alipenda kutoa shukurani zake akisema "Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa ujasiri wa kufanya albam yangu mwenyewe na pili mume wangu kwa kuniruhusu kufanya kazi hii ya uimbaji pia kujitoa kwake kwa hali na mali, vile vile bila kumsahau Mchungaji Joseph Malumbu wa Kijichi Mtongani ambaye alihusika katika usimamaizi wa albam ya Ringa kwa Yesu. Pia niwaombe tu wapenzi wa muziki wa injili waipokee albam yangu na wainunue kwa wingi kwani humo kuna nyimbo nzuri sana zenye kumtukuza Bwana Yesu hivyo kila mmoja ajipatie nakala yake sasa kwani tayari albami ipo madukani.
Kwa mialiko popote ndani na nje ya Tanzania wasiliana naye kwa nambari
+255675 406917/ +255756823477
au kwa barua pepe
zetridaezekiel@yahoo.com