mkalamatukio

Jumuiya ya marafiki wa Kinondoni yapata uongozi wa muda

Toka kushoto waliosimama ni Abdul Kazembe (mjumbe) Mahmoud Kamusi(Mjumbe)Adam Tuga Bush (mjumbe)
Toka kushoto waliokaa Florah Samuel (mweka hazina msaidizi) Suzane Bagilla (katibu mkuu) Yahya Poli (Mwenyekiti) Mkala Fundikira (makamu wa mwenyekiti) na Jully Kitundu (mjumbe)
Jumuiya ya marafiki wa Kinondoni (Kinondoni Group) jana ilifankiwa kufanya mkutano wa kujadili na kuipitisha rasimu ya katiba na kuteua viongozi wa muda ambao walipewa jukumu la kuhakkisha jumuiya inapata usajili katika kipindi cha mwezi mmoja. 

Kikao hicho kilichoendeshwa na mwenyekiti wa kikao Bw Yahaya Poli kilikuwa na ajenda mbili 

1. Kuijadili na kuipitisha rasimu ya katiba ya jumuiya hiyo.
2. Kuteua viongozi wa na kamati tendaji ya muda.

Mkutano huo ulifanikiwa kuijadili na kuipitisha katiba hiyo pia mkutano uliwateua Bw Yahaya Poli kuwa mwenyekiti, Mkala Fundikira kuwa makamu wa mwenyekiti, Suzzane Bagila kuwa katib mkuu, Bw Ivan Minja kuwa katibu msaidizi na Ismail Kagambo kuwa mhazini mkuu akisaidiwa na Anna Samuel, vile wanajumuiya wanne waliteuliwa kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji ambao ni Abdul Kazembe, Jully Kitundu, Adam Bush na Mahmoud Kamusi. Hawa wanaungana na uongozi na kuwa 10 wanaunda kamati ya utendaji itakayokuwa chini ya Mwenyekiti Yahaya Poli. Dhumuni la kuanzisha jumuiya hiyo ni kujiunga pamoja na kusaidiana na kuwekeza katika fursa mbali mbali zitakazojitokeza

Akizungumzia uteuzi wake Bw Poli alisema"Napenda niwashukuru wajumbe wote wa mkutano huu kwa kuniamini na kunipa fursa ya kuiongoza jumuiya ya Kinondoni, naahidi kuitendea haki fursa hii na kuiongoza jumuiya kuelekea maendeleo ya ki uchumi na kijamii. Na naahidi kujitoa kwa hali na mali ili kuona tunapiga hatua za ki maendeleo siku hadi siku. Vile niwashukuru waratibu wetu Bw Ivan Minja na Bw Mkala Fundikira kwa kutukutanisha hapa leo, nitawaomba waendelee na moyo huo huo na jumuiya itafika mbali ki maendeleo.Alimaliza.

Jumuiya hiyo ina wanachama zaidi 2300 katika mtandao wa Facebook inakojulikana kama Kinondoni Group, ambapo iliasisiwa na Bw Ivan Minja huku Bw Mkala Fundikira akiendesha kundi la Telegram kupitia simu za mkononi. Makamu mwenekiti wa jumuiya hiyo alisema kamati tendaji imepewa kazi ya kuhakikisha jumuiya inasajiliwa ili wanachama wengi zaidi wa Kinondoni Group katika mtandao wa kijamii wa Facebook waweze pia kupata fursa ya kujiunga na jumuiya yao ya marafiki wa Kinondoni na wafaidike na matunda yote yatakayotokana na kuwa mwanajumuiya hai. Kikao hicho kilichofanyika Mamaz Tavern(Mamaz pub zamani) kilihudhuriwa na wanajumuiya 16 huku wengine wengi wakitoa udhuru kadhaa.
Mwenyekiti mteule Yahaya Poli akisisitiza jambo katika mkutano wa jana.
Makamu wa mwenyekiti (katikati) Mkala Fundikira na katibu Suzzy Bagilla (kulia) wakimsikiliza mwenyekiti.

Toka kushoto ni Fatyy Dula, Dada Rukia, Emmy Stephen, Dada Mariam, Ivan Minja na Kaka Poli

Toka kushoto ni Adam Bush, Florah Samuel, Mahmoud Kamusi na Abdul Kazembe.


Mudrikati Swedi kulia na suzzy Bagila.

Dax kushoto na Issa Mndeme wakifuatilia kikao.
Makofi kidogo.
Dada Jully Kitundu na Adam Bush.
Rukia Mussa na Emmy Stephen.
Picha ya pamoja





Picha na Camilius Kamili wa mkalamatukio blog

WAZIRI HAWA GHASIA AZINDUA MAFUNZO YA MADEREVA WA MABASI YA MWENDO WA HARAKA DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika  Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akijaribu kuendesha moja ya basi la mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika  Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam
 Babasi ya wendo wa haraka yaliyoingia nchini kutoka nchini china,
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Askari wa usalama barabarani wakipiga picha mabasi hayo.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Mohamed Mpinga (kushoto), akibadilishana mawazo na wadau wa usafirishaji kabla ya uzinduzi huo.
 Meza kuu hiyo ikiwa na viongozi mbalimbali.
 Msemaji  wa Mradi wa DART, Sabri Mfuruki, akizungumza (katikati) akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji, William Masanja. 
 Wanahabari wakichukua taarifa katika uzinduzi huo.
 Wakufunzi wa kutoa mafunzo kwa madereva hao kutoka China wakitambulishwa.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi ndani ya mchuma wakati wa uzinduzi huo. Hapo wanakwenda Kimara kutoka Ubungo na kisha kurudi Ubungo 'Hakika na Raha tupu'
Wanachi na wadau wengine wakiangalia mabasi hayo.


Dotto Mwaibale

MADREVA waliobahatika kuanza kupata mafunzo ya kimataifa ya kuendesha mabasi ya mwendo wa haraka chini ya mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka (DART), wametakiwa kuzingatia mafunzo hayo kwa makini.

Mwito huo umetolewa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, wakati akizinduzi mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika  Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo.

"Mafunzo mtakayopata nawaombeni muyapokee kwa bidii na umakini mkubwa kwani yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa" alisema Ghasia.

Ghasia alisema mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa  mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo hayatalenga tu kuendesha magari bali pia namna ya kuwahudumia wateja.

Alisema anaamini mafunzo hayo yatawejengea madereva hao weredi na dinadhamu katika kazi yao ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kuandamwa na utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alisema mradi huu wa mabasi yaendayo kasi ni mradi wa aina yake hapa nchini na barani Afrika kwa ujuma na utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi na ni msingi wa maendeleo ya nchi.

Mahitaji ya madereva wanao hitajika katika mradi huo ni 330 na kuwa mradi huu ulioanza ni wa awamu ya kwanza na utakuwa wa awamu tano.

NHIF yawataka bloggers kujiunga na mfuko wa bima ya afya!

           1 
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akifungua semina ya kati ya mfuko huo na Ma blogger wanachama wa Chama habari za mitandao ya kijamii Tanzania Bloggers Nertwork TBN inayofanyika katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kurasini TEC jijini Dar es salaam, Katika semina hiyo mablogger hao wameaswa kujiunga na huduma ya KIKOA ili kujihakikishia huduma bora za afya zinazotolewa na mfuko huo kupitia bima hiyo, Katika picha kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mablogger TBN Bwana Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa Chama hicho Bi. Khadija Khalili.
2
Mhariri wa mtandao wa Bagamoyo News Bw. Sayed Abdul akitoa shukurani kwa niaba ya Mablogger mara baada ya mgeni rasmi kufungua semina hiyo inayofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Maaskofu.
3
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza katikasemina hiyo wakati alipokuwa akitoa mada kwa wana TBN inayofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Maaskofu.
4
Mmiliki wa Blogu ya K-VIS Blog Khalfan Said akishiriki katika semina hiyo pamoja na washiriki wengine.
5
Baadhi ya mablogger wakishiriki katika semina hiyo.
6
Robert Okanda kushoto na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.
IMG_5316
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti kulia Rachel Palangyo katikati na John Kitime wakiwa katika semina hiyo.

Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya Tabora


Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.
Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.



Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum.
Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.

Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
Team Irene wakifuatilia mchakato
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN central zone