mkalamatukio

Mratibu wa asasi ya Better Living Aid atoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi!


Watangazaji Hamisa Mussa Lubilo na Deogratius Yagomba wa VOT fm 89.0 wakimuuliza maswali mratibu wa asasi ya Better Living Aid walipomualika leo asubuhi katika kipindi cha Meza huru!
Mratibu wa asasi ya kiraia ya Better Living Aid Bw Mkala Fundikira leo akiwa amavalia fulana ya mkakati wa Imetosha unaopinga mauaji dhidi ya watu wenye ualbino ambao yeye ni mjumbe wa kamati kuu, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi mjini Tabora waiunge mkono asasi yake inayodhamiria kujenga vyoo na zahanati katika kijiji  cha Amani kilichopo Ipuli Tabora, kijiji chenye wakazi wazee na wasiojiweza na waishio na gonjwa sugu la ukoma. Alitoa wito huo akiongea katika kipindi cha meza huru cha Vot fm89.0 alisema "nawaomba wenye maduka ya vifaa vya ujenzi watuunge mkono kwa kuchangia hata mifuko mitano ya simenti, bati mbili au hata kifaa chochote cha ujenzi ambacho kitataumika katika ujenzi wa vyoo na zahanati katika kijiji hicho alimradi tunahitaji michango ya aina yeyote ile" 
Mkala Fundikira akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na watangazaji wa kipindi cha Meza huru, kipindi kinachoruka ktk kituo cha redio cha VOT fm 89.0 ya Tabora leo asubuhi.
Pamoja na kueleza kuwa asasi yao inayoundwa na marafiki toka mitandao ya jamii kama Facebook  na Viber pia alieleza kuwa tangu waanze kusadia kijiji hicho washapeleka vyakula, vyandarua na masweta kwa nyakati tofauti, pia ikiwemo kulipia upulizwaji wa dawa za kuuwa wadudu pamoja na kunguni ambao walikuwa wakisumbua wakazi wa kijiji cha Amani. 
Mkala akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wenye kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino ya mkakati wa Imetosha.
Alipoulizwa dhamira ya asasa yao ni kusaidia Tabora tu au na mikoa mingine? Mratibu huyo alijibu "Hapana, Better Living Aid itasaidia na kwingineko pia, kwa mfano tunatafuta wahisani ili tukajenge zahanati kijijini Masweya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Masweya hakuna zahanati pamoja na kuwa pana wakazi zaidi ya 7000, nafikiri wa Tanzania tuwe wahalisia kuwa serikali yetu haitoweza kukidhi mahitaji ya wa Tanzania wote kwa wakati mmoja hivyo basi ni wakati muafaka wa sisi kama jamii kuanza kujitolea na kuwezesha asasi kama yetu kupeleka huduma za afya sehemu kama Masweya"

Fundikira pia alimshukuru Mh Munde Tambwe Abdallah kwa kutoa ahadi ya Mifuko 50 ya simenti, lori 10 za mchanga pamoja na tano za mawe na kokoto , alisema "Tena kabla sijasahau nimpongeze na kumshukuru sasa sana sana Mh Munde Tambwe kwa kutupa msaada ambao ni msingi, kwa maana ya kuwa ahadi yake ndiyo itaanzisha ujenzi wa majengo hayo ya vyoo na zahanati, hivyo basi na wengine wajitolee ili tusonge mbele" 
Hoteli ambamo chakula cha usiku cha uchangishaji fedha kwa ujenzi wa vyoo na zahanati utafanyika baadae mwezi huu jijini Dar es Salaam iliyopo maeneo ya Ocean road.
Aidha asasi hiyo ina mpango wa kuandaa chakula cha usiku jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Southern Sun baadae mwezi huu ambapo Mh Samuel Sitta(waziri wa uchukuzi) amekubali kuwa mgeni rasmi, karamu hiyo itaandaliwa ili kuchangisha fedha za kuwezesha miradi hiyo iweze kukamilika. "Bado tupo kwenye hatua za mwanzo za maandalizi lakini tunataraji karamu hiyo ya uchangishaji pesa ifanyike ama mwishoni mwa mwezi wa MEI au mwanzoni mwa mwezi Juni 2015. Pia Fundikira aliwashukuru Mh Aden Ragen(Mbunge wa Tabora mjini), Mh Munde Tambwe(Viti maalum), Sylvester Koka(Mbunge wa Kibaha) na wanachama na wote wa Better Living Aid kwa kuwezesha kifedha upulizwaji wa dawa kijiji cha Amani uliogharimu Tsh Laki 980.

Tembelea mtandao wa betterlivingaid.Blogspot.Com ujue zaidi kuhusu asasi hii na malengo yake au piga namba 0754 666620 kwa maelezo.

MBUNGE NDESAMBURO NA MEYA WA MOSHI JAFARY MICHAEL WAENDELEA NA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA MOSHI MJINI.

Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika jirani na Super Market ya Nakumat.
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo wakimsikiliza Ndesamburo.
Ndesamburo akizungumza.
Baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakimsilikiza Ndesamburo.
Msatahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara .
Mbunge waMoshi mjini Philemoni Ndesamburo akimsikiliza Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi.(hayuko pichani) akiwa na viongozi wengine wa Chadema.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.

MASHINDANO YA LUCY OWENYA CUP YAZINDULIWA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI.


Mbunge wa viti Maalumumkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akiwasili katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini na kushirikisha kata 16 za jimbo hilo.
Baadhi ya wananchi waliohudhulia ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.
Mbunge Owenya akicheza ngoma katika shrehe za ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup.
Baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo zikiwakatika uwanja wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya uunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.
Mratibu wa mashindano hayo,Charles Mchau akizungumza jambo katika ufunguzi wa mashindano hayo.
Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro, Lucy Owenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 ,Mashindano yaliyoanza katika jimbo la Moshi vijijini yakishirikisha kata za Jimbo hilo.
Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya akisalimianana mwamuzi Batista Mihafu wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.
Mbunge wa Viti maalumu ,Lucy Owenya akikagua baadhi ya timu zinazpshiriki mashindano hayo .
Mbunge Lucy Owenya akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro ,Lucy Owenya akisalimiana na mmoja wa wachezaji wanaoshiriki mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 yaliyozinduliwa juzi katika jimbo la Moshi vijijini na kushirikisha timu kutoka kata 16 za jimbo hilo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Hatimaye wakazi wa kijiji cha Amani Tabora usiku wa leo watalala bila kero ya kunguni!

Kijji cha Amani kinavyoonekana
Taasisi ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal Nsyepa General Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za jijini Dar es Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu kama kunguni na wengineo katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa Tabora. Hatua hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye uathirika wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia wakazi wa hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine wajengewe vyoo zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye hali ya kutumika, huku vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka. Akiongea na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo alisema"kwa kweli tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada huu, kwani tumekuwa tukilala kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala kwa raha kama watu wengine" pia aliongeza "Ila tu jamani msituchoke, bado tunakumbushia ombi la kujengewa vyoo zaidi kwani idadi yetu na ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni changamoto, lakini pia tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na muuguzi wapate mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"

Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.

Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya. 

Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.

Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa

Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa
Hpa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro

Job DONE

Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini


Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa
Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho
Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo.

Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa  kunguni na wadudu wengine.
Rundo la mahindi likiwa limotolewa nje kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni nani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa.
Baadhi ya panya waliokutwa ndani ya chumba cha mkazi mmoja wa kjijini hapo leo.
Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid Mkala Fundikira kushoto akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma.

Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa.
Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji
Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita  kiasi.
Habari na picha kwa hisani ya TBN Central zone!