mkalamatukio

Leo ndio leo Malkia wa Miss Dar Indian Ocean kupatikana leo!

 Warembo wa Miss Dar Indian Ocean jana walitembelea Club Billicanas kujinadi kwa mara ya mwisho ambapo leo watachuana vikali kuwania taji la Miss Dar Indian Ocean. Shindano hilo litafanyika leo usiku kuanzia saa 2 katika viwanja vya Nyumbani lounge ambapo viingilio kwa viti vya kawaida ni Tsh 10,000/= na zile za VIP zikipatikana kwa Tsh 30,000/=. Shindano hilo limedhaminiwa Konyagi kupitia kinywaji chake cha Zanzi, CXC Africa, Tsn Super market, Redds Original,TBC, Channel 10, Blog ya wananchi, Nyumbani Lounge. Chini ni picha za baadhi ya warembo wa shindano hilo.
Msaidizi wa Matron wa warembo Miss Baby James
Mjumbe wa kamati ya Miss Dar Indian Bw Khalid Mkwabi aka Dudu (Kushoto) akiwakaribisha mashabiki wa urembo katika show ya leo. Kulia ni Miss Baby James

Kamati ya Miss Tanzania yatembelea kambi ya Redds Miss Dar Indian ocean!

Kamati ya Redds Miss Tanzania jana jioni ilifanya ziara katika kambi ya Redds Miss Dar Indian Ocean iliyopo katika Hoteli ya Chichi wilayani Kinondoni, jijini Dar. Ziara yao ilikuwa ni pamoja na kuwafunda warimbwende hao na kuwapa muda warembo hao wa kuuliza maswali kadha wa kadha. Kilele cha shindano hilo la Miss Dar Indian Ocean kitafanyika jumamosi tarehe 7/6/2014 katika viwanja vya Nyumbani Lounge. Warembo hao leo hii mchana watakuwa na pre judgement itafanywa na kamati ya Redds Miss Kinondoni chini ya muandaaji wa kanda hiyo Bw Innocent Melleck. Chini ni picha za tukio hilo
Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu Miss Tanzania Bw Hashim Lundenga, Mkuu wa itifaki na nidhamu Bw Albert Makoye na wakala wa Miss Kinondoni Bw Innocent Melleck katika
Katibu wa Miss Tanzania Bw Bosco Majaliwa na Bw Hashim Lundenga
Wakala wa zamani wa Miss Knondoni Bw Yusuf Omary aka Boy George akiwa na matron wa Miss Dar Indian Ocean Husna Maulid Miss Kinondoni no2 2011 
Baadhi ya warembo wa Kutoka kushoto Mariam Salum, Hasnat Hussein na Janet Geofrey wakimsikiliza Bw Hashim Lundenga, kamati ya Miss Tanzania ilipotembelea kambi yao jana jioni.
Wakala wa Miss Shinyanga Bi Asela Magaka
Wadau wa tasnia ya urembo 
Kutoka kushoto Albert Makoye, Innocent Melleck na Hidan Ricco(Afisa habari Miss Tanzania) 
Kutoka kushoto Miss Getrude Massawe, Sasha Deogratius, Camilla John, Suzzane na Shamila 
Tumepozi!

Mjumbe wa kamati Miss Dar Indian Ocean Bw Hassan Lema na wakala wa Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahma Yusuph
Bibi Rahma Yusuph
Mshirki wa zamani wa Miss Tanzania, wakala wa Miss Geita na mjumbe wa Miss Tanzania Bw Lucas

Washiriki wa Miss Dar Indian Ocean wajichua vikali kuelekea kilele cha shindano hilo!

Shamila Yusuf


Tazama picha za washiriki wa shindano la urimbwende la Miss Dar Indian Ocean 2014 wakiwa katika mazoezi ya mwisho kabla ya kilele cha shindano hilo jumamosi hii ya tarehe 7/6/2014 katika viwanja vya Nyumbani Lounge ambako bendi inayoundwa vijana wenye vipaji toka Tanzania house of talent (THT) watatumbuiza shindano hilo. Akiongea na blog hii muandaaji wa shindano hilo Bibi Rahma Yusuf anayeanda kupitia kamuni yake ya Rahmat Entertainments alisema maandalizi yote yapo sawa kinachosubiriwa ni ni siku saa na tarehe tu.  Viingilio ni Tsh 10,000/= viti vya kawaida na Tsh 30,000/= kwa viti maalum(VIP), onesho litaanza mnamo saa 2 za usiku mpaka majogoo. Washiriki hao wapo ya mkufunzi wao Miss Husna
Miss Sophia
Miss Mary Shila 
Joyce James 
Monica Nshimba
Miss Sasha Deogratius
Miss Hasnat Hussien
Janet Geofrey

Miss Getrude Massawe
Miss Mariam Salum
Miss Suzzane SAWAYA
Miss Ayaan Abdul
Miss Camilla John

Miss Dar Indian Ocean patakuwa hapatoshi!

Muandaaji wa Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahama Yusuph
Baada ya kufanya shindano la vipaji kwa mafanikio makubwa mnamo tarehe 23/5/2014 ambapo washiriki watano waliiingia fainali, sasa shindano la Miss Dar Indian Ocean litafanyika jumamosi ya tarehe 7/6/2014 katika viwanja vya Nyumbani Lounge, kiaina inaelekea waandaaji wamejipanga vema sana nadau na mashabiki wa tasnia hii wameombwa kujitokeza kwa wingi siku ya tukio ambapo wakali wa THT watatumbuiza hafla hiyo.

Baadhi ya wageni waliohudhuria shindano la vipaji Miss Dar Indian Ocean!

Mfanyabiashara Teef Fundikira akiteta kitu na Mkurugenzi wa kampuni ya Aset Bibi Asha Baraka.
Mdau wa tasnia ya urembo Bi Hawa  Mkamba(kulia) akiwa na rafiki yake.
Kutoka kushoto Asha Baraka, Mkurugenzi wa Lino International inayoandaa shindano la Miss Tanzania na Khadija Kalili muandaaji wa Miss Pwani
Mfanyabiashara Bw Hassan akiwa na muandaaji wa Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahma Yusuf.


Shindano la Miss Dar Indian Ocean litafanyika jumamosi ya tarehe 7/06/2014 katika ukumbi wa Chichi Hotel, Kinondoni.
Wadau wa urembo wakifuatilia onesho hilo kwa umakini mkubwa! 
Wazee wa kazi: Hashim Lundenga na Bw Bosco Majaliwa
Mkuu wa itifaki na nidhamu Bw Ephraim Makoye
Toka kushoto Hassan, Hidani Ricco na Boy George(Muandaaji wa zamani wa Miss Kinondoni) 

Wajue top five wa vipaji Miss Dar Indian Ocean!

Shindano la urembo la Miss Dar Indian Ocean likiwa linakaribia, siku ya ijumaa  tarehe 23/5/2014 wapenzi wa tasnia ya urembo jijini Dar na wilaya zake walishuhudia mchuano mkali wa kugombea ushindi wa kipaji katika ukumbi wa Chichi hotel ambapo warembo watano kati ya 15, walifanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la kipaji zitakazofanyika siku ya kumtafuta Miss Dar Indian Ocean ambayo ni Jumamosi ya tarehe 7/6/2014 katika ukumbi huo huo maridhawa wa Chichi hotel. Onesho hilo lilihudhuriwa na kamati ya Miss Tanzania pamoja na Miss Tanzania 2012 Salha Israel, pamoja na wadhamini kama CXC na wengine wengi. Dalili zinaonesha show ya Miss Dar Indian Ocean itakuwa si mchezo kwani kwa onesho dogo tu la kipaji ukumbi na jukwaa vilipambwa vilivyo na kampuni maaurfu ya Vayle Springs. Mtandao huu ulipoongea na muandaaji wa shindano hilo Bibi Rahma Yusuf ambaye anaanda shindano hilo kupitia kampuni yake ya Rahmat Entertainments alisema kwa kujiamini "Hii ni trela tu muvi yenyewe ni tarehe 7June ukikosa show hiyo bora uhame mji" Onesho hilo la vipaji lilidhaminiwa na Chichi hotel.
Kutoka kushoto ni Suzzete Fetrick, Mary Amos, Sasha Deogratius, Camilla John na Getrude Massawe, hawa ndio walioingia fainali za Miss Dar Indian Ocean Talent show.
Judges: Kutoka kushoto ni jaji Hassan, Husna Sajent na Iddi Zonki
Kutoka kushoto ni muandaaji wa Miss Mwanza Bw Dotto, Yusuf Omari aka Boy George, Salha Israel na katibu wa Miss Tanzania Bw Bosco Majaliwa wakifuatilia kwa makini shindano la vipaji.

Picha zaidi za semina ya Redds Miss Tanzania!

Kulia ni wakala wa Redds Miss Njombe
Tunachukua notice
Tom Chilala mwenye shati jeupe na Khadija Kalili kushoto kwake


Hidan Ricco na Ephraim Makoye wa kamati ya Miss Tanzania

Kulia ni wakala wa Miss Singida 
Baadhi ya waandaji mawakala wakifuatilia semina kwa umakini
Muandaaji wa Redds Miss Temeke Bw Kisaka na William Malecela wa Blog ya wananchi.