mkalamatukio

Bibi afariki saa 48 baada ya kujua wajukuu zake wamefika hospitali kumuona!

Katika hali ya kusikitisha Mama Hawa Haji Kamanga (71) alifariki leo hii saa 2.40 Hospitalini Ocean Road  baada ya kupigania uhai wake kwa siku kadhaa alizokuwa na hali mbaya sana lakini ilielekea alipigana kubaki hai mpaka pale wajukuu zake wawili walipofika toka America siku ya Jumamosi na kwenda moja kwa moja Ocean Rd Hospital kumuona Bibi yao. Wajukuu zake hao Kaela Jr (3)na Hadassah Bianca (1) walipofikishwa wodini Marehemu akaambiwa wajuu zako wamekuja kukuona inasemekana marehemu aliyekuwa na hali mbaya kwa wakati huo alitabasamu na kujaribu kusema kitu lakini hakuweza kutoa sauti, lakini bila shaka alifurahi kujua hatimaye wajukuu zake wamemkuta akiwa hai, na hatimaye akaamua muda ulikuwa sahihi kuacha kupigania uhai wake. Mama Hawa Kamanga ana watoto kadhaa wanaoishi nchini Marekani. Marehemu alilazwa Ocean Road wiki mbili hivi baada ya kuhamishiwa hapo kutokea katika hospitali ya Dk Mvungi ambako alilazwa kwa uchunguzi wa awali. Kwa sasa mipango ya mazishi inafanyika na tutaendelea kufahamishana humu na kwingineko.
    Inna Lillah wa inna illahi Rajiun!

Shabiki wa Arsenal apoteza nyumba baada ya Man United kuishinda Gunners!

Hali mbaya
Robin Van Persie akiwazamisha The Gunners
Shabiki mkereketwa wa timu ya Arsenal (the Gunners) Mganda Henry Dhabasani mkazi wa jijini Kampala alijikuta akipoteza nyumba yake  dhidi Rashid Yiga ambaye aliweka dau la gari ya Toyota Premio na mkewe baada ya kudai Man united ingeifunga Arsenal bila shaka na wazee wa kijadi walikuwepo na kushuhudia dau hilo likipitishwa kwa maandishi kabla ya mchezo huo amabao mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Robin Van Persie alifunga bao pekee la mchezo katika kipindi cha kwanza na kuwasimamisha The Gunners katika mbio zao za kutaka kujikita zaidi katika usukani wa ligi hiyo maarufu na yenye msisimko kuliko zote duniani. Gazeti la Observer la Uganda lilieleza kuwa shabiki huyo Dhabasani mwenye wake watatu na watoto watano alizirahi baaada ya mchezo kwisha. Hata hivyo aliondoshwa katika nyumba yake siku iliyofuata.

[Video] KISOMO CHA MWISHO CHA MAMAA NYAWANA FUNDIKIRA MDA MFUPI KABLA YA MAZISHI

UHARAKA WA MUDA WA KUHAKIKISHA MWILI WA MAREHEMU UNAZIKWA ULIZINGATIWA TU MARA BAADA YA MWILI WA MAREHEMU KUWASILI TABORA MNAMO SAA 12 JIONI. KISOMO CHA MWISHO NA MAOMBI YA MWISHO ILIFANYWA KISHA KUELEKEA KATIKA MAZIKO YA MWILI WA NYAWANA FUNDIKIRA KATIKA MAKABURI YA ITETEMYA AMBAKO IKO IKULU YA MACHIFU WA UKOO WA FUNDIKIRA. 
ILIPOFIKA MUDA WA SAA 1:10 USIKU SHUGHULI YA MAZIKO ILIENDELEA NA KUHAKIKISHA MWILI WA MAREHEMU UMEPUMZISHWA.

*UMATI MKUBWA WA WATU ULITANDA PEMBEZONI MWA BARABARA WAKISHUHUDIA MSAFARA WA KUELEKEA KATIKA MAZISHI, ILIKUWA NI MAAJABU HAIJAWAHI TOKEA HAPO MKOANI*
UMATI WA WATU NJIANI KUELEKEA MAZISHI YA NYAWANA 
[TUNAOMBA RADHI KWA VIDEO HII KWANI HAIJACHUKULIWA KATIKA MAZINGIRA BORA, VIKWAZO VILIKUWA VINGI IKIWEMO MWENDOKASI WA GARI NA GIZA]

PICHA ZA MAZISHI YA NYAWANA FUNDIKIRA

MAMAA NYAWANA AMEPUMZISHWA KATIKA MAKAZI YAKE YA MILELE KATIKA MAKABURI YA ITETEMYA HAPA MKOANI TABORA, NJE KIDOGO NA MJI
MAZISHI YAMECHELEWESHWA KUTOKANA NA KUCHELEWA KUWASILI KWA MWILI HUO WA MAREHEMU

Umati unaosubiri mwili wa Nyawana umevunja rekodi!


Kadri muda uendavyo ndivyo watu wamezidi kufika ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo ya Gongoni, Tabora mjini. Hata hivyo mwili wake umechelewa kidogo kuwasili mjini hapa lakini watu wameendelea kujazana wakikaa juani bila taabu yeyote. Hii ni ishara kuwa watu wa Tabora walimkubali sana Nyawana ambaye wao walipenda kumwita Mamaa Nyawana au Jembe! kwani watu wapatao elfu moja wamejitokeza kushuhudia au kutoa heshima za mwisho kwa Nyawana.

Sheikh akitoa mawaidha mawili matatu kwa wahudhuriaji








Waombolezaji wakisubiri mwili wa Marehemyu Nyawana uwasili kutoka Dar es Salaam.






Chakula kikiandaliwa



Waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni kubwa kwa kuondokewa na kipenzi cha Tabora Mamaa Nyawana
Huzuni huzuni huzuni!

Voice of Tabora ( Vot fm 89.0fm) kurusha live shughuli za mazishi ya Nyawana Fundikira

Mac Denny akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa VOT fm 89.0  redio walipokuwa wakiwasilisha ubani wao kwa Baba mdogo wa marehemu Bw Adam Fundikira
Kituo cha redio cha Voice of Tabora kimejitolea kurusha Live shuhuli zote za mazishi ya marehemu Nyawana Fundikira ambaye aliwahi kufanya kazi katika kituo hicho kwa miaka kadhaa. Kituo hicho cha redio kinamilikiwa na Mh Aden Rageh mbunge wa Tabora mjini. Familia ya marehemu imepongeza hatua hiyo ya VoT fm kwani wapenzi wengi wa Mamaa Nyawana ambao hawatoweza kufika Tabora kumzika wataweza kufuatilia mazishi yake bila wasiwasi. Hongera Voice of Tabora 89.0 fm
 Fundi mitambo Dj Faster akiandaa urushaji Live shuhuli ya maziko ya Nyawana

Gari la matangazo live la Vot fm 89.0

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakimsikiliza ustaadh nyumbani kwa Baba mkubwa wa marehemu Nyawana Gongoni, Tabora.