mkalamatukio

Winga Adam Johnson atuhumiwa kubaka binti mdogo!

Mchezaji wa kiungo wa kilabu cha Sunderland Adam Johnson amesimamishwa na kilabu chake baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kujamiiana na msicha mwenye umri wa miaka (15).

Winga huyo mwenye miaka (27) anasadikika kupokea pauni 50,000 (Tsh milioni 1370) kwa wiki alikamatwa nyumbani kwake na polsi toka Durham katika hekalu lake lenye thamani pauni 1.8m mnamo siku ya jumatatu na baadae kupatiwa dhamana.

Kilabu cha Sunderland kimethibitisha kuwa kimemsimisha Johnson kupisha upelelezi, na hatua hiyo itaanza kazi jumanne ambapo Sunderland itacheza na Hull City katika mfululizo wa ligi kuu ya England Barclays Pemier league. Sunderland ilimsaini Johnson kwa pauni 10m toka Manchester city mwaka 2012. Imeelezwa kuwa winga huyo mwenye mtoto mmoja amekuwa akipenda kushobokewa na wasichana na ni mpenda starehe wa hali ya juu. 

Adam Johnson akiwa na mpenzi wake mwaka2012 Man City ilipotwaa ubingwa England.
Hapa akishangilia goli dhidi ya watani wa jadi New Castle
Hii ndio nyumba ambamo Adam Johnsona alikamatiwa na polisi wa Durham
Imetafsiriwa na Mkala Fundikira 
habari na picha mailonlinefootball

Tafrija ya Tanzania bloggers yafana Serena hotel!

Mwenyekiti wa Mtandao wa mabloga Tanzania Bw Joachim Mushi (The habari blog) akisisitiza jambo wakati akiwakaribisha wageni waalikwa na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi katibu mtendaji wa MCT Bw Kajubi Mukajanga na Blogger Othman Maulid(Zanzibar leo) 
Kutoka kushoto Mkala Fundikira(keronyingi blog), Jennifer Zighilla(Chingaone blog) na Joshua Fanuel 
Mgalula Fundikira, Peter Moe na Mkala Fundikira 
Mrs Issa Michuzi, Shamim na mdau
Kutoka kushoto Rahel Pallangyo, Chingaone, Malunde na Monica Joseph Monfinance
Malunde1, Mgalula Fundikira, Faraji Swai na Mdau
Mgalula Fundikira, Henry Mdimu (Balozi IMETOSHA MOVEMENT) Mkala Fundikira na Rahel Pallangyo
Malunde1 akisalimiana na Mgeni rasmi Bw Mukajanga.


Mdau, Malunde na Jo Mwaisango(Mbeya yetu)


Msanii Jhikoman alikuwepo pia

Wakala wa Mdhamini Vodacom, NMB na Raha
William Malecela( Blog ya wananchi)
Afisa uhusiano wa Vodacom Bw Kevin Twissa akihutubia hafla hiyo

Toka kushoto ni Mgeni rasmi Bw Kajubi D Mukajanga, Joachim Mushi, Issa Michuzi, Othman Maulid, Josh Fanuel na Henry Mdimu.
Chingaone,Josh Fanuel na Father Kidevu
Mwakilishi kutoka USA embnassy ya Tanzania
Msanii Jhikoman akitumbuiza na wimbo wa Ushirkina na John Kitime (Cheka na Kitime blog)
Jhikoman akipiga gitaa
Mkala Fundikira, Woinde Shizza na Faraji Swai
Mgeni rasmi akikata Ndafu
Mkala na Rose Ndauka(Bongo movie star)
Freddy, Khadija Kalili(Bongo weekend) na Mkala
Rose Ndauka, Mkala na mwenyekiti Mushi
Mabloga wafanya dhihaka miongoni mwao

Mdau na Rose Ndauka
Adela kavishe (dallykavisheblog)
Mdau na Chingaone
Zainul Mzige(Mo Blog) na Woinde Shizza.
Picha zote kwa hisani ya mkalamatukio blog

Shabiki wa Chelsea mpigania haki za binadamu atuhumiwa kwa ubaguzi Paris!


Bw Richard Barklie akihutubia kongamano la haki za binadamu nchini India
Imebainika kuwa askari polisi wa zamani na mpigania haki za binadamu Bw Richard Barklie ni mmoja kati ya mashabiki watatu wa Chelsea waliomzuia mtu mweusi Suleyman Syla kupanda treni kwa kuwa ni mweusi. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea baada ya mchezo wa ubingwa wa ulaya (UEFA Champions league) kati ya Paris Saint Germain(PSG) na Chelsea uliochezwa jijini Paris Ufaransa jumanne iliyopita. Bwana Barklie alibainika baada ya Metropolitan Police ya Uingereza kuonesha picha za washukiwa wa tukio hilo zilizokamatwa na kamera za cctv za stesheni hiyo ya treni za ardhini maarufu kama METRO.

Bw Barklie ambaye pia ni mkurugenzi katika taasisi ya hiari mjini Belfast Northen Ireland ya WAVE TRAUMA CENTRE ameshasimamishwa kazi na taasisi hiyo kupisha upelelezi.

Barklie ambaye ni mmiliki wa tiketi ya msimu ya Chelsea fc akiwa na wenziwe watatu walimsukuma Bw Syla asiingie ndani ya treni (METRO) huku wakiimba (we are racists we are racists this is how we ike it) Sisis ni wabaguzi na hivi ndivyo tupendavyo. Police nchini England imeshawatambua watuhumiwa lakini hakuna aliyekamatwa mpaka sasa, Idara hiyo ya polisi imeeleza upelelezi utaingia hatua inayofuata.

Hata hivyo kupitia mwanasheria wake Bw Barklie amakanusha kuhusika na vitendo vya kibaguzi vilivyotokea siku hiyo lakini anakiri kuwepo eneo la tukio, na amedhamiria kujisafisha.

Metropolitan police pia imeeleza haiwezi kukamata mtu kwa makosa aliyoyafanya nje ya Uingereza, kwa mawazo yangu basi bila shaka Polisi ya Paris itabidi iiombe serikali ya England washukiwa wapelekwe Ufaransa kwa mahojiano na pengine kushtakiwa iwapo itaonekana wana kesi ya kujibu.

Kilabu cha Chelsea kupitia meneja wa timu Jose Mourinho kimeelzwa kusikitishwa na tukio hilo na kuwa kitawafungia wote watakapatikana na kesi ya kujibu. Taarifa ya msemaji wa kilabu hicho cha jijini London ameelza kuwa mmiliki wa timu hiyo Bw Roman Abramovich ametiwa kinyaa na kitendo hicho. Pia kilabu hicho kimeshamkaribisha Bw Syla London katika mchezo wa marudiano kati ya timu hizo mbili.
Picha ya Bw Barklie iliyochukuliwa toka cctv.
Hotuba India
Barklie akiwa katika harakati za haki za binadamu barani Afrika.
Bw Suleyman Syla ndiye mhanga wa tukio la kibaguzi lililotokea stesheni ya treni za chini ya ardhi (METRO) jijini Paris Ufaransa.
Picha na habari kwa hisani ya mailonline/AFP/Metropolitan police

Msanii Moses Bushagama aka Mez B afariki dunia leo!

Mez B enzi za uhai wake!
Msanii Moses Bushagama aka Mez B aliyewahi kung’ara na ngoma ya kikuku cha mama Roda ambayo mimi Mkala Fundikira nilimfanyia video yake katika miaka ya 2000 katika studio za Royal Productions, pamoja na nyimbo zingine nyingi amefariki dunia leo mjini Dodoma ambako mama yake huishi baada ya kuugua kifua kikuu(TB). Binafsi nimeshtushwa na kifo chake hasa baada ya kupata habari za kifo chake bila kufahamu kama alikuwa akiugua kwa muda.Mez alikuwa na kipaji cha aina yake na sauti laini, tutamkumbuika daima.
                           Mungu ilaze pema roho yake!
Picha kwa hisani ya Dj Choka

Simba yashindwa kuunguruma Tanga!


Timu ya Simba leo jioni ilishindwa kuunguruma dhidi ya Coastal union ya jijini Tanga kkatika mchezo uliopooza hivyo kuendelea kusuasua katika ligi ya msimu huo. Pamoja na kuleta mashabiki wengi toka jijini Dar timu hiyo ya Msimbazi haikucheza vizuri sana.



Homa ya mchezo kati ya Coastal union na Simba sports club yapamba moto!

Wakazi wa jiji la Tanga, viunga vya vyake na mikoa ya jirani leo hii watapata burudani inayotarajiwa kuwa ya kupendeza leo hii jioni mnamo saa 10.15 za jioni wakati Wekundu wa Msimbazi Simba SC itakapoingia katika stadia ya Mkwakwani kucheza mchezo wa Vodacom Premier league 2014/15 dhidi ya Coastal union ya jijini hapa kuwania pointi 3  muhimu hasa kwa Simba ambayo imekua ikifanya vibaya msimu huu na kupelekea hofu kwa washabiki wake kuwa uenda ikateremka daraja. Mpambano huo bila shaka utaoneshwa LIVE na kituo cha Televisheni cha AZAM ambacho mitambo yake imeonekana mje ya uwanja wa Mkwakwani, kama ionekanavyo hapo chini.
OB Van ya Azam Tv ikiwa tayai kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Mkwakwani stadium.
Sare za Simba SC zikiwa zimeanikwa kwa mauzo nje ya uwanja wa Mkwakwani
Mshabiki wa Simba kushoto akijadili bei ya fulana ya timu hiyo ya jijini Dar es Salaam karibu na uwanja wa Mkwakwani.
Picha na habari keronyingi blog