07/15/15

Bandora Mirambo alipochukua fomu ya ubunge wa Tabora mjini mapema leo.



Bandora Salum Mirambo akionesha fomu yake ya ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi
Mama Hidaya Rashid Amani katibu msaidizi wilaya akimuandikia risiti Bw Bandora.
Bandora Mirambo akitia sahihi katika kitabu cha kuchukulia fomu ya ubunge wa Tabora mjini.

Ada ya fomu!
Maelekezo!
Saidi Zaidi kulia na Juma Mgawe wakifuatilia kwa makaini makabidhiano ya fomu.

Mama Hidaya Rashid Amani akitoa maelekezo ya ujazaji fomu
Bandora akisalimiana na mdau nje ya ofisi za CCM Wilaya.
Apolo (kushoto) akiwa na Bandora Mirambo mara baada ya Bandora kuchukua fomu.
Bandora akipongezwa na kada wa chama baada ya kuchukua fomu ya ubunge kwa jimbo la Tabora mjini.
Bandora Mirambo akiwa na baadhi ya wapiga kura wa jimbo hilo waliomsindikiza kuchukua fomu katika ofisi za CCM  wilaya ya Tabora mjini.

Binti wa Michuzi Ajitoa Kimasomaso; Achukua Form ya Ubunge wa Viti Maalum

 
 Zahara Michuzi alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.

Zahara Michuzi ni binti wa Issa Michuzi blogger na mpiga picha hodari wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamalizia muda wake sasa.

Binti wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikua wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
 Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa fomu hizo.
 Binti huyo wa Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora
 Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.
 Zahara (kushoto) akilipia fedha halali ya form hiyo huku mama yake mlezi (katikati) akishuhudia kitendo hicho.
 Zahara sasa akianza safari yake ya kuufukuzia ubunge wa viti maalum huku akiipitia fomu
Mwasham (kushoto) akitoa baadhi ya ufafanuzi kwa baadhi ya vipengele vilivyomo katika form hiyo.
Picha zote na aloyson.com TBN

VYUO VYATAKIWA KUTOA ELIMU KULINGANA NA MAHITAJI YA AJIRA HAPA NCHINI



Na Woinde Shizza,Arusha
VIJANA wengi  wanaohitimu vyuo hawapati kazi mara tu ya kuhitimu

masomo yao kutokana na kutokuwepo kwa vyanzo vya ajira vinavyokwenda
sambamba na ongezeko la wahitimu na kuchangia kuwepo kwa wimbi la
wahitimu wasiokuwa na ajira nchini.



Hayo yalisemwa    na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na
utalii ,Selestini Gesimba alipokuwa akizungumza katika mahafali ya
tano ya Chuo cha Taifa cha Utalii(NCT) ,kampasi ya Arusha ambapo jumla
la wanafunzi 55  walihitimu fani za mapishi, uokaji,mapokezi,na huduma
ya vyakula na vinywaji katika ngazi ya cheti.



Alivitaka vyuo mbalimbali kutoa elimu kulingana na mahitaji ya ajira
ili kuwezesha wanafunzi wanaohitimu kupata ajira  kwa haraka na
hatimaye kuondokana na changamoto ya wimbi kubwa la wanafunzi
wanaohitimu na kukaa mtaani bila ajira.



Gesimba alitoa rai kwa vijana wa kitanzania kujiunga na Chuo cha Taifa
cha Utalii ili wapate ujuzi ambao utatoa fursa ya kufanya kazi kwenye
sekta ya utalii na pia fursa ya kuweza kujiajiri wenyewe.



‘sekta ya utalii nchini ni ya muhimu sana na inapaswa kudhaminiwa
kwani imekuwa ikichangia asilimia 17.5 kwenye pato la Taifa na
kuifanya kuwa ya kwanza kwa kuingizia Taifa Dola bilioni mbili
ikifuatiwa na sekta ya madini ambayo imeliingizia Taifa Dola bilioni
1.7 mwaka 2004 .’alisema Gesimba.



Alisema kuwa, sekta hiyo ni miongoni mwa sekta inayokuwa kwa kasi
kubwa duniani ambapo imekuwa ikikua kwa  asilimia 4.5 hadi 5 kwa mwaka
ambapo imekuwa chachu ya kukuza na kuendeleza sekta nyingine za
kiuchumi kama kilimo, miundombinu , mawasiliano na usafiri pamoja na
kuwa kichochea kikubwa cha kupunguza umaskini katika jamii.



Naye Mtendaji Mkuu wa wakala wa chuo cha Taifa cha Utalii ,Rosada
Msoma alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutoa mafunzo na
kuwaunganisha wanafunzi wake na fursa mbalimbali za ajira ambapo kwa
mwaka huu kati ya wanafunzi hao 55 tayari wanafunzi 21 wameshapata
ajira huku wengine wakiendelea kuitwa kwenye usahili maeneo
mbalimbali.



Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake,Neema Mollel alisema
kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu
wa jenereta pindi umeme unapokatika chuoni hapo, ukosefu wa hostel
changamoto inayosababisha wanafunzi wanaosoma mbali kutoweza
kuhudhuria kozi mbalimbali chuoni hapo.



Aidha waliomba chuo hicho kuwezeshwa zaidi na kuweza kutoa kozi
mbalimbali kwa ngazi ya diploma ili kuwawezesha wanafunzi wake kupata
elimu ya juu zaidi ambapo itawawezesha kukabiliana na changamoto ya
ajira ndani na nje ya nchi.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ,Adoh  Mapunda alisema kuwa,serikali
mkoani Arusha wapo tayari kushirikiana na chuo hicho katika kuboresha
huduma mbalimbali za masomo ili kuwezesha chuo hicho kukua zaidi na
kuendelea kutoa elimu iliyo bora zaidi.



Mapunda alikitaka chuo hicho kuboresha zaidi maswala ya hoteli ili
kuwavutia wateja wengi zaidi kuweza kujiunga chuoni hapo kutokana na
elimu nzuri ,na kuwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa
kukitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi kwa ujumla.

Bandora uso kwa uso na Mh Aden Rageh ubunge Tabora mjini!

Bandora Salum Mirambo akiwasilia katika ofisi za CCM wilaya ya Tabora kuchukua fomu za ubunge wa Tabora mjini
Wagombea ubunge wa jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh Aden Rageh na Bandora Mirambo leo 
hii walikutana uso kwa uso walipofika ofisi za CCM wilaya kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge wa wa Tabora mjini. Wote wawili katika kuonesha siasa si chuki wala ugomvi walilakiana na kusalimiana kwa uzuri kabisa.


Wawania kuteuliwa na CCM wakisabahiana
 Mh Aden Rageh ndiye mbunge aliyemaliza muda wa ubunge wa Tabora mijni ambapo alishinda ubunge huo mwaka 2010 kwa kumuangusha  kwenye kura za maoni ndani ya CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2005 marehemu Siraju Kaboyonga ambaye naye alimshinda Henry Mgombelo mwaka 2005 aliyekuwa mbunge mwaka 2000 . Hali hii imeonesha kuwa wapiga kura wa Tabora wamekuwa na tabia ya kutorudisha mbunge katika kiti hicho kwa mara ya pili mfululizo, Mh Rageh ambaye alipata kuwa mwenyekiti kilabu cha Simba cha jijini Dar bila shaka atakuwa na kibarua kigumu cha kuuvunja mwiko huo.

Bandora Mirambo ni mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Salu Security yenye makao yake makuu mjini Sinyanga na matawi kadhaa mikoa ya kanda ya ziwa.

Tabasamu kubwa!