Bi.Deograsia Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na Habari, Chuo Kikuu Dodoma UDOM, hii leo akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa shule ya Sekondari Mara. Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini.
#BMGHabari
Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye, hi leo akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa shule ya Sekondari Mara.
Wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara wakifuatilia mada kutoka kwa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo (kushoto), akizungumza wakati wa mafunzo hayo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo jana. Baada ya ufunguzi alishiriki na wadau wengine mafunzo hayo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akizungumza kwenye mafunzo kwa wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara, hii leo. Kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye, Bi.Deograsia Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na Habari, Chuo Kikuu Dodoma UDOM na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kuhoto) akiwa pamoja na Afisa Utamaduni Halmashauri ya Musoma Vijijini, Twalib Kamugisha (kulia) wakifuatilia mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara.
Afisa Utamaduni Halmashauri ya Musoma Vijijini, Twalib Kamugisha (kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara TDFAA, Johnson Ibambai maarufu kama Dunia (kulia), wakifuatilia mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara
Wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, wakiwa kwenye mafunzo ya filamu yanayotolewa na Bodi ya Filamu mkoani humo.
Bodi ya Filamu nchini imewataka wadau wa sekta hiyo kuwasilisha miswada ya kazi zao ili kukaguliwa kabla ya kuanza kuigiza ili kuondoa na usumbufu wa kuzifungia kazi zisizo na maadili.
Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fissoo, ametoa kauli hiyo kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia ya filamu mkoani Mara, yanayofanyika Mjini Musoma.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa usumbufu wa ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya miswada ya filamu kurekodiwa kabla ya kukaguliwa na baadaye filamu zake kuzuiliwa wakati wa kuingia sokoni hivyo kuibua usumbufu mkubwa.
Wakiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo, Dkt.Herbert Makoye kutoka Taasisi ya Sanaa Bagamoyo pamoja na Deograsia Ndunguru kutoka Chuo Kikuu Dodoma, wamewahimiza wanatasnia wa filamu kuzingatia weledi katika uandaaji wa kazi zao kwa kuzingatia maudhui bora pamoja na maandalizi yanayokidhi uhitaji.
Washiriki wa mafunzo hayo wameelezea umuhimu wake ambapo wamesema yatawasaidia kuboresha uzalishaji wa kazi zao ikiwemo kuzingatia maudhui bora tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Bonyeza HAPA kujua zaidi