05/05/15

Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .
Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.
Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.

Bilionea Dangote bado anataka kuinunua Arsenal!

Uwanja wa the Emirate London ya kaskazini
Bilionea mNigeria mfanyabiashara wa saruji Bw Aliko Dangote ameeleza nia yake ya kuinunua klabu ya Arsenal ya England. Dangote ambaye ndiye mtu tajiri kuliko wote katika bara la Afrika ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani bilioni 15 aliuambia mtandao wa bloomberg kuwa "Naweza kuinunua Arsenal lakini si kwa bei ya kiwazimu ila kwa bei ambayo wamiliki watashawishika kuniuzia"

Dangote ambaye ana pesa nyingi kuliko mmiliki wa sasa wa Arsenal Stan Kroenker mwenye 67% ya hisa na mwanahisa mwingine Mrusi Alisher Usmanov.
Aliko Dangote(58) bilionea m Nigeria, mwenye mapenzi na Arsenal Football club ya jijini London, England.

Lakini Dangote alibainisha kuwa mpango wa kununua kilabu hicho maarufu kama the gunners haupo hivi karibuni, alisema "Tunawekeza kiasi cha dola bilioni 16 katika miradi tofauti miaka michache ijayo, kwani nataka kupeleka biashara zangu katika kiwango fulani, na nikimaliza hilo ndipo ofa ya kuinunua Arsenal itafuata" Pia Dangote amepata kukaririwa akisema kocha Arsene Wenger anatakiwa kubadili mfumo wa timu yake. Arsenal imekuwa na sifa ya kutandaza soka safi na la kuvutia lakini wameshindwa kushinda ubingwa wa England kwa karibu miaka 11 na kabla ya mwaka jana ambapo walishinda kombe la FA walikuwa hawajashinda kikombe chochote kwa miaka 9.

Mwanahisa mkuu wa Kilabu hicho Bw Stan Kroenker amenunua hisa zaidi hivi karibuni na haielekei ana mpango wa kukiuza kilabu hicho katika miaka ya karibuni.

Dangote pia anajenga kiwanda cha saruji mjini Mtwara ambapo wakazi wengi wa mkoa huo watapata ajira za muda na za kudumu.
Stan Kroenker (67) bilionea Mmarekani ndiye mbia mwenye hisa kubwa katika kilabu cha Arsenal kwa sasa
Kocha Wenger amatakiwa kubadili mfumo wa timu yake na Dangote
source Mirroronline