Pichani ni Mhudumu wa Mapango ya Chinhoyi Cephas Sithole akitoa maelezo kwa timu ya waandishi wa habari waliombatana na wadau wa utalii kutoka nchini Afrika Kusini kwenye ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii nchini Zimbabwe katika mapango Chinhoyi.(Picha zote na Zainul Mzige).
Waandishi wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African), Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige (modewjiblog), Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Safari ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga wenye gharama nafuu Fastjet Tanzania ikiwa ni moja ya mipango yao ya kuimarisha safari zake za kutoka Dar es Salaam-Lusaka na Harare.
Safari hiyo ilikuwa maalum kwa ajili kuhudhuria maonyesho ya naneya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) ambayo yameanza kurindima jijini Harare katika ukumbi wa Harare International Conference Centre (HICC).
Mungoza watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini Zimbabwe, Aleck Makumire akitoa maelezo wa timu ya waandishi wa habari kabla ya kushuka kwenye mapango hayo wakati wa ziara maalum ya kutembelea vivutio vya Utalii nchini humo.
Mungoza watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini Zimbabwe, Aleck Makumire akiwa ndani ya mapango ya Chinhoyi akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Tanzania katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini humo.
Waandishi wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
Wakirejea kutoka kwenye mapango hayo ambayo chini yana maji ambayo hayatembei wala kukauka. (pichani kwa chini yakionekana kuwa na rangi ya bluu lakini ukichota ni meupe).
Mwandishi wa habari Timothy Kitundu (East Africa Business Week) akitoka kudhuru mapango hayo wakati wa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.
Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA) akifurahia ukodak wa kamre ya modewjiblog akitokea ndani ya mapango ya Chinhoyi. Kulia ni Mwambata wa Waziri wa Utalii anayehusika na masuala ya uhamiaji kwa Afrika nchini Zimbabwe, Sherry Sibanda.
Picha ya pamoja na wenyeji wetu.
Ziara ya waandishi kutembelea kanisa la Mtakatifu Barbara.
This delightful little round church situated above Kariba town on the hill known as Kariba Heights, was built by workers and engineers employed by Impresit, the Italian company contracted to build the Kariba dam wall. The church is dedicated to St Barbara, who is the patron saint of engineers/construction workers.
On the outside walls of the church is a dedication in Latin to the memory of the construction workers killed during the building of Kariba Dam and a plaque with the names of those who lost their lives is found inside. The church has beautiful stained glass windows and an open-air design which is perfectly suited to the hot climate of Kariba. A bell tower at the back of the church still contains the original bell constructed by hand by Italian workers at the time and hoisted into place with a crane.
Read the detailed story about the church bell of Santa Barbara at this link: The Bell of Santa Barbara Church: A Modern Legend in the Making
Picha ya kumbukumbu nje ya kanisa hilo.
Kulia ni Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige akiwa ameambatana na waandishi wenzake kwenye ziara hiyo.
Sehemu ya muonekano wa Ziwa Kariba kwa juu zinapopaki boti za utalii za watu binafsi na makampuni.
Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu, Mariam Said na Justin Damian wakipata ukodak wakati wa ziara hiyo ya Kariba.
Muonekano wa Ziwa Kariba.
Muonekano wa ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige akitazama ukingo wa ukuta huo wakati wa ziara ya Kariba nchini Zimbabwe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Going Places Tours & Travel ya Zambia, Rachel Ward akipozi na Mwambata wa Waziri wa Utalii anayehusika na masuala ya uhamiaji kwa Afrika nchini Zimbabwe, Sherry Sibanda kwenye meli kubwa ya kitalii inayotumika kutembeza watalii ambayo inalaza zaidi ya watu 50 huku ikiwa na sehemu ya ukumbi wa burudani na wakati mwingine hukodiwa kama ukumbi wa harusi ndani ya maji pamoja na baadhi ya vyumba maalum kwa wanandoa wanaoenda mapumzikoni (Honey moon).
Sherry Sibanda na Captain wa muda Zainul Mzige wakipata ukodak ndani ya meli hiyo.
Captain wa muda Frank Aman akipozi kwa ukodak.
Captain wa muda Timothy Kitundu ndani ya meli.
Muonekano wa Meli hiyo.
Usalama Kwanza: Mariam Said (Daily News) akivaa boya kabla ya kuanza safari ya kuzunguka ziwa Kariba na kulia ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava akisaidiwa kuvaa boya na Nahodha ya boti hiyo.
Kutoka kushoto ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava, Cherry Sibanda na Mariam Said wakiwa wamepumzika huku wakipitia baadhi ya vipeperusha vya boti za kitalii zinazokodishwa kwa ajili ya kupumzika katika ziwa la Kariba.
Kundi jingine likiwa kwenye ziara ya ziwa Kariba likiongozwa na Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA).
Kituo cha mafuta katika Bandari ya Marine Land kikiwa ndani ya Ziwa Kariba.
Boti ya Matusadona inayokodishwa kwa watalii ambapo kila kichwa ni $5000 kwa usiku mmoja ambayo ina uwezo wa kubeba watu saba pamoja na mpishi maalumu kwa ajili ya kuwapikia chakula.
Viboko ndani ya Ziwa Kariba.
Wanahabri wakirejea baada ya ziara ya kuzunguka Ziwa Kariba.
Timu ya waandishi wa habari kutoka Tanzania wakipiga picha katika shamba la Mamba la Padenga ambalo ni shamba kubwa la ufugaji wa Mamba kuliko yote kusini mwa Afrika.
Baadhi ya Mamba wakiwa mapumziko ndani ya shamba hilo.
Mmoja wa Mamba akiwa ametega Nzi wajae ndani ya mdomo wake.
Na Modewjiblog team, Harare