Moyes akiwa na Shinji Kagawa ziarani Japan kiangazi hiki. |
Kagawa: Anafikiri anapaswa kuwemo katika kikosi cha kwanza Man united ingawa alichelewa kuripoti mazoezini. |
Kwa maoni yangu David Moyes anatakiwa amkumbushe Kagawa kuwa Man united ni kilabu kilichopata mafanikio makubwa huku kikiwa na usiri mkubwa ndani ya kilabu hicho, na sijapata kumsikia mchezaji akilalamika katika vyombo vya habari juu yakutopangwa na Sir Alex Ferguson kwa kuwa hakuruhusu mchezaji yeyote kuongea na vyombo vya habari hasa kwa habari hasi kama hiyo. Sir Alex amepata kusema mara nyingi kuwa meneja ni lazima awe ndio mhimili wa kila kitu katika klabu na meneja asiruhusu mchezaji kujiona mkubwa kuliko kikosi kizima, ndio maana nasema Moyes amkumbushe Kagawa jukumu lake.