Msanii machachari wa muziki wa kizazi kipya Bob Junior aka Sharobaro aka Rais wa wasafi hatimaye kwa mara ya kwanza atafanya onesho la kukata na shoka mjini Tabora katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Haj litakalofanyika Jumanne ya tarehe 15/10/2013. Akithibitisha hilo mratibu wa onesho hilo kubwa Mkala Fundikira ambalo litawaleta pia wasanii wa vichekesho Masele cha pombe na Masai nyota mbofu wa kipindi cha ucheshi cha Vituko show alisema kila kitu kipo tayari kwa sasa yeye na jopo la waandaaji wenzie wanamalizia vitu vidogo vidogo tu na kuisubiria siku ya onesho. Pia Mkala alisema kuna msanii mwingine wa Bongo Flava ataungana na hao ambao amewataja kuja Tabora kumwaga burudani atamtaja siku zijazo.