04/22/15

RAIS MSTAAFU MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI AWASILI JIJINI WASHINGTON DC.


 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiambata na mama Sitti Mwinyi wawasili jijini Washington DC tayari kwa tamasha maalum la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa utawala Lilly Munanka wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, mara alipowasili hotelini.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi Edward Taji.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme.
  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Emmanuel Swere.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi John Anbiah
     Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiwa ameongozana na mama Sitti   Mwinyi na baadhi ya msafara wake katika hoteli waliyofikia.
                                  PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI
Click here to Reply or Forward 1.43 GB (9%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 12 hours ago Details

BALOZI MPYA WA ANGOLA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.


 Mhe, balozi wa Angola Agostinho Tavares akipokelewa na afisa wa ubalozi  Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi .
 Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwa na furaha baada ya mgeni wake kufika ofisini .
 Mhe balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Angola Agostinho Tavares.
 Mhe Balozi wa Angola nchini Marekani Agostinho Tavares akiweka sahihi  kitabu cha wageni.
 Mhe balozi wa Angola chini Marekani Agostinho Tavares akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha .
Mhe balozi Libarata Mulamula na balozi wa Angola nchini marekani Agostinho Tavares pamoja na afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme walipokua wakibadilishana mawazo. 

Picha kwa hisani ya camera ya ubalozi

             

Ujumbe wa Imetosha ukiwa Metro Fm 99.4 Mwanza!


Kutoka kushoto ni Juma Herman (meneja wa Green Palm Hotel), Issaya Mwakilasa aka Wakuvwanga, Jhikolabwino Manyika, Kelvina John, Mwenyekiti Masoud Kipanya na Tonny Alphonce(Mtangazaji Metro fm 99.4

Siku ya Ijumaa ya tarehe 17/04/2015 ujumbe wa Imetosha Foundation ukiongozwa na Mwenyekiti Masoud Kipanya ulifanya mahojiano katika kituo cha redio cha Metro Fm 99.4 kwenye kipindi cha Pambazuko la Metro fm 99.4 ikiwa ni katika mfululizo wa kujitambulisha kanda ya ziwa kwa taasisi hiyo inayopinga mauaji kwa watu wenye ualbino kwa njia ya elimu. Msanii wa vichekesho (comedian) Wakuvwanga ambaye ni mjumbe wa taasisi hiyo alitoa kali alipoulizwa angependekeza adhabu gani kwa watakaopatikana na hatia ya kuua watu wenye ualbino? akajibu "Kwa kuwa hawa si watu bali ni wanyama kutokana na vitendo vyao viovu basi napendekeza serikali iwapeleke Mikumi national park iwafungie ndani ya senyenge ili watalii wawe wanaenda kuwaona kama wanavyoenda kuwaona Simba na wanyama wengine! Kipindi hicho maridhawa kiliendeshwa na watangazaji Tonny Alphonce na Katumba Madua
Mtangazaji wa kipindi cha Pambazuko la Metro Fm, Tonny Alphonce akimuuliza swali Masoud Kipanya.
Masoud Kipanya akijibu swali toka kwa mtangazaji wa Metro Fm 99.4zaji Tonny Alphonce.
Tonny akimpiga swali Wakuvwanga, anayesikiliza kwa umakini wa hali ya juu, soma uone jibu lake!
Kutoka kushoto ni Katumba Madua, Wakuvwanga na  msanii wa muziki wa Reggae Jhikoman

Moja ya studio za Metro Fm 99.4 ambazo wanazo tatu katika jengo hilo lililopo kati kati ya jiji la Mwanza
Picha ya Pamoja ndani ya Metro fm 99.4 toka kushoto ni Juma Herman, Mkala Fundikira, Kelvina John, George Binagi, Tonny Alphonce, Rosier, Sophia George, Wakuvwanga Masoud na Katumba Madua
Jhikoman kushoto, Rosier(receiptionist) na Masoud
Masoud akibadilishana mawazo na Sophia George wa Metro fm 99.4 ya Mwanza wiki iliyopita ujumbe wa Imetosha Foundation ulipotembelea studio za kituo hicho cha redio

Mtandao huu unaomba radhi kwa kuchelewa kurusha habari hii kwa wakati muafaka kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Ahsante!