Mheshimiwa Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!

Mheshimiwa Sitta ajiweka mbali na lawama za wivu wa uwaziri mkuu!

Mh Samuel Sitta akitangaza nia leo mchana Itetemia Tabora
Mheshimiwa Samuel Sitta leo hii alitangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitangaza nia yake hiyo mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.

Akieleza sababu tano zilizomfanya atangaze nia yake ambazo ni 

Mabango nayo yalikuwepo!

Mh Sitta akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora leo mchana.
Mh Magreth Sitta akisalimia wananchi wa Itetemia

1.Muungano
Toka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.

2. Mchakato wa katiba
Pamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.



Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba.
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini
Binafsi naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.

3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda
Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza  huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira  chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.




4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa
Rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.

5. Kuimarisha CCM kiuchumi
Chama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake  kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni "wafadhili" 


Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui



Agness Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia leo




Aidha Mh Sitta akijibu swali toka kwa mwandishi wa habari aliyeuliza "Mh Sitta unasemaje juu ya shutuma za waziri mkuu aliyejiuzuru wadhfa wake kuwa wewe na Mh Mwakyembe mlikuwa na wivu naye ndio maana mkamuonea mpaka ikabidi ajiuzuru? Mh Sitta akajibu "Bwana mwandishi kwa nini swali hilo humuulizi yeye mwenyewe aseme ni kipi alichoonewa? Mchakato wa uchunguzi ulifanyika mwaka 2008 mpaka sasa ni miaka 7 hivi sasa muda wote huu alikuwa wapi hata leo aseme alionewa? Jibu ambalo lilipelekea vicheko na vigerere toka kwa wananchi walioudhuria hafla hiyo.