Moja ya kikundi cha ngoma za kimila cha Waswezi wakimsikiliza Mh Samuel Sitta. |
Mh Samuel John Sitta ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa Mtemi wa himaya ya Unyanyembe Mtemi Said (Swetu) Fundikira aliyetawala kuanzia mwaka 1917 mpaka mwaka 1927 ni mwanasiasa mkongwe kwa siasa za Tanzania jana akijibu swali la mwandishi wa habari toka CG Fm 89.5 ambaye aliuliza "kwa kuwa tayari wana Ccm, 8 washatangaza nia ya kutaka kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nini wewe usingeamua kujiunga na mmoja wao ili kumuongezea nguvu, badala ya na wewe kutangaza nia? Mh Sitta akajibu "Kila mtu anajipima yeye mwenyewe uwezo wake kisha anaamua cha kufanya, vile vile urais ni huru na ni haki kwa mtu yeyote kugombea. Mdogo wangu Kigwangwala na yeye ana mpango wa kugombea, ni jambo zuri. Aidha Mh Sitta akaongeza kusema "lakini hata wewe ndugu mwandishi ungeweza kugombea, nashangaa sijui kwa nini hugombei" Jibu hili liliwafanya watu wengi waliohudhuria hapo Itetemia jana kuangusha vicheko.
Kikundi cha kina mama wakicheza na kuimba |
Mheshimiwa Sitta akisalimiana na baadhi ya watu waliofika Itetemia jana |
Mzee Ifuma Abdallah akimsindikiza Bibi Kagori Said Fundikira (Mama mzazi wa Mh Samuel Sitta) na kulia ni Agnes Kijoh Sitta(binti ya Mh Sitta) |
Kushoto ni Kefa Kijoh na Agnes Kijoh Sitta wakisalimia wageni |
Habari na picha Mkala Fundikira wa TBN CENTRAL ZONE