11/26/15

Benki ya Amana yazindua wiki ya huduma kwa wateja baada ya kutimiza miaka minne!


Mteja wa muda mrefu wa bemki ya Amana Bw Masoud Khalfan ambaye akizindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Main la benki ya Amana jijini Dar ka kukata utepe. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud, Kulia ni mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mohamed Mussa, kushoto ni mteja wa siku nyingi wa benki hiyo Bw Dossa.
Mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mussa kushoto akiwa na mkuu wa kitengo cha fedha Bw Fahad Hamid siku ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Amana Bank imeadhimisha miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24 Novemba 2011. Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi siku ya jumatatu wote walikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi yetu yote ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.
Meneja wa tawi la Main  Bi Aisha Awadh akimwelekeza kitu mteja wa benki mama Sangawe.
Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7 Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na za kisasa. Amana Bank mpaka sasa ina matawi saba ambapo manne yapo jijini Dar nayo ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na main ambapo ndipo makao makuu ya benki hiyo ya aina yake nchini.

Mfanyakazi wa benki ya Amana (Kushoto) akiwahudumia wateja kwa viburudisho katika siku ya wiki ya huduma kwa wateja wiki hii.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidiTunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu  huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.
Mtoa huduma kwa wateja Bi Zainab wa tawi la Mwanza akimhudumia kwa viburudisho mteja wa benki hiyo.

Mteja huyu akijipatia huduma katika tawi la Mwanza
Huduma kwa wateja.
Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya 27/11/2015, kwa hafla ya  kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank ambapo mkurugenzi wa benki hiyo  Dk Muhsin Masoud atakuwa katika tawi la jijini Mwanza mjini kukutana na wateja na kupokea maoni na ushauri wa kila aina utakaotolewa na wateja wao.
Baadhi ya wateja wakijipatia huduma katika benki ya Amana tawi la jijni Arusha.

Huduma kwa wateja zikiendelea jijini Arusha.