06/07/14

Leo ndio leo Malkia wa Miss Dar Indian Ocean kupatikana leo!

 Warembo wa Miss Dar Indian Ocean jana walitembelea Club Billicanas kujinadi kwa mara ya mwisho ambapo leo watachuana vikali kuwania taji la Miss Dar Indian Ocean. Shindano hilo litafanyika leo usiku kuanzia saa 2 katika viwanja vya Nyumbani lounge ambapo viingilio kwa viti vya kawaida ni Tsh 10,000/= na zile za VIP zikipatikana kwa Tsh 30,000/=. Shindano hilo limedhaminiwa Konyagi kupitia kinywaji chake cha Zanzi, CXC Africa, Tsn Super market, Redds Original,TBC, Channel 10, Blog ya wananchi, Nyumbani Lounge. Chini ni picha za baadhi ya warembo wa shindano hilo.
Msaidizi wa Matron wa warembo Miss Baby James
Mjumbe wa kamati ya Miss Dar Indian Bw Khalid Mkwabi aka Dudu (Kushoto) akiwakaribisha mashabiki wa urembo katika show ya leo. Kulia ni Miss Baby James