Tia saini mwanangu Tabora wanakusubiria kwa hamu |
Dimpoz (kwa poz) ambaye kwa karibu miezi mitatu amekuwa katika bara la Ulaya akifanya maonesho katika nchi tofauti zikiwemo England, Holland, Norway, Sweden na nyingi nyingine amethibitisha kuwa ataporomosha show kali mjini Tabora mnamo tarehe 31/05/2013 katika kusindikiza kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa shindano la Redds Miss Tabora 2013. Pichani ni picha kadhaa za Ommy Dimpoz akisaini mkataba wa kufanya onesho hilo kubwa huku akishuhudiwa na mlezi wa kamati ya Miss Tabora 2013 Bw Mgalula Fundikira. Hatua hii itakuwa ni kukidhi matamanio ya muda mrefu ya mashabiki wa Ommy Dimpoz Tabora kumshuhudia msanii wao kipenzi kwa ukaribu zaidi siku hiyo ya tarehe 31/05/2013 ambapo shoka litaungua mpini utabaki!
Ommy akianguka sahihi! |
Ahsante sana: Inaelekea ndicho asemacho Mgalula. |