Gari dogo likiwa imeacha barabara baada ya theluji nyingi kudondoka na kupelekea dereva wa gari hilo kupoteza mwelekeo na kutumbukia pembezoni mwa barabara(Free way) |
Wikiendi iliyopita ilikuwa ni ya heka heka kubwa katika miji iliyo Kaskakazini mashariki mwa nchi ya Marekani ambapo barabara nyingi zilipitka ama kwa taabu au kutopitika kabisa katika majimbo ya Pennsylyvania na New Jersey ambapo pia imeelezwa kulikuwa na uchelewesho katika usafiri wa anga ambapo baadhi ya wasafiri walishindwa kuelekea waendako kwa takribani masaa matano hivi. Hata hivyo hali ilielekea kurudi katika ukawaida wake kuanzia j3 kwa maeneo ya Philadelphia na kwingineko.
Watoto nao walipata muda wa kuchezea snow |
Misururur mikubwa ya magari ilionekana maeneo mengi huko America wikiendi iliyopita |
Hata mitaani pia hapakusamehwa na hali mbaya ya hewa |
Ramani hii ilionesha maeneo yaliyoathirika zaidi. |