Warembo watakaoshiriki shindano la kumtafuta ReddsMiss Tabora 2013 litakalofanyika katika ukumbi wa Frankman Palace mnamo tarehe 31.Mei.2013 wamekuwa wakiendelea na mazoezi makali chini ya mwalimu wao Miss Pili Issa ambaye ni Miss Tabora 2010 katika ukumbi wa Club Royal mjini Tabora. Katika onesho hilo ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Fatma Mwassa kama mgeni rasmi, kiingilio kitakuwa sh elfu 10 kwa viti vya kawaida na sh elfu 20 kwa viti maalum VIP.