Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Shabiki wa Chelsea mpigania haki za binadamu atuhumiwa kwa ubaguzi Paris!
Bw Richard Barklie akihutubia kongamano la haki za binadamu nchini India |
Bw Barklie ambaye pia ni mkurugenzi katika taasisi ya hiari mjini Belfast Northen Ireland ya WAVE TRAUMA CENTRE ameshasimamishwa kazi na taasisi hiyo kupisha upelelezi.
Barklie ambaye ni mmiliki wa tiketi ya msimu ya Chelsea fc akiwa na wenziwe watatu walimsukuma Bw Syla asiingie ndani ya treni (METRO) huku wakiimba (we are racists we are racists this is how we ike it) Sisis ni wabaguzi na hivi ndivyo tupendavyo. Police nchini England imeshawatambua watuhumiwa lakini hakuna aliyekamatwa mpaka sasa, Idara hiyo ya polisi imeeleza upelelezi utaingia hatua inayofuata.
Hata hivyo kupitia mwanasheria wake Bw Barklie amakanusha kuhusika na vitendo vya kibaguzi vilivyotokea siku hiyo lakini anakiri kuwepo eneo la tukio, na amedhamiria kujisafisha.
Metropolitan police pia imeeleza haiwezi kukamata mtu kwa makosa aliyoyafanya nje ya Uingereza, kwa mawazo yangu basi bila shaka Polisi ya Paris itabidi iiombe serikali ya England washukiwa wapelekwe Ufaransa kwa mahojiano na pengine kushtakiwa iwapo itaonekana wana kesi ya kujibu.
Kilabu cha Chelsea kupitia meneja wa timu Jose Mourinho kimeelzwa kusikitishwa na tukio hilo na kuwa kitawafungia wote watakapatikana na kesi ya kujibu. Taarifa ya msemaji wa kilabu hicho cha jijini London ameelza kuwa mmiliki wa timu hiyo Bw Roman Abramovich ametiwa kinyaa na kitendo hicho. Pia kilabu hicho kimeshamkaribisha Bw Syla London katika mchezo wa marudiano kati ya timu hizo mbili.
Picha ya Bw Barklie iliyochukuliwa toka cctv. |
Hotuba India |
Barklie akiwa katika harakati za haki za binadamu barani Afrika. |
Bw Suleyman Syla ndiye mhanga wa tukio la kibaguzi lililotokea stesheni ya treni za chini ya ardhi (METRO) jijini Paris Ufaransa. |
Homa ya mchezo kati ya Coastal union na Simba sports club yapamba moto!
Wakazi wa jiji la Tanga, viunga vya vyake na mikoa ya jirani leo hii watapata burudani inayotarajiwa kuwa ya kupendeza leo hii jioni mnamo saa 10.15 za jioni wakati Wekundu wa Msimbazi Simba SC itakapoingia katika stadia ya Mkwakwani kucheza mchezo wa Vodacom Premier league 2014/15 dhidi ya Coastal union ya jijini hapa kuwania pointi 3 muhimu hasa kwa Simba ambayo imekua ikifanya vibaya msimu huu na kupelekea hofu kwa washabiki wake kuwa uenda ikateremka daraja. Mpambano huo bila shaka utaoneshwa LIVE na kituo cha Televisheni cha AZAM ambacho mitambo yake imeonekana mje ya uwanja wa Mkwakwani, kama ionekanavyo hapo chini.
OB Van ya Azam Tv ikiwa tayai kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Mkwakwani stadium. |
Sare za Simba SC zikiwa zimeanikwa kwa mauzo nje ya uwanja wa Mkwakwani |
Mshabiki wa Simba kushoto akijadili bei ya fulana ya timu hiyo ya jijini Dar es Salaam karibu na uwanja wa Mkwakwani. |
Promota wa Lennox Lewis aamua kuwa mwanamke!
Frank Maloney akishangilia ushindi wa Lenox Lewis |
Frank Maloney(61) promota maarufu wa ndondi wa zamani ambaye amewahi kuwa promota wa bingwa wa zamani wa uzito wa Juu Lennox Lewis ameamua kujibadili kuwa mwanamke na Kujiita Kellie. Kwa kauli yake Maloney alisema "Nimekuwa nikijisikia hivi tangu utotoni mwangu, hatimaye nimechoka kuishi kivulini. Pia alieileza ugumu ulikuwa ni kumfahamisha mkewe anachotaka kufanya, pia ameeleza atafanya operesheni ya badiliko la kijinsia, na kuwa hafanyi hayo ili awe na mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote bali ndivyo alivyokuwa akijisikia awe kwa miaka yote.
Maloney anavyoonekana sasa akiwa kama Kellie. |
Ajuza Kellie akiweka pozi |
Picha na habari kwa hisani ya mailonline na sunday mirror
Shabiki wa Liverpooll auawa kwa kumkejeli shabiki wa Arsenal!
Kwani timu yako ikifungwa goli tano lazima uanguke?
Baada ya timu ya Arsenal (The Gunners) jana kupokea kipigo kikali kilichoendana na maumivu makali cha goli 5-1 toka kwa timu ya Liverpool (Bwawa la maini) aka (Liverfools) kocha Arsene Wenger aliteleza na kuanguka nje ya stesheni ya treni ya LIVERPOOL LIME STREET akiwa anaelekea kupanda treni kuelekea London baada ya mchezo huo wa Barclays Premier league ambapo askari wawili walikimbilia kumuinua kutoka hapao alipoangukia. Wenger alionekana mwenye maumivu makali kufuatia mwereka huo ambapo mashabiki wengi wa Manchester United wamedhihaki wenzao wa Arsenal kuwa mwereka huo ni kiwewe cha kufungwa na Liverpool na hatimaye kupoteza uongozi wa ligi hiyo maarufu duniani.
Ouch!
Maumivu makali!
Pole baba,haya simama!
Picha kwa hisani ya Twitter/TSBible, habari kwa hisani ya mailonlne
Arsene Wenger/Alex Ferguson na David Moyes waenda Xmas shopping pamoja!
Huyu bwana kushoto mwa picha anajiuliza ninaowaona ndio wenyewe ama? |
Je inaweza ikawa kweli, kuwa Arsene Wenger, David Moyes na Sir Alex Ferguson wakaenda shopping pamoja?
Jana waenda shopping ya Christmas nchini Uingereza waliweza kujikuta wakipigana vikumbo na sura maarufu kama Kocha wa zamani wa Man united Sir Alex Ferguson, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na Kocha mpya wa Man united David Moyes lakini kumbe hao wote hawakuwa wao halisi bali ni watu wanaofanana nao tu, ingawa watu kadhaa walistushwa na uwepo wa watatu hao wakifikiri ni wenyewe, pia mamia ya waenda shopping walipiga picha watu hao. Wazo hilo lilitolewa na National Football Museum ambao walitaka kunogesha sherehe za Christmas nchini Uingereza(Uk)
Come on ref what is that? |
Mpiga mbizi shujaa amkaribia Papa!
Wapiga mbizi Vincent Canabal na Daniel Botelho walihatarisha maisha yao ili kumkaribia papa hatari katika pwani ya visiwa vya Bahama huko Marekani katika fukwe za Tiger ambapo Vincent alikuwa akimlisha chakula cha mbwa, papa huyo mwenye urefu wa futi 16 alivutiwa na chakula hicho ndipo akawa mtulivu.
Vincent akimlisha papa chakula cha mbwa. |
Shabiki wa Arsenal apoteza nyumba baada ya Man United kuishinda Gunners!
Hali mbaya |
Robin Van Persie akiwazamisha The Gunners |
Valencia ndiye mchezaji mwenye kasi kuliko wote duniani!
Nyota wa Arsenal Theo Walcot amekuwa akifikiriwa ndiye mcheza soka mwenye kasi kuliko wote duniani, lakini imebainishwa kuwa kiungo wa timu ya Man United Antonio Valencia ametajwa na FIFA kuwa ndiye mcheza soka mwenye kasi kuliko wote ulimwenguni, inasadikika kuwa kiungo huyo anakadiriwa kufikia mwendo kasi wa kilometa 22 kwa saa. Na orodha ya wachezaji na kasi ni kama ifuatavyo hapo chini.
1. Antonio Valencia km 22 (kwa saa) Man united
2. Gareth Bale km 21.56 (kwa saa) Real Madrid
Orodha hiyo pia imeonesha kuwa Aaron Lenon wa Totenham Hotspurs anashika nafasi ya tatu na ya nne imechukuliwa na Christiano Ronaldo huku Lionel Messi akiangukia nafasi ya sita.
Habari na picha kwa hisani ya mtandao wa the express
1. Antonio Valencia km 22 (kwa saa) Man united
2. Gareth Bale km 21.56 (kwa saa) Real Madrid
Orodha hiyo pia imeonesha kuwa Aaron Lenon wa Totenham Hotspurs anashika nafasi ya tatu na ya nne imechukuliwa na Christiano Ronaldo huku Lionel Messi akiangukia nafasi ya sita.
Habari na picha kwa hisani ya mtandao wa the express
Azam yailaza Rhino Fc!
Timu ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam leo hii imeilaza timu ya Rhino Rangers ya mjini Tabora kwa goli 2 kwa sifuri kwa magoli ya Gaudence Mwaikimba kwa shuti kali lililopita kulia mwa lango la kipa wa Rhino Fc mnamo dakika ya 56,baada ya kazi nzuri ya wachezaji wa Azam Fc upande wa kulia mwa uwanja.
Baadhi ya maelfu ya mashabiki wa soka mjini Tabora wakifuatilia kwa makini mchezo kati ya Azam Fc na Rhino Rangers uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi. |
Huku Rhino Rangers ikijaribu kusawazisha bao hilo la Mwaikimba ilijikuta ikongezwa bao la pili kupitia mchezaji wa kiungo Seif Kalihe mnamo dakika ya 77 ya mchezo huo uliodorora. Timu ya Rhino Rangers itabidi ijilaumu kwa kutocheza kwa kujituma kama ambavyo ilicheza katika mchezo dhidi ya Simba ambapo waliweza kuibana Simba na kutoka nayo sare ya goli 2-2. Mchezo ujao wa Rhino utakuwa dhidi ya JKT Oljoro wikiendi ijayo mjini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Patashika langoni mwa Azam |
Basi la wachezaji wa Rhino Rangers likitoka uwanjani baada ya mchezo wao dhidi ya Azam Fc kwisha. |
Totenham wawastaajabisha Real Madrid kwa dau la kumuuza Gareth Bale!
Gazeti la michezo lenye ukaribu na kilabu cha Real Madrid leo hii limedai kuwa Mwenyekiti wa Totenham Hotspurs ya jijini London, Uingereza Bw Daniel Levy amewapa bei ya kumnunua mshambuliaji Gareth Bale kuwa ni Euro145 Milioni au kwa maneno mengine ni Pauni 125 Milioni ya Malkia wa Uingereza. Bei hiyo imewastua sana Madrid kwani hawakutegemea kabisa Bw Levy anaefahamika vema kutoa bei zisizoendana na uhalisia ambapo awali aliwasumbua sana Man United kuwanunua Michael Carrick na Dimitar Bernatov. Bei hiyo pia imelistua sana gazeti la Marca ambalo limetoa kichwa cha habari UNA LOCURA ikiwa na maana Crazy au "wazimu"
Wakati huo huo ripoti toka Spain katika gazeti la Marca zimeeleza kuwa Daniel Levy ameshapokea ofa ya Pauni 85 milioni toka klabu ya PSG ya ufaransa inayomilikiwa na matajiri wa kiarabu. Pia taarifa hiyo ilisema katika ofa zote Muhimu ni ile iliyotolewa na klabu ya Manchester United ya England ingawa chanzo hicho hakikueleza ni kiasi gani Man United wameofa kwa klabu hiyo yenye makazi yake kaskazini mwa jiji la London.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)