Totenham wawastaajabisha Real Madrid kwa dau la kumuuza Gareth Bale!

Totenham wawastaajabisha Real Madrid kwa dau la kumuuza Gareth Bale!

Gazeti la michezo lenye ukaribu na kilabu cha Real Madrid leo hii limedai kuwa Mwenyekiti wa Totenham Hotspurs ya jijini London, Uingereza Bw Daniel Levy amewapa bei ya kumnunua mshambuliaji Gareth Bale kuwa ni Euro145 Milioni au kwa maneno mengine ni Pauni 125 Milioni ya Malkia wa Uingereza. Bei hiyo imewastua sana Madrid kwani hawakutegemea kabisa Bw Levy anaefahamika vema kutoa bei zisizoendana na uhalisia ambapo awali aliwasumbua sana Man United kuwanunua Michael Carrick na Dimitar Bernatov. Bei hiyo pia imelistua sana gazeti la Marca ambalo limetoa kichwa cha habari UNA LOCURA ikiwa na maana Crazy au "wazimu"



Wakati huo huo ripoti toka Spain katika gazeti la Marca zimeeleza kuwa Daniel Levy ameshapokea ofa ya Pauni 85 milioni toka klabu ya PSG ya ufaransa inayomilikiwa na matajiri wa kiarabu. Pia taarifa hiyo ilisema katika ofa zote Muhimu ni ile iliyotolewa na klabu ya Manchester United ya England ingawa chanzo hicho hakikueleza ni kiasi gani Man United wameofa kwa klabu hiyo yenye makazi yake kaskazini mwa jiji la London.