Shabiki mkereketwa wa timu ya Arsenal (the Gunners) Mganda Henry Dhabasani mkazi wa jijini Kampala alijikuta akipoteza nyumba yake dhidi Rashid Yiga ambaye aliweka dau la gari ya Toyota Premio na mkewe baada ya kudai Man united ingeifunga Arsenalbila shaka na wazee wa kijadi walikuwepo na kushuhudia dau hilo likipitishwa kwa maandishi kabla ya mchezo huo amabao mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Robin Van Persie alifunga bao pekee la mchezo katika kipindi cha kwanza na kuwasimamisha The Gunners katika mbio zao za kutaka kujikita zaidi katika usukani wa ligi hiyo maarufu na yenye msisimko kuliko zote duniani. Gazeti la Observer la Uganda lilieleza kuwa shabiki huyo Dhabasani mwenye wake watatu na watoto watano alizirahi baaada ya mchezo kwisha. Hata hivyo aliondoshwa katika nyumba yake siku iliyofuata.