03/05/13

Wazambi kuwakilisha kamati ya Miss Tabora katika semina ya Miss Tanzania




Nassor Wazambi
Mjumbe wa kamati ya Miss Tabora Bw Nassor Wazambi
ameteuliwa kuhudhuria semina ya mawakala wa Miss Tanzania itakayofanyika nje kidogo ya jiji la Dar katika hoteli ya kitalli ya Girraffe Hotel iliyopo kando kando ya bahari ya Hindi.  

Semina hiyo ni ya kawaida kila mwaka kufanywa na kamati ya Miss Tanzania kwa kushirikiana na mdhamini mkuu kampuni ya bia Tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Premium cold. Shindano la Miss Tabora linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei, kamati ya Miss Tabora imeahidi kuwaandalia wakazi wa Tabora onesho kabambe ambalo halijawahi fanyika tangu Miss Tabora ianze.

Semina itafanyikia katika ukumbi huu.

Bwawa la kuogelea lipo kwa wakaazi.