Winga huyo mwenye miaka (27) anasadikika kupokea pauni 50,000 (Tsh milioni 1370) kwa wiki alikamatwa nyumbani kwake na polsi toka Durham katika hekalu lake lenye thamani pauni 1.8m mnamo siku ya jumatatu na baadae kupatiwa dhamana.
Kilabu cha Sunderland kimethibitisha kuwa kimemsimisha Johnson kupisha upelelezi, na hatua hiyo itaanza kazi jumanne ambapo Sunderland itacheza na Hull City katika mfululizo wa ligi kuu ya England Barclays Pemier league. Sunderland ilimsaini Johnson kwa pauni 10m toka Manchester city mwaka 2012. Imeelezwa kuwa winga huyo mwenye mtoto mmoja amekuwa akipenda kushobokewa na wasichana na ni mpenda starehe wa hali ya juu.
Adam Johnson akiwa na mpenzi wake mwaka2012 Man City ilipotwaa ubingwa England. |
Hapa akishangilia goli dhidi ya watani wa jadi New Castle |
Hii ndio nyumba ambamo Adam Johnsona alikamatiwa na polisi wa Durham |
Imetafsiriwa na Mkala Fundikira
habari na picha mailonlinefootball