Winga Adam Johnson atuhumiwa kubaka binti mdogo!

Winga Adam Johnson atuhumiwa kubaka binti mdogo!

Mchezaji wa kiungo wa kilabu cha Sunderland Adam Johnson amesimamishwa na kilabu chake baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kujamiiana na msicha mwenye umri wa miaka (15).

Winga huyo mwenye miaka (27) anasadikika kupokea pauni 50,000 (Tsh milioni 1370) kwa wiki alikamatwa nyumbani kwake na polsi toka Durham katika hekalu lake lenye thamani pauni 1.8m mnamo siku ya jumatatu na baadae kupatiwa dhamana.

Kilabu cha Sunderland kimethibitisha kuwa kimemsimisha Johnson kupisha upelelezi, na hatua hiyo itaanza kazi jumanne ambapo Sunderland itacheza na Hull City katika mfululizo wa ligi kuu ya England Barclays Pemier league. Sunderland ilimsaini Johnson kwa pauni 10m toka Manchester city mwaka 2012. Imeelezwa kuwa winga huyo mwenye mtoto mmoja amekuwa akipenda kushobokewa na wasichana na ni mpenda starehe wa hali ya juu. 

Adam Johnson akiwa na mpenzi wake mwaka2012 Man City ilipotwaa ubingwa England.
Hapa akishangilia goli dhidi ya watani wa jadi New Castle
Hii ndio nyumba ambamo Adam Johnsona alikamatiwa na polisi wa Durham
Imetafsiriwa na Mkala Fundikira 
habari na picha mailonlinefootball