Showing posts with label Elimu. Show all posts
VYUO VYATAKIWA KUTOA ELIMU KULINGANA NA MAHITAJI YA AJIRA HAPA NCHINI
Na Woinde
Shizza,Arusha
VIJANA wengi wanaohitimu vyuo
hawapati kazi mara tu ya kuhitimu
masomo yao kutokana na kutokuwepo kwa vyanzo vya ajira vinavyokwenda
sambamba na ongezeko la wahitimu na kuchangia kuwepo kwa wimbi la
wahitimu wasiokuwa na ajira nchini.
Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na
utalii ,Selestini Gesimba alipokuwa akizungumza katika mahafali ya
tano ya Chuo cha Taifa cha Utalii(NCT) ,kampasi ya Arusha ambapo jumla
la wanafunzi 55 walihitimu fani za mapishi, uokaji,mapokezi,na
huduma
ya vyakula na vinywaji katika ngazi ya cheti.
Alivitaka vyuo mbalimbali kutoa elimu kulingana na mahitaji ya ajira
ili kuwezesha wanafunzi wanaohitimu kupata ajira kwa haraka na
hatimaye kuondokana na changamoto ya wimbi kubwa la wanafunzi
wanaohitimu na kukaa mtaani bila ajira.
Gesimba alitoa rai kwa vijana wa kitanzania kujiunga na Chuo cha Taifa
cha Utalii ili wapate ujuzi ambao utatoa fursa ya kufanya kazi kwenye
sekta ya utalii na pia fursa ya kuweza kujiajiri wenyewe.
‘sekta ya utalii nchini ni ya muhimu
sana na inapaswa kudhaminiwa
kwani imekuwa ikichangia asilimia 17.5 kwenye pato la Taifa na
kuifanya kuwa ya kwanza kwa kuingizia Taifa Dola bilioni mbili
ikifuatiwa na sekta ya madini ambayo imeliingizia Taifa Dola bilioni
1.7 mwaka 2004 .’alisema Gesimba.
Alisema kuwa, sekta hiyo ni miongoni mwa sekta inayokuwa kwa kasi
kubwa duniani ambapo imekuwa ikikua kwa asilimia 4.5 hadi 5 kwa
mwaka
ambapo imekuwa chachu ya kukuza na kuendeleza sekta nyingine za
kiuchumi kama kilimo, miundombinu , mawasiliano na usafiri pamoja na
kuwa kichochea kikubwa cha kupunguza umaskini katika jamii.
Naye Mtendaji Mkuu wa wakala wa chuo cha Taifa
cha Utalii ,Rosada
Msoma alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutoa mafunzo na
kuwaunganisha wanafunzi wake na fursa mbalimbali za ajira ambapo kwa
mwaka huu kati ya wanafunzi hao 55 tayari wanafunzi 21 wameshapata
ajira huku wengine wakiendelea kuitwa kwenye usahili maeneo
mbalimbali.
Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake,Neema Mollel alisema
kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu
wa jenereta pindi umeme unapokatika chuoni hapo, ukosefu wa hostel
changamoto inayosababisha wanafunzi wanaosoma mbali kutoweza
kuhudhuria kozi mbalimbali chuoni hapo.
Aidha waliomba chuo hicho kuwezeshwa zaidi na kuweza kutoa kozi
mbalimbali kwa ngazi ya diploma ili kuwawezesha wanafunzi wake kupata
elimu ya juu zaidi ambapo itawawezesha kukabiliana na changamoto ya
ajira ndani na nje ya nchi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ,Adoh Mapunda alisema kuwa,serikali
mkoani Arusha wapo tayari kushirikiana na chuo hicho katika kuboresha
huduma mbalimbali za masomo ili kuwezesha chuo hicho kukua zaidi na
kuendelea kutoa elimu iliyo bora zaidi.
Mapunda alikitaka chuo hicho kuboresha zaidi maswala ya hoteli ili
kuwavutia wateja wengi zaidi kuweza kujiunga chuoni hapo kutokana na
elimu nzuri ,na kuwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa
kukitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi kwa ujumla.
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA BAJAVERO DAR WAPATA MAFUNZO JUU YA HEDHI SALAMA.
Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko
ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama.
Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
Daktari
Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho
Wanafunzi wakiwa wanafundishwa moja ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya na Daktari
Edna Kiogwe.
Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Tano sita na saba wakiwa wanafurahia Jambo wakati wa mafunzo
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato wakifurahia Pads za
Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi
Duniani.
Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero,
Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia.
Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi huahirisha shughuli za kimasomo kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao
Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi.
Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na huwa wanadhani mwanamke peke yake ndio anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna
Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi huahirisha shughuli za kimasomo kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao
Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi.
Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na huwa wanadhani mwanamke peke yake ndio anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna
Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya Bajavero walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.
Habari na picha kwa niaba ya blogs za mikoa
Hanifa Fundikira ahitimu uzamili!
Bibi Hanifa Mdemu Fundikira akipozi nje ya Chuo kikuu cha Northampton nchini England baada ya kuhitimu. |
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)