Shangwe na burudani za kutosha zinatarajiwa kufanyika katika sikukuu ya Eid hapo kesho mkoani Tabora panapo majaaliwa ya M/Mungu. Mashabiki mbalimbali mjini Tabora watarajiwa kufurahia onesho hilo katika maeneo mawili tofauti ambapo mchana itakuwa Bwalo la Polisi kuanzia saa 8 mchana na Usiku katika viwanja vya Muungano Mesi kuanzia saa 2 usiku.
Wasanii wa kila nyanja wametua mjini hapo na kufanya mahojiano CG Fm Redio leo mchana; wasanii hao ni Kassim Mganga a.k.a tajiri wa mahaba, Ommy Dimpoz, Mkude Simba (Kitale) na rafiki yake Stan Bakora, Young Killer, na Baraka Da Prince.
Kassim Mganga akiwa CG Fm Redio, 89.5 The point of no Return
Ommy Dimpoz
Manoni (Mtangazaji CG Fm Redio 89.5 The Point of no Return) akifanya mahojiano na wasanii.
Mkudesimba Original (Kitale)
Kitale na Stani Bakora, ...eti "Tembo wa Ulaya mkubwa sana kama mbuzi"
Stan Bakora
Baraka Da Prince
Stephania (Mtangazaji CG FM)
Young Killer (Handsome aliyekosa matunzo) akishuka free style.
Mgalula Fundikira (Mkurugenzi wa Royal Nsyepa Entertainment) akizungumzia maandalizi ya onesho hilo aliloliandaa baada ya muda mrefu toka arudi kutoka Hispania
Kutoka kushoto, Kassim Mganga, Mubenga (Meneja wa Ommy Dimpoz), Stan Bakora na Abdul katika nyumba za Tabora Rest House walikofikia wasanii hao.
Wakijipima uwezo wa ukali wa "SAUM"
Picha na Aloyson -TBN Kanda ya magharibi