06/05/14

Kamati ya Miss Tanzania yatembelea kambi ya Redds Miss Dar Indian ocean!

Kamati ya Redds Miss Tanzania jana jioni ilifanya ziara katika kambi ya Redds Miss Dar Indian Ocean iliyopo katika Hoteli ya Chichi wilayani Kinondoni, jijini Dar. Ziara yao ilikuwa ni pamoja na kuwafunda warimbwende hao na kuwapa muda warembo hao wa kuuliza maswali kadha wa kadha. Kilele cha shindano hilo la Miss Dar Indian Ocean kitafanyika jumamosi tarehe 7/6/2014 katika viwanja vya Nyumbani Lounge. Warembo hao leo hii mchana watakuwa na pre judgement itafanywa na kamati ya Redds Miss Kinondoni chini ya muandaaji wa kanda hiyo Bw Innocent Melleck. Chini ni picha za tukio hilo
Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu Miss Tanzania Bw Hashim Lundenga, Mkuu wa itifaki na nidhamu Bw Albert Makoye na wakala wa Miss Kinondoni Bw Innocent Melleck katika
Katibu wa Miss Tanzania Bw Bosco Majaliwa na Bw Hashim Lundenga
Wakala wa zamani wa Miss Knondoni Bw Yusuf Omary aka Boy George akiwa na matron wa Miss Dar Indian Ocean Husna Maulid Miss Kinondoni no2 2011 
Baadhi ya warembo wa Kutoka kushoto Mariam Salum, Hasnat Hussein na Janet Geofrey wakimsikiliza Bw Hashim Lundenga, kamati ya Miss Tanzania ilipotembelea kambi yao jana jioni.
Wakala wa Miss Shinyanga Bi Asela Magaka
Wadau wa tasnia ya urembo 
Kutoka kushoto Albert Makoye, Innocent Melleck na Hidan Ricco(Afisa habari Miss Tanzania) 
Kutoka kushoto Miss Getrude Massawe, Sasha Deogratius, Camilla John, Suzzane na Shamila 
Tumepozi!

Mjumbe wa kamati Miss Dar Indian Ocean Bw Hassan Lema na wakala wa Miss Dar Indian Ocean Bibi Rahma Yusuph
Bibi Rahma Yusuph
Mshirki wa zamani wa Miss Tanzania, wakala wa Miss Geita na mjumbe wa Miss Tanzania Bw Lucas