07/31/13

Utamliliaje mtu leo, kesho umtukane?

OMMY Dimpoz akilia jukwaani baada ya kulemewa na majonzi ya kifo cha Ngwair tarehe 31/05/2013 Tabora.
Siku chache baada ya kifo cha Albert Mangwea (Ngwair) kulitokea  sintofahamu baada ya msanii Ommy Dimpoz kushutumiwa na gazeti moja la kidaku kuwa alimtukana Ngwair kuwa kafa masikini (kibwege) alipokuwa akipokea tunzo yake pale Milimani city katika kilele cha Kilimanjaro Music Awards. Ninachokumbuka alisema "Sisi wasanii wa Tanzania tumechoka kufa masikini huku tukiwa na majina makubwa" na akatoa wito kwa makampuni makubwa yawape kipaumbele wasanii wa Tanzania katika suala zima la promosheni za bidhaa zao kitu ambacho kitainua kipato cha wasanii wa Tanzania badala ya kutumia wacheza mpira wa nje kama Lionel Messi. Hali ilikuwa mbaya sana kwa Ommy Dimpoz huku akilaaniwa na kusiwa huku na kule na hasa katika mitandao ya kijamii. Kabla ya Kili Music Awards huko Tabora katika kilele cha Redds Miss Tabora 2013 Ommy alitoa kauli hiyo mbele ya Mh William Ngeleja na alimuomba awasaidie kupeleka kilio chao(wasanii) bungeni ili ziunde sheria nzuri zenye kulinda maslahi ya wasanii!