06/30/15

Kauli ya Sergio Ramos kuiambia Real Madrid anataka kujiunga na Manchester United yawakuna wengi!



Mlinzi mahiri wa kilabu cha Real Madrid Sergio Ramos amuambia uongozi wa kilabu hicho nguli kuwa anataka kujiunga na Manchester United na si vinginevyo kitendo hicho kimewapendeza mashabiki wengi wa soka hasa nchini England ambao wanaichukulia Real Madrid kama klabu onevu yaani inajiona yenye haki ya kuchukua mchezaji yeyote toka kilabu chochote na wakati wowote, kitu ambacho kimekuwa kikivikwaza vilabu vingine na hata mashabiki wao.
Kitendo cha mchzaji wao wa kutumainiwa Sergio Ramos kuamua kuondoka tena basi ili akajiunge na Man united ambao tayari wana machungu na Madrid kwa kuwachukulia Christiano Ronaldo na mbaya zaidi kumtaka goilikipa wao David de Gea. Vyombo kadhaa vya habari na magazeti ya michezo hasa ya England yameeleza kuudhiwa mno Louis Van Gaal kwa kwa kitendo cha Madrid kugoma kulipa pesa ambayo Man united ingependa Madrid wailipe kwa kuwaoka kipa bora zaidi duniani De Gea, lakini Madrid nao wanaona kwa nini walipe pesa nyingi kumnunua mchezaji ambaye mkataba wake umebakiza miezi 12 tu. Imeelezwa kuwa Man united wanataka Madrid iwalipe pauni milioni 33 huku Real Madrid wakiofa kulipa pauni milioni 10 tu. Kitu ambacho kimewaudhi Man united na wameelezwa kuwa tayari kumlazimisha De Gea amalize mkataba wake na aondoke bure kiangazi kijacho.

Real Madrid na wao sasa wanaonja joto ya jiwe toka kwa mchezaji wao, na Man united wanaitumia nafasi hiyo kuiteteresha Real Madrid. Duru zingine za habari zinaeleza kuwa hiyo ni janja ya Ramos kupata mkataba mpya na mnono toka Los Bloncos, imefahamika Ramos si mmoja wa wachezaji wanaolipwa vinono na Real Madrid hivyo anatumia mwanya huu ili kujipatia mshahara mnono.
Haya ni baadhi ya maoni ya baadhi wasabiki wa soka wengine si washabiki wa Man united lakini wanaonesha kukasirisha na kitendo cha Real kutaka wachezaji wa vilabu vingine huku wao wakigoma kuuza wao wanapotakiwa.

Habari na picha kwa hisani ya 
mailonline imefasiriwa na Mkala Fudikira