05/02/15

Mayweather amshinda Pacquiao kwa pointi na kuweka rekodi ya ushindi mara 48!

Floyd Mayweather akitua moja ya sumbwi kati ya mengi yaliyompa ushindi dhidi ya m Philipino Manny Pacquiao .

Lile pambano la kuvunja rekodi ki pesa zilizohusishwa kwa mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hatimaye limefanyika katika ukumbi wa MGM Grand garden arena jijini Las Vegas ambapo Money Mayweather aliibuka mshindi kwa pointi 118-110, 116-112 na 116-112 pamoja na kuwa Pacquiao kama ilivyotarajiwa na wengi alirusha ngumi nyingi lakini zisizo na mashiko yeyote katika maana ya kumuingizia pointi kwa upande mwingine Mayweather alicheza kiujanja na kuepuka ngumi za Manny lakini huku akijiingizia pointi kwa masumbwi yake ya moja kwa moja na kuwapendeza waamuzi.
Jamie Foxx akiimba wimbo wa taifa la Marekani, hata hivyo imeelezwa watumiaji wengi wa mtandao wa Twitter wakimshutumu aliuimba vibaya wimbo huo wa taifa 
Mayweather akipanda ulingoni huku akionesha sura yenye wasiwasi pamoja na kuwa alishinda pambano hilo.
nGail Banawis, akiwa na Word Chorale waliimba wimbo wa taifa la Phillipines,
Pacquiao akiingia ukumbini tayari kwa pambano
Pacquiao akirusha sumbwi la mwilini dhidi Mayweather
Pacquiao akipewa huduma wakati wa mapumziko.
Money akipewa maelekezo na mkufunzi wake
Money Mayweather akishangilia ushindi wake leo hii lakini mashabiki wengi nchini mwake walimbeza.
Floyd "Money"Mayweather akiwa na mikanda yake na mmoja alioushinda leo hii.
Ndege  binafsi za watu maarufu na wenye fedha zao zikiwa zimeujaza uwanja wa Las Vegas kabla ya pambano

Picha na habari kwa hisani kubwa ya mailonline