NYAWANA |Mama wa matashititi enzi za uhai wake
MULARD | MUME WA ZAMANI WA NYAWANA [CHANZO CHA PICHA]
Mwanamuziki maarufu wa Taarabu marehemu Nyawana Fundikira anatarajiwa kuzikwa kesho mchana au jioni kutegemeana na uwasili wa mwili wa marehemu mkoani Tabora. Ambapo baada ya kufanyiwa yale yote muhimu mkoani Dar mwili wake utasafirishwa kwa njia ya gari mpaka mjini Tabora kwa mazishi.
Mazishi yake yatafanyika kijijini kwao Itetemya yalipo makaburi na Ikulu ya familia ya kichifu ya Fundikira na Mtemi Isike Mwana Kiyungi. Nyawana Fundikira ambaye ameacha watoto wawili Said Murad (22) na Queen Murad (15) ambao alijaliwa kuwapata katika ndoa yake yake ya kwanza na Bw. Omar Khamis Murad (pichani). Murad mwanamichezo maarufu sana mjini Tabora ni meneja wa uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.